• ePaper
Sunday, October 11, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

HATIMAYE IMELIPA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 11, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
HATIMAYE IMELIPA
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

HATIMAYE kambi ya Simba iliyowekwa nchini Afrika Kusini imelipa, baada ya kuichapa Yanga kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Simba iliweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara, wakati wa mapumziko ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Hata hivyo, kambi hiyo.iliyowekwa Polokwane nchini Afrika Kusini imefanikiwa kulipa kisasi cha Simba kufungwa michezo mingi na Yanga katika miaka ya hivi karibuni.

Katika dabi za misimu mitatu iliyopita, Yanga imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Simba.

Yanga ilishinda 5-1 mzunguko wa kwanza na kuichapa Simba 2-1 mzunguko wa pili katika msimu wa 2023/24.

Baadaye ilishinda 1-0, huku ikiibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0 msimu wa mwaka 2024/25.

Vilevile msimu wa 2025/26, Simba ilishinda 1-0 katika Kombe la Muungano, huku dabi mbili za Ligi Kuu zikimalizika kwa sare ya 0-0 na 2-2.

Msimu huu, Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii.

Pambano la jana, lilianza kwa kasi ya kushambuliana pande zote, dakika ya tano ya mchezo, Yanga ilipata bao la kuongoza lililowekwa kimiani na mchezaji wake, Peter Shalulile kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Maxi Nzengeli na mpira kujaa wavuni.

Katika dakika ya 15, Simba walijibu shambulizi ambapo Elie Mpanzu alipata nafasi na kufumua shuti kali lililogonga mwamba.

Simba walionekana kulishambulia lango ya Yanga kama nyuki, dakika ya 28, Neo Maema alipata nafasi na kupiga shuti lililoishia mikononi mwa kipa, Djigui Diarra.

Staa wa Simba, Clatous Chama nusura aisawazishie timu yake bao baada ya kupiga shuti kali lililotoka sentimeta chache nje ya lango pasi ilitoka kwa Nathael Chilambo.

Dakika ya 44, Simba walifanya shambulizi la kushtukiza ambapo Mpanzu alipiga shuti akiwa nje ya eneo la hatari, kipa akaokoa, hadi mapumziko ya kipindi cha kwanza Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, dakika ya 49, Simba ilifanya shambulizi la kushitukiza, Nathaniel Chilambo alipiga shuti likatoka nje .

Simba walijipanga upya, dakika ya 67 Neo Maema aliwainua mashabiki wa klabu hiyo. katika viti baada ya kusawazisha bao la kwanza kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Libasse Gueye.

Wakitandaza kandanda safi huku wakipigiana pasi fupi fupi, Simba walipata bao la pili dakika ya 71, lililowekwa kimiani na Elie Mpanzu kufuatia kumtoka kipa Diarra na kuukwamisha mpira wavuni, hadi mchezo unamalizika Simba waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba imekwea kileleni kwa pointi 21 huku Yanga ikibakia na pointi zake 18, timu zote zimecheza mechi saba kila mmoja.

Katika msimu huu, Simba ilianza na ushindi Simba ilianza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, ikapata ushindi wa mabao mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji, ikaifunga tena mabao 2-1 Singinda Black Stars, ikashinda bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, ikapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold na kumaliza na Azam FC kwa kuifunga mabao 2-0.

Huku Yanga ikianza na ushindi wa mabao 3-1  dhidi ya Namungo FC, ikapata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Coastal Union, ikaufunga mabao 4-0 JKT Tanzania, ikaifunga Pamba Jiji mabao 2-0, ikaichapa Fountain Gate FC mabao 2-0 na kumalizia  Geita Gold kwa kuifunga bao 1-0.

Simba iliwakimishwa na Mamadou Kassali, Nathael Chilambo, Libasse Gueye, Antony Mligo, Rushine De Reuck, Clatous Chama, Neo Maema, Yusuph Kagoma, Ismael Toure, Elie Mpanzu na Anicet Oura.

Yanga: Djigui Diarra, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Maxi Nzengeli, Husseine Zakouani, Peter Shalulile, Yao Kouassi, Albert Kangwanda, Chadrack Boka, Mudathir Yahya na Duke Abuya.

Previous Post

TANZANIA NJIA NYEUPE MISS GRAND 2026

Next Post

RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

Next Post
RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JUKWAA LA WANAWAKE LAIBUKA  NA MAAZIMIO 10 KUHUSU AMANI

JUKWAA LA WANAWAKE LAIBUKA  NA MAAZIMIO 10 KUHUSU AMANI

10 months ago
MAAGIZO YA DK. MWINYI KWA WATUMISHI Z’BAR

MAAGIZO YA DK. MWINYI KWA WATUMISHI Z’BAR

12 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

    RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HATIMAYE IMELIPA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NJIA NYEUPE MISS GRAND 2026

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, YANGA ZAPIGWA ‘STOP’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?