• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DC HANANG’ AWATAKA VIONGOZI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KWA WAKATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 28, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DC HANANG’ AWATAKA VIONGOZI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KWA WAKATI
0
SHARES
20
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, Vita Rashid Kawawa, amewataka viongozi na watendaji wa wilaya hiyo kuwasikiliza wananchi, kushughulikia malalamiko yao na kutatua kero zinazowakabili kwa wakati, ili kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali na kuongeza uelewa kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kawawa ametoa agizo hilo leo Oktoba 28, 2026, akifungua mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kwa viongozi na watendaji katika Wilaya ya Hanang’, akisisitiza kuwa ni wajibu wa viongozi kuhakikisha wananchi wanasikilizwa, wanapewa majibu ya hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto wanazowasilisha katika maeneo yao.

Amesema kuwa usikilizaji wa wananchi na utatuzi wa changamoto zao ni miongoni mwa misingi muhimu ya utawala bora, inayosaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya Serikali na wananchi huku akiwataka viongozi kuwaeleza wananchi kuhusu kazi na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuongeza uelewa, ushiriki na imani yao katika shughuli za maendeleo.

Katika hatua nyingine, Kawawa amesisitiza umuhimu wa viongozi na watendaji kutoa kipaumbele kwa makundi yenye uhitaji maalumu, yakiwemo watu wenye ulemavu, wajane na wagane, kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki na kutendewa haki bila ubaguzi na kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma katika upatikanaji wa huduma.

Awali Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Idara ya Katiba na Ufuatiliaji wa Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Prosper Kisinini, amewataka viongozi na watendaji kutokata tamaa katika utekelezaji wa majukumu yao, huku wakizingatia misingi ya haki, uwajibikaji na utawala bora.

Kisinini amesisitiza kuwa watendaji wanapaswa kutenganisha migogoro binafsi na majukumu yao ya kikazi, pamoja na kuhakikisha kuwa maamuzi wanayoyafanya yanazingatia sheria, haki na usawa bila upendeleo wala kumuonea mtu yeyote.

Mafunzo hayo ni jitihada za serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria katika kuwajengea viongozi na watendaji uelewa wa misingi ya uraia na utawala bora, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuchangia utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili kufika Dira ya Maendeleo 2050.

Previous Post

WATAALAMU JIPANGENI TUPATE TRILIONI 7.3/ COP 31- MUYUNGI

Next Post

SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TPDC KATIKA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Next Post
SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TPDC KATIKA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TPDC KATIKA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

1 year ago
WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

2 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?