• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

TAIFA STARS HAKUNA KULALA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 30, 2025
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
TAIFA STARS HAKUNA KULALA
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

BAADA ya kuishia hatua ya robo fainali katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN 2024), timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’,  imeanza kufanya maandalizi ya kampeni ya kufuzu Kombe la Dunia.

Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), utakaopigwa Septemba 5, mwaka huu.

Baada ya mchezo huo, Stars itarudi dimbani kupambana na Niger ambapo pambano hilo limepangwa kufanyika  Septemba 9, mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan Complex,  Zanzibar.

Akizungumza jijini  Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema upande wa benchi la ufundi wanajiandaa kutangaza kikosi hicho.

Ndimbo amesema Kocha, Hemed Suleiman ‘Morocco‘ anatarajia kutangaza kikosi bora ambacho kitaenda kupambana kusaka alama sita katika mechi hizo mbili.

“Tumeanza maandalizi kwa mechi hizo mbili ambazo ni muhimu kwetu kocha anatarajia kutangaza kikosi kesho.

“Tuna imani kubwa kwamba timu yetu itafanya vizuri katika mechi hizo na kuipeperusha vyema bendera ya nchi,” alisema ofisa huyo.

Hata hivyo, Ndimbo aliipongeza Taifa Stars kwa  kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya CHAN 2024 kwani ni hatua kubwa na wameweka historia ya aina yake.

Amesema kuwa ana imani msimu ujao wa katika mashindano hayo, Stars itafika mbali zaidi na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

“Ukweli nachukua fursa hii kuwapongeza wachezaji wa  Taifa Stars kwa kujituma na kufika hatua ya  robo fainali ya CHAN 2024, tumepata uzoefu mkubwa na nina imani kuwa wataenda kufanya vizuri zaidi katika mechi zinazofuata,” amesema.

Ofisa huyo alisema anaishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kuanzia mashindano hayo yalivyoanza hadi kufikia tamati.

Previous Post

IBENGE ATAMBIA KIKOSI

Next Post

MAELFU WAZIDI KUMIMINIKA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA CCM DK. SAMIA

Next Post
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan

MAELFU WAZIDI KUMIMINIKA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA CCM DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAELEKEZO YA SERIKALI KUHUSU USAFI NA UPANGAJI VIZIMBA KIVUTIO MUHIMU

MAELEKEZO YA SERIKALI KUHUSU USAFI NA UPANGAJI VIZIMBA KIVUTIO MUHIMU

1 month ago
AJIRA 45,000 ZANUKIA

AJIRA 45,000 ZANUKIA

3 days ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?