• ePaper
Friday, May 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

‘MIFUMO YA UUZAJI MAZAO YA WAKULIMA, WAIMARISHWA’

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 11, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
‘MIFUMO YA UUZAJI MAZAO YA WAKULIMA, WAIMARISHWA’
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Singida

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imeendelea kuboresha mifumo ya kuuza mazao ya wakulima.

Amesema lengo kuu ni kuhakikisha usafirishaji mazao na kuondoa madalali waliokuwa wakimnyonya mkulima.

Dk. Samia, aliyasema hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika juzi uwanja wa Bombadia mkoani Singida.

“Hatua hiyo ya kubadili mifumo, imesaidia kuongeza uwazi, kwa mfano mwaka jana, wastani wa bei ya mkulima, ilifika asilimia 70 ya bei ya soko la dunia, alipata mkulima hapa Tanzania,” alisema.

Aliongeza: “Nafahamu zipo changamoto za wanunuzi kuchelewesha malipo badala ya kulipa ndani ya saa 48, wanachukua siku tatu hadi nne, nataka niwaambie tayari serikali imechukua hatua.”

Alizitaja hatua hizo ni kuwafutia leseni wanaohujumu mfumo huo, ikiwemo wanaoweka uchafu katika mazao na wanaonunua nje ya mfumo.

“Hawatapatiwa tena kibali cha kuuza nje, yaani hao ndiyo wamejiondoa katika soko ila hapa kuna ombi la mgombea ubunge wa Ilongelo (Haidary Gulamali) kwamba, dengu zipo ghalani unatuambiaje.

“Nataka kusema kwamba, tunahangaika kutafuta masoko, wakulima wenye mazao tulieni, tutatoa vibali vya kusafirisha nje kwa wale ambao tutawapa vibali, lakini bado tunahangaika kutafuta soko la dengu na mbaazi,” alisisitiza.

Alisema serikali ipo katika mazungumzo, yamefikia pazuri, hivyo bei haitashuka chini ya soko la dunia.

Dk. Samia, alisema mwaka huu, uzalishaji umekuwa mkubwa duniani, hata nchini uzalishaji wa mbaazi na dengu umeongezeka.

“Kwa ujumla, bei ya dunia imeshuka, lakini tupo katika mazungumzo.

“Pamoja na hayo, bado bei ya mnadani katika stakabadhi ghalani ni bora zaidi kuliko bei ya madalali. Hatutashuka chini ya asilimia 60 ya bei ya soko la dunia,” alisisitiza.

Aliwataka wafanyabiashara kuheshimu mifumo ambayo serikali imeamua kwenda nayo, huku akiwahakikishia wakulima kwamba, serikali itaendelea kuboresha mifumo ya kuuza mazao.

Vilevile, alisema mfumo wa ushirika utapitiwa upya ili uwe wenye tija zaidi kwa mazao hayo.

Previous Post

DK. BASHIRU AELEZEA UJASIRI WA DK. SAMIA

Next Post

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

Next Post
TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

5 months ago
WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

8 months ago

Popular News

  • MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?