• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWINYI AFAFANUA MSINGI WA MAENDELEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 19, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. MWINYI AFAFANUA MSINGI WA MAENDELEO

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi

0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na HANIFA RAMADHANI, 

Zanzibar

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema msingi wa maendeleo ya nchi yoyote duniani, unatokana na amani, umoja, mshikamano na maridhiano.

Amesema kutokana na hilo, alipoingia madarakani mwaka 2020, jambo la kwanza aliloimarisha, lilikuwa mshikamano, maridhiano na kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Dk. Mwinyi, alisema hayo, katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika Viwanja vya Mnarani, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema bila ya amani, umoja, mshikamano na maridhiano, hakuna jambo lolote la maendeleo litakalofanyika nchini.

Mgombea huyo, alisema hiyo ndiyo sera mama kwa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, hivyo aliwahimiza wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani wanaposimama majukwaani, waendelee kuhimiza suala hilo, kila dakika nchi iendelee kuwa na amani na kukua kimaendeleo.

Akizungumzia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2025, Dk. Mwinyi, alisema Chama kiliinadi kwa wananchi miaka mitano iliyopita, wameitekeleza kwa asilimia kubwa, hivyo kuwaonesha kwa vitendo  kwamba, CCM ikiahidi, inatekeleza.

“CCM ni Chama imara, kwani tuliahidi tumetekeleza na kuvuka Ilani yetu, ninawaahidi miaka mitano ijayo, yajayo ni neema zaidi,” aliahidi.

Aliwasisitiza wanachama wa CCM na wananchi, kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu na kukichagua Chama, kipate ushindi wa kishindo.

“Hamasa za kujitokeza kwa wingi katika mikutano ni jambo moja, lakini uchaguzi ni kupiga kura, tuhakikishe tunajitokeza kwa wingi, Chama kishinde kwa kishindo,” alisisitiza.

Dk. Mwinyi, alimwombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia, yeye na wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani wa CCM.

Naye, Mgombea Uwakilishi kupitia nafasi za wanawake, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Riziki Pembe Juma, aliwasisitiza wananchi, kuendelea kutunza amani, kwani ndiyo inayowaletea mafanikio na kutambua ikipotea,  kinamama na watoto ndiyo wanaohangaika.

Alisema kinamama, wamejipanga kuhakikisha wanasaka kura kwa kuwatoa watu majumbani, kwenda kuipiga kura CCM iendelee kushinda kwa kishindo.

Kwa upande wake, Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kijini, Badria Attai Masoud, alimpongeza Dk. Samia kwa kudumisha Muungano na kuondoa hoja zaidi ya 15, huku akitekeleza miradi ya maendeleo.

Pia, alimpongeza Dk. Mwinyi kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa asilimia kubwa, ukiwemo ujenzi wa barabara zinazokwenda Kijiji cha Kijini.

Previous Post

WASIRA AZUNGUMZIA FAIDA ILANI YA CCM

Next Post

NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

Next Post
NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

11 months ago
MRATIBU ACT ATOBOA SIRI KUJIUNGA CCM

MRATIBU ACT ATOBOA SIRI KUJIUNGA CCM

10 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?