• ePaper
Saturday, June 6, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 3, 2025
in Habari, Kitaifa
0
SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameeleza namna alivyowasaidia wanasiasa waliokuwa wamekimbilia nje ya nchi na kusema kwamba, siasa siyo kuharibu nchi, kubezana na kutukanana, bali ni uungwana. 

Pia, amesema kwa dhamira ya kujenga nchi, alianzisha upatanishi na vyama vya upinzani kwa kufanikisha waliokuwa nje, kurejea na kufutiwa kesi zilizokuwa zikiwakabili.

Akilihutubia taifa jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo, Rais Dk. Samia alisema baada ya kuingia madarakani, alitoa fursa muhimu kwa vyama vya siasa, ikiwemo kufanya mikutano na shughuli za kisiasa baada ya kuzuiwa miaka saba. 

“Siasa siyo kutukanana, siyo kubezana, siasa siyo kuharibu nchi. Wazee wetu wa zamani ukiwa na harakati hizo walikuwa wanasema huyu hajui siasa, siasa maana yake ni usalama na uungwana.

“Mwaka 2020 hadi 2023 nilifanya kazi kubwa ya kuzungumza nao nikanyoosha mkono wa rehema njooni Watanzania, njooni tukae tukazungumze yetu.

“Nikidhani nawanyooshea Watanzania mkono wa rehema na wataupokea watakuja tukae vizuri ni hawa hawa niliowakuta nje wana ‘suffer’ (wanahangaika) hawana hata shilingi, nikatoa kiposho changu nilichogawiwa cha safari nikawapa waendelee na maisha wakiwa nje,” alisema.

Aidha, Rais Dk. Samia alisema serikali haikuzuia chama chochote cha siasa kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu, ambapo chama ambacho hakikushiriki kilijiondoa baada ya kuona dalili za kushindwa na mipasuko waliyokuwa nayo.

ATOA NENO KWA VIONGOZI WA DINI

Aidha, Rais Dk. Samia aliwaomba viongozi wa dini kusimama na kutekeleza majukumu yao, kuhakikisha hawatumiki kuvuruga nchi.

Dk. Samia alisisitiza iwapo kuna jambo lolote, njia sahihi za kukaa na kufanya mazungumzo zipo ambazo ni kukaa na kujadiliana.

Alibainisha hakuna eneo baya la kumpata mwananchi kama ndani ya dini, kwani mtu anapolishwa maneno kupitia dini inabaki ndani ya moyo tofauti na siasa ambayo huingia akilini na baadaye kuondoka baada ya jambo zuri kuja.

“Viongozi wetu wa dini kaeni katika mstari wenu, dini zetu zote zinasema kila mamlaka imeletwa na Mungu iwe kuna mwanamke, mwanaume na sababu ya Mungu kuleta mamlaka hiyo hakuna anayeijua,” alisema.

Vilevile, Rais Samia alisema ubora wa dini uko mioyoni mwa waumini na kusisitiza nchi haitaendeshwa na madhehebu ya dini, kwani serikali haina dini.

Aliongeza hakuna kitabu cha dini kinachosema dini zitatumika kuvuruga nchi, ila ni utashi wa watu binafsi ambao hutumia vivuli vya dini.

“Msivae majoho ya dini kutengeneza utashi wenu binafsi kupitia vivuli vya dini niwaombe sana viongozi wa dini tusimame tusivuruge nchi yetu,” aliongeza.

Rais Dk. Samia alieleza serikali itaendelea kusimama na kuilinda nchi kwa nguvu zote.

Previous Post

VIONGOZI SIMBASC WATAKIWA KUJITATHMINI

Next Post

MENEJA PANTEV ATIMULIWA SIMBASC

Next Post
MENEJA PANTEV ATIMULIWA SIMBASC

MENEJA PANTEV ATIMULIWA SIMBASC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM Z’BAR YAAHIDI KAMPENI ZA KISTAARABU

CCM Z’BAR YAAHIDI KAMPENI ZA KISTAARABU

9 months ago
DK. SAMIA, AHIMIZA WAKULIMA WAJISAJILI KATIKA MFUMO WA RUZUKU YA MBEGU, PEMBEJEO

DK. SAMIA, AHIMIZA WAKULIMA WAJISAJILI KATIKA MFUMO WA RUZUKU YA MBEGU, PEMBEJEO

9 months ago

Popular News

  • MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WFP KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USIMAMIZI WA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?