• ePaper
Sunday, May 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 8, 2025
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI
0
SHARES
20
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Andrew Lentz, pamoja na mambo mengine wamejadili ushirikiano wenye faida kwa nchi zote mbili.

Mkutano huo kati ya Rais Dk. Samia na Kaimu Balozi Lentz ulifanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma  huku wakiazimia kuendeleza ushirikiano wenye manufaa ya pamoja na kuendeleza mikataba ya ushirikiano baina ya mataifa hayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, katika mazungumzo hayo Balozi Lentz, ambaye aliambatana na Kamisaa wa Siasa na Masuala ya Uchumi wa ubalozi huo, alielezea dhamira ya Marekani katika kuendeleza uhusiano katika nyanja ya uchumi, siasa na usalama baina ya mataifa hayo mawili.

 “Marekani imedhamiria siyo katika ushirikiano tegemezi wa misaada, bali wenye manufaa kwa mataifa yote mawili,“alifafanua Kaimu Balozi Lentz.

Sehemu ya taarifa hiyo ya Ikulu iliongeza, mkutano huo ulihusu majaliano yaliyojikita katika miradi ya kimkakati ya Marekani na Tanzania ambayo iko kwenye majadiliano.

MIRADI YA KIMKAKATI

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, pande zote mbili zinatambua mchakato wa majadiliano wa miradi hiyo kati ya Marekani na Tanzania ukiwemo wa  gesi asilia (LNG), mradi Tembo Nickel, ambayo yote iko katika hatua za mwisho za kusubiri utiaji saini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, mradi wa tatu uliojadiliwa ni wa machimbo ya madini ya Graphite, uliopo Mahenge, mkoani Morogoro ambao bado unafanyiwa kazi.

RAIS DK. SAMIA

Kwa upande wake, Rais Dk. Samia alipongeza dhamira ya Marekani na kuahidi kwamba Tanzania iko tayari kuhakikisha hatua zilizosalia katika miradi hiyo zinakamilishwa. 

 “Kama nchi isiyofungamana na upande wowote, iko wazi, tayari na imedhamiria kushirikiana na wadau wote ambao wanaheshimu uhuru wetu na maono yetu kwa ustawi wetu,” alisema Rais Dk. Samia.

“Miradi hii ya kimkakati ina umuhimu mkubwa kwa taifa na tumedhamiria kuikamilisha kwa ajili ya kutoa ajira, uwekezaji na ustawi endelevu wa watu wetu,”alisisitiza Rais Samia.

Rais Dk. Samia alitaja kampuni 400 za Marekani zinazofanya kazi nchini  kwamba ni uthibitisho wa umadhubuti, uwazi na ushirikiano wa kiuchumi wa muda mrefu na Marekani.

Mbali na uwekezaji, mazungumzo hayo yaligusia kwa kina masuala ya ushirikiano likiwemo la utulivu wa kisiasa, usalama wa kikanda, mageuzi ya kiuchumi, ukuaji wa sekta binafsi, sekta ya afya na uhusiano kati ya raia wa mataifa hayo mawili.

KAIMU BALOZI LENTZ

Kaimu Balozi Lentz, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa maono na mipango yake madhubuti kupitia Dira ya ya Taifa ya Maendeleo 2050, na kusisitiza kwamba serikali ya Marekani iko tayari kusaidia utekelezaji wake huku akielezea kuguswa na Falsafa ya 4R katika uongozi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, pande zote mbili zilikubaliana kuimarisha mawasiliano ya mara kwa mara na kuchukua hatua kwa wakati katika utekelezaji wa makubaliano kwa lengo la kuondoa vikwazo katika ushirikiano baina ya mataifa hayo.

THAMANI YA MIRADI

Mradi wa LNG unakadiriwa kuwa thamani ya Dola za Marekani bilioni 42, ambao ukikamilika utazalisha maelfu ya ajira, kukuza pato la taifa na kuifanya Tanzania kuwa msafirishaji mkubwa wa LNG duniani.

Tembo Nickel ni mradi wenye thamani ya Dola milioni 942 million, uliopo Ngara, Kagera unahusisha madini muhimu ya utengenezaji wa betri za magari ya umeme, utakaochochea ukuaji wa viwanda, kusaidia usambazaji wa nishati safi duniani na kuongeza mapato ya mauzo ya nje.

Mradi wa Mahenge Graphite wenye thamani ya Dola za Marekani  milioni 300, ni moja ya miradi mikubwa duniani utakuza uzalishaji wa betri, nishati jadidifu na kuiweka Tanzania katika nafasi ya kuwa kinara wa usambazaji wa  madini hayo yanayotumika kutengeneza betri duniani.

Previous Post

TULIENI NYUMBANI

Next Post

RAIS DK. SAMIA AWATAKIA HERI WATANZANIA MIAKA 64 YA UHURU

Next Post
RAIS DK. SAMIA AWATAKIA HERI WATANZANIA MIAKA 64 YA UHURU

RAIS DK. SAMIA AWATAKIA HERI WATANZANIA MIAKA 64 YA UHURU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BIL. 36.6/- ZAPAISHA UCHUMI WA VIJANA

BIL. 36.6/- ZAPAISHA UCHUMI WA VIJANA

5 months ago
DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

5 days ago

Popular News

  • MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?