• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MWAMENGO, DEPU WANUKIA YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 24, 2025
in Burudani, Michezo
0
MWAMENGO, DEPU WANUKIA YANGA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

IKIBAKI wiki moja kabla ya dirisha dogo la usajili  katika Ligi Kuu Tanzania Bara kufunguliwa, klabu ya Yanga inakaribia kunasa saini za washambuliaji Emmaniel Mwanengo na Laurindo Depu.

Mwamengo raia wa Tanzania anayekipiga TRA United na Muangola Depu kutoka Radomiak Radom ya Poland, wanatakiwa na Yanga kuboresha kikosi kwa michuano ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu huu.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Yanga imepanga kuwanasa nyota hao na wengine huku ikilenga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya nyota wake, kusalia na kikosi ambacho kitakuwa tishio.

UHURU ilipomtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, aligoma kuwazungumzia wachezaji hao huku akisema klabu tayari imeshaanza kufanyia kazi ripoti ya kocha wake, Pedro Goncalves.

Kamwe amesema viongozi wao tayari wapo mawindoni kutafuta wachezaji ambao mwalimu anawahitaji.

Amesema Pedro ataongeza wachache ili kuboresha timu katika nafasi ambazo ameona zina mapungufu kufanya vizuri katika mechi zinazokuja.

 “Sisi tutafanya usajili mapema zaidi kukimbizana na muda, tunataka tukimsajili mchezaji acheze mechi inayofuata dhidi ya Al Ahly ya Misri, siyo kusubiri taratibu, sijui vibali, kama yupo anasajiliwa moja kwa moja anakwenda katika mazoezi,” amesema Kamwe.

Yanga inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 16 katika mechi sita, ikishinda mechi tano na kutoka sare moja.

Katika CAFCL, Yanga ipo nafasi ya pili katika kundi B ikiwa na pointi nne baada ya kushuka dimbani mara mbili, ikishinda mechi moja na kutoka sare moja.

Timu hiyo ipo sawa na kinara Al Ahly ya Misri zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, AS FAR Rabat ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria zikifuatia kila moja ikiwa na pointi moja.

Yanga ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR nyumbani kabla ya kutoka suluhu dhidi ya JS Kabylie ugenini.

Previous Post

BARKER APEWA WATATU SIMBA

Next Post

MOURINHO WA YANGA PRINCESS AFUNGUKA

Next Post
MOURINHO WA YANGA PRINCESS AFUNGUKA

MOURINHO WA YANGA PRINCESS AFUNGUKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA NI KIONGOZI MWENYE NGUVU KUIVUSHA TANZANIA – CHONGOLO

DK. SAMIA NI KIONGOZI MWENYE NGUVU KUIVUSHA TANZANIA – CHONGOLO

11 months ago
KOCHA GAMONDI AJIVUNIA TAIFA STARS

KOCHA GAMONDI AJIVUNIA TAIFA STARS

9 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?