• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KIPA NIGERIA ASHUSHA PRESHA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 16, 2025
in Burudani, Michezo
0
KIPA NIGERIA ASHUSHA PRESHA

KIPA wa timu ya Taifa ya Nigeria,  Stanley Nwabali

0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

CAIRO, Misri

KIPA wa timu ya Taifa ya Nigeria,  Stanley Nwabali ameshusha presha baada ya benchi la ufundi baada ya kujiunga na timu hiyo nchini Misri.

Nigeria imeweka kambi yake nchini humo kujiandaa na michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) inayotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, mwaka huu.

Timu hiyo imepangwa kundi C ikiwa na timu za Tunisia, Uganda na Tanzania huku mechi zote za makundi zikipangwa kuchezwa huko Fes.

Ujio wa Nwabali umeongeza mzuka katika kitengo cha makipa wa Nigeria ambapo mlinda mlango huyo ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho.

Nwabali aliwasili na kuondoa wasiwasi wa hivi karibuni, kufuatia kukutwa na tatizo la kifundo cha mguu, pia jeraha la mkono ambalo likiripotiwa kuhitaji kufanyiwa upasuaji.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, hajacheza ndani ya kikosi cha timu ya Chippa United tangu mchezo wa Nigeria dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Nigeria itaingia katika AFCON 2025 ikiwa katika nafasi ya  nne kwa ubora wa soka Barani Afrika.

Pia, timu hiyo inashika nafasi ya 38 ya viwango vya ubora duniani kote.

Nigeria imewahi kutwaa taji la AFCON, mwaka 1980, 1994 na 2013.

Imewahi kushika nafasi ya pili ya michuano hiyo ya AFCON mara 5 na imewahi kucheza fainali za Kombe la Dunia mara sita.

Timu hiyo imeelezwa kuwa ina kikosi chenye thamani zaidi ya Euro milioni 280.

Kikosi hicho kina jumuisha nyota kama Victor Osimhen, Ademola Lookman, Alex Iwobi, Calvin Bassey na Wilfred Ndidi.

Wakati huo huo, Nigeria leo itacheza mechi wa kirafiki dhidi ya Misri utakaopigwa Uwanja  wa Kimataifa wa Cairo  nchini Misri.

Misri  katika michuano ya AFCON 2025 imepangwa kundi B  ikiwa na timu za Zimbabwe, Afrika Kusini na Angola.

Previous Post

TRA UNITED KAZI KAZI

Next Post

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

Next Post
OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

IBENGE FURAHA TELE

IBENGE FURAHA TELE

2 months ago
KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

1 month ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?