• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NDOTO YATIMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 1, 2026
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
NDOTO YATIMIA
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

> Hatua kwa hatua Stars ilivyovunja mwiko wa AFCON 1980, 2019 na 2023

> Gamondi aweka rekodi ‘bab kubwa’ 

> Waliocheza AFCON miaka 45 iliyopita wafunguka

AMINA KASHEBA Na NASRA KITANA

WAKATI ndoto ya Watanzania kuishuhudia Taifa Stars ikicheza hatua ya mtoano Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ikikamilika juzi, Kocha wa timu hiyo ya taifa, Miguel Gamondi, amevunja mfupa uliowashinda makocha wa ndani na nje kwa zaidi ya miaka 45.

Taifa Stars ilikamilisha ndoto hiyo kwa kanuni ya ‘best looser’ baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika kundi C la AFCON 2025 ikiwa na alama mbili kufuatia kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia katika mtanange wa mwisho wa makundi uliopigwa Uwanja wa Prince Moulay Abdellah jijini Rabat, Morocco.

Timu hiyo itashuka dimbani Jumapili kuvaana na Morocco katika hatua ya 16 bora itakayochezwa Uwanja wa Prince Moulay Abdellah.

Ikiwa moja kati ya miamba 16 itakayocheza mtoano, mafanikio hayo yameifanya Stars kuweka rekodi hiyo kwa mara kwanza huku Muargentina Gamondi akivunja mwiko uliowashinda makocha watano tofauti waliowahi kuinoa timu hiyo.

Makocha hao ni Mpoland Slawomir Wolk aliyeinoa Stars kaitka fainali za mwaka 1980, Emmanuel Amunike raia wa Nigeria (2019), Adel Amrouche kutoka Algeria na Mtanzania Hemed Morocco katika fainali za mwaka 2023, ambao wote vikosi vyao viliishia makundi.

Mwaka 1980, Wolk aliiongoza Taifa Stars katika mechi tatu ikifungwa mbili na kutoka sare moja wakati mwaka 2019 Mnigeria Amunike aliiongoza Stars kufungwa mechi zote tatu na kuburuta mkia.

Katika fainali za mwaka 2023, Taifa Stars chini ya Amrouche na baadaye Morocco, ilimaliza nafasi ya tatu kwa alama mbili, ikifungwa mechi moja na kutoka sare mbili.

Amrouche aliiongoza Stars katika mechi moja ambayo ilipoteza kabla ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na nafasi yake kukaimiwa na mzawa Morocco ambaye aliiongoza kupata sare mbili na kurejea nyumbani.

Akizungumza kutoka Morocco, Kocha Gamondi, alisema kujituma kwa wachezaji wake dhidi ya ubora wa wachezaji wa Tunisia ndiyo sababu muhimu ya kutopoteza mechi hiyo.

Kocha huyo alisema ana imani ubora waliouonyesha wachezaji wake juzi utaendelea katika mchezo ujao dhidi ya Morocco kuhakikisha wanatinga robo.

WALIOKIPIGA 1980 WAFUNGUKA

Wakizungumzia mafanikio ya Stars na ubora wa Gamondi, wachezaji wa soka ambao walikipiga Taifa Stars katika fainali za 1980, wametoa maoni tofauti tofauti.

Beki wa Taifa Stars katika fainali hizo, Leopard Mukebezi ‘Taso’, aliipongeza timu hiyo kwa kuweka historia hiyo huku akimwagia sifa nyingi kocha Gamondi kwa kuiongoza vyema miamba hiyo.

“Pongezi kwa Stars kwa kupambana kwa jasho na damu, wameweka rekodi ya kipekee. Lakini katika mechi dhidi ya Morocco utulivu unapaswa kuwa mkubwa zaidi tufanikiwe zaidi na zaidi,” alisema.

Gwiji huyo alisema soka la sasa linahitaji zaidi mbinu, maarifa na kujituma tofauti na enzi zao ilihitajika zaidi kipaji, hivyo Taifa Stars iongeze juhudi kufanya vyema zaidi.

Aliyekuwa mshambuliaji katika kikosi hicho, Sunday Manara maarufu Computer, alisema wachezaji kuwa watulivu zaidi katika kusikiliza mbinu za Gamondi watakapovaana na Morocco.

Makipa Idd Pazi na Juma Pondamali, waliweka wazi kwamba ni jambo bora kuona Taifa Stars ya sasa ikiwemo rekodi hiyo japokuwa fainali ya mwaka 1980 ilikuwa ngumu zaidi kufanya hivyo.

“Hivi sasa wana raha maana kipindi chetu inakwenda timu moja, hivyo mnapaswa kupambana kwa jasho na damu kuhakikisha mnavuka. Lakini pongezi kwa kocha Gamondi kuwa sehemu ya historia na nafikiri anapaswa kupewa mkataba rasmi,” alisema.

Naye Pondamali alisema: “Hivi sasa wachezaji wanapata raha kwa sababu mpira ndiyo sehemu ya maisha yao kiujumla tofauti na sisi tulikuwa tunafanya na kazi nyingine, pia sasa hamasa imekuwa kubwa kiasi kwamba wanakuwa na mwamko wa kupambana,”.

SAMATTA, FEI TOTO

Nahodha Mbwana Samatta ambaye alikipiga katika timu hiyo fainali za 2019, 2023 na sasa, alisema amefurahia kuwa sehemu ya historia hiyo kubwa.

 “Ninafuraha kuiongoza timu kuvuka hatua nyingine, hii inaonyesha Tanzania tunaendelea katika soka hasa timu ya taifa, tutaendelea kupambana tufike mbali zaidi,” alisema.

Naye Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye alikipiga katika AFCON za 2019, 2023 na sasa, alisema kila mchezaji anajivunia kuwa sehemu ya historia hiyo.

 “Tumeweka historia kubwa na tunajivunia, kila mchezaji alipambana kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema.

SAFARI YA MABILIONI

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), michuano ya AFCON inatarajiwa kutumia dau la dola za Marekani milioni 32 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 78.3 za Tanzania kwa ajili ya zawadi pekee.

Katika mchanganuo wa fedha hizo, bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kuvuna dola za Marekani milioni saba ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 17.1.

Timu itakayoshika nafasi ya pili itavuna dola za Marekani milioni nne ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 9.7 za Tanzania.

Timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali, kila moja itaondoka na dola za Marekani milioni 2.5 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 6.1 za Tanzania.

Timu nne zitakazoishia hatua ya robo fainali zitavuna dola za Marekani milioni 1.3 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 3.1 za Tanzania.

CAF pia imeeleza kwamba, miamba minane itakayoishia hatua ya 16 bora itavuna dola za Marekani 800,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.9 za Tanzania.

Timu zitakazoishia nafasi ya tatu katika kundi, kila moja itaondoka na dola za Marekani 700,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.7 wakati zile zitakazoburuta mkia katika kila kundi zitavuna dola za Marekani 500,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.2 za Tanzania.

Previous Post

UJUMBE WA KILAINI, ANNA ABDALLAH MWAKA 2026

Next Post

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

Next Post
RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

6 months ago
STEVE NYERERE, WEMA SEPETU WAMLILIA LUKUVI

STEVE NYERERE, WEMA SEPETU WAMLILIA LUKUVI

1 month ago

Popular News

  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?