• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 14, 2026
in Makala, RIPOTI MAALUMU
0
‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’
0
SHARES
18
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST

“BODA boda kwangu ni zaidi ya kazi, kwani inanipa uhakika wa kipato kwa siku na kuweka akiba yangu ya maendeleo, imekuwa mkombozi mkubwa wa kiuchumi,

Ni ajira inayoniweka mjini, kwa kuwa ndiyo tegemeo langu katika uendeshaji wa maisha ya familia yangu,”.

Hiyo ni kauli ya Mwendesha pikipiki wa Mnazi Mmoja, Nasri Kassim, aliyezungumza na mwandishi wa makala hii kuhusu usafirishaji wa abiria kwa pikipiki maarufu bodaboda.

 Alisema shughuli hiyo ya usafirishaji imewasaidia vijana wengi kuachana na vikundi vibaya kujikita katika kazi hiyo halali na kuachana na zile zisizo faa.

Kassim alimweleza mwandishi kwamba kabla ya kazi hiyo, hakuwa na kazi ya kueleweka, alikuwa anabahatisha tu pa kupata riziki ya siku, hakuwa na uhakika wa kiuchumi.

Mwendeshaji wa pikipiki, Kituo cha Abiola, Dar es Salaam, Johnson Mutta, alisema sababu ya ongezeko la pikipiki ni upatikanaji wake kuwa mwepesi zaidi,kwani wauzaji wake wamekuwa wengi na wanazitoa kwa mikopo kuanzia kiasi cha sh. 150,000, na kila wiki unapeleka marejesho.

Alisema kwa hali hiyo ndiyo maana vijana wengi wamekuwa na wepesi wa kumiliki pikipiki na kusababisha ongezeko kubwa mjini, kwani kijana akiipata kwa mkataba ndani ya miaka miwili inakuwa ya kwake.

Alieleza kuwa, bodaboda zimewasaidia kwa kiasi kikubwa vijana katika kujikwamua kiuchumi kwani kabla ya hapo, vijana wengi akiwemo yeye walikuwa hawana ajira.

“Mfano mimi kabla ya kuanza kuendesha bodaboda, nilikuwa sina ajira ya kufanya, nilikuwa nakaa kijiweni na kufanya vibarua vidogo vidogo ambavyo havikuwa na tija, lakini kwa sasa kupitia chombo hiki cha usafiri kwa siku napata faida kuanzia  sh. 30,000 na zaidi.

“Boda boda imenisaidia kuendesha familia yangu kwa maana ya kuoa na kusomesha watoto wangu wawili, naheshimu kazi hii na kuipenda kwa sababu inaongoza maisha yangu na imenijengea heshima katika jamii,”alisema.

Usafiri wa pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ na bajaji umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wengi, kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Mfano kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mji, hutumia usafiri huo kuwahi majukumu yao hasa wale wanaofanyia katikati ya miji, huwasaidia kuwahi kuliko magari binafsi na yale ya usafiri wa umma.

ONGEZEKO LA PIKIPIKI NA BAJAJI

Akielezea idadi ya pikipiki na bajaji zilizosajiliwa kwa mwaka jana, Mtakwimu  wa Usajili wa Leseni za Vyombo vya Usafirishaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), Nicolaus Kamzora, alisema idadi ya leseni zilizotolewa za pikipiki na bajaji kuanzia Julai 2024 hadi Juni mwaka jana, zimevuka lengo kusudiwa.

Alisema kuna ongezeko kubwa la vyombo hivyo vya usafiri nchini, ambavyo hutumika maeneo mengi ikiwemo katikati ya miji.

Kamzora alisema kwa mwaka jana, ya leseni za pikipiki 53,191 zimesajiliwa sawa na asilimia 97 ya malengo yao ya kufikia leseni 55,000 nchi nzima.

Katika usajili wa Bajaji alisema kwa mwaka jana, walisajili leseni 22,629 sawa na asilimia 87 ya lengo la kusajili leseni 26,0000.

Alieleza leseni zote za bajaji na pikipiki na zilizosajiliwa ni 75,820, sawa na asilimia 94, lengo ikiwa kufikia leseni 81,000.

MIKOA YENYE BAJAJI NA PIKIPIKI NYINGI

Akieleza majiji yenye idadi kubwa ya leseni za pikipiki na bajaji aliutaja Mkoa wa Mbeya, kuongoza kwa kuwa na pikipiki17,172 na bajaji 3,738  hivyo kufanya jumla ya 20,910.

Kamzora alisema Mkoa wa Dodoma ulikuwa na leseni za pikipiki 7,156 na bajaji 1,227 ambapo jumla  yake ni 8,383.

Katika Mkoa wa Mwanza ulikuwa na jumla ya leseni za pikipiki zilizosajiliwa 6,111 na bajaji 816 jumla yake ni 6,927.

Vilevile, Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na leseni za pikipiki 2,795 na bajaji 3,803 jumla ni 6,598.

Kwa wingi wa vyombo hivyo vya usafiri katika mikoa hiyo minne, ina jumla ya pikipiki 33,234 na bajaji 9,584 ambapo jumla ni 42,818.

Alieleza kuwa, lengo la takwimu hizo ni kipimo cha kujipima utendaji kazi na kiwango cha udhibiti wa ajali, kupanga mipango, ya usajili na udhibiti wa vyombo hivyo katika kufanya tathimini.

Alisema visa vya ajali za barabarani zinapimwa kwa ukaguzi, wa endeshaji wengi wamesajiliwa huku wachache wakiwa hawajasajiliwa.

UCHUNGUZI 

Kwa mujibu wa uchunguzi mdogo uliofanywa na mwandishi wa makala hii, ulibaini baadhi ya ruti za magari, ambazo zinaidadi kubwa ya abiria wanaoingia katikati ya mji kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo kazi za kiofisi na biashara, ndizo zenye idadi kubwa ya watumiaji wa pikipiki na bajaji.

Baadhi ya ruti hizo zenye watu wengi ni Gongo la Mboto, Mbagala, Kibaha, Buza, Mbezi, Kimara, Kigamboni kuingia katikati ya mji.

Katika ruti hizo, kuna idadi kubwa ya wananchi ambao wanaingia katikati ya mji, hivyo kwa sababu ya changamoto ya usafiri wananchi wengi wanajikuta wakikosa usafiri, hivyo kulazimika kutumia usafiri wa bodaboda.

Mfano, katika maeneo mengi hayo yaliyoyatajwa, bodaboda zinapakia abiria wawili kuwafikisha katikati ya mji kwa sh. 2,000 kila mmoja.

Pia, bajaji zinapakia abiria kwa sh. 1000 kwa kila mmoja kuwafikisha katikati ya mji au kuwatoa mijini kuwarudisha katika makazi yao pembezoni.

Mfano kutoka Buza hadi Gerezani au Mnazi Mmoja ni sh. 2,000 kwa kila abiria, ambapo pikipiki hupakiza abiria wawili.

Kutoka Gongo la Mboto hadi Gerezani au Mnazi Mmoja, kuanzia Tabata, Segerea hadi Gerezani au Mnazi Mmoja ni sh. 1,000 kwa bajaji na 2,000 hadi 3,000 kwa kila mmoja.

Hali hiyo imesababisha ongezeko kubwa la pikipiki na bajaji katikati ya miji, hali ambayo inechochea kero kubwa kwa watembea kwa miguu, ambao hufika katika miji hiyo kununua bidhaa mbalimbali na kufanya shughuli zao za kiofisi.

Siyo kwa watembea kwa miguu tu, bali kwa wingi huo wa bajaji na pikipiki husababisha foleni kubwa katikati ya miji, na kuwa kero kubwa kwani waendeshaji wengi huwa hawafuati sheria za barabarani.

Wanaweza kusimama sehemu yoyote barabarani, bila kujalisha kuwepo kituo au hakuna kituo cha kushusha abiria, hali ambayo husababisha ajali au foleni kwa vyombo vingine vya usafiri.

MANUFAA KWA VIJANA

Mkazi wa Gongo la Mboto, Juliana Benson ambaye ni mtumiaji wa usafiri wa bodaboda alisema sababu ya yeye kupenda  kutumia usafiri huo mara kwa mara ni kuokoa muda kuwahi katika majukumu yake, kwani hauchelewi foleni.

Alisema changamoto ya usafiri huo ni kusababisha ajali kuliko mwingine, japokuwa anautumia anahofia suala hilo.

CHANGAMOTO YAKE

Licha ya wingi huo wa vyombo hivyo vya usafiri, kuchochea furaha kwa wananchi na kuongeza tija kwao, lakini unageuka kuwa karaha kwa wananchi katikati ya majiji, kwasababu ya idadi kubwa ya vyombo hivyo vya usafiri.

Kukiwa na foleni kidogo, ndani ya dakika tatu utashuhudia utitiri wa pikipiki zikisubiri kuvuka huku zikiziba njia hata ya watembea kwa miguu.

Kwa wingi huo, zimekuwa zikileta kero katika njia za watembea kwa miguu na magari, hali inayosababisha wakati mwingine kusababisha ajali kwa abiria na kwa vyombo vingine vya usafiri.

JITIHADA ZA LATRA

Akielezea usajili na usimamizi wa pikipiki na bajaji katikati ya miji, kwa  Kibaha Pwani, katika semina ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo, alisema wanaendelea kusimamia usajili wa leseni za pikipiki na bajaji.

Alisema lengo la kusimamia leseni hizo ni kutaka kuona vyombo vya usafiri ardhini, vinafuata sheria za barabarani za usajili na kufuata taratibu.

Mkurugenzi Suluo, alisema hakuna aliye juu ya sheria wamiliki wote wa vyombo vya usafiri ardhini wanatakiwa kuvimiliki kwa mujibu wa sheria.

Alisema wako baadhi ya waendesha pikipiki na bajaji, hawafuati sheria  hali inayosababisha ajali, ambao wengi ni wale wasiokuwa na leseni wala mafunzo ya kutumia vyombo hivyo vya usafiri.

“Sheria zipo, lazima zifuatwe hakutakuwa na huruma wala msamaha kwa yeyote anayevunja sheria, tutahakikisha tunatekeleza hilo kulinda usalama wa abiria,”alisema.

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Barabara wa LATRA,  Johansen Kahatano, alisema wingi wa pikipiki mijini na kutokufuata sheria, ikiwemo usajili wa leseni ni sababu ya ajali nyingi zinazotokea zikisababishwa na vyombo hivyo vya usafirishaji wa abiria.

Alisema LATRA inafanya jitihada kubwa za kuyafikia makundi ya bodaboda mikoani na mijini kuwapatia elimu kuhakikisha wanafuata sheria kuepusha ajali za mara kwa mara zinazojitokeza.

Alieleza kuwa, wanaendelea kufanya jitihada kubwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama barabarani, kuhakikisha wanatoa elimu ya utekelezaji wa shughuli zao za usafirishaj,  ikiwemo kusajili vyombo hivyo.

Usafiri huo umekuwa maarufu kwa Tanzania, hususan katika miji mikubwa inayokusanya idadi kubwa ya watu kama Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha na maeneo mengine, huwasaidia wananchi hao kuwahi katika majukumu yao.

Kwa umuhimu wa usafiri huo, pikipiki na bajaji zimekuwa zikiongezeka kila kukicha kwa sababu watu wengi wanautumia,  kuwahi kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Vyombo hivyo vya usafiri vimekuwa gumzo kubwa katikati ya majiji yakiwemo Dar es Salaam, Dodoma na Arusha, kwani wengi hupenda kuutumia na kusababisha ongezeko lake kuwa kubwa.

0000 

“Boda boda kwangu ni zaidi ya kazi, kwani inanipa uhakika wa kipato kwa siku na kuweka akiba yangu ya maendeleo, imekuwa mkombozi mkubwa wa kiuchumi,” Nasri Kassim,Mwendesha pikipiki wa Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Previous Post

SIMAMIENI HAKI

Next Post

MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

Next Post
MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAASKOFU WABEBA AJENDA YA UMOJA

MAASKOFU WABEBA AJENDA YA UMOJA

1 month ago
SHILOLE AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA

SHILOLE AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA

2 weeks ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?