• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MAKOCHA YANGA, SIMBA WAZITAMBIA  AL AHLY, ESPERANCE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 22, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
MAKOCHA YANGA, SIMBA WAZITAMBIA  AL AHLY, ESPERANCE
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

MAKOCHA Pedro Goncalves wa Yanga na Steve Barker wa Simba wametamba kuwa watashinda katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly na Esperance De Tunis.

Yanga itashuka nchini Misri kesho kupambana na timu ya Al Ahly katika Uwanja wa Al Salam jijini Cairo kuanzia saa 1:00 usiku.

Kikosi cha Simba  kitashuka keshokutwa katika Uwanja wa Stade Olympique Mammadi nchini Tunisia kupambana na Esperance De Tunis ya Tunisia kuanzia saa 1: 00 usiku.

KOCHA WA YANGA

Akizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam, jana, muda mfupi kabla ya kuondoka nchini, kocha wa Yanga, Pedro Goncalves alisema uzoefu wa wachezaji wa timu yake, unampa matumaini ya kushinda mchezo huo wa ugenini.

Alisema kuwa kwa sasa timu yake imepata muunganiko mzuri kitu ambacho kitasaidia kuwa bora zaidi na matokeo mazuri.

“Tunakwenda kusaka pointi tatu, natumaini tutazipata, wachezaji wetu hawana presha kwa sababu wamecheza mechi nyingi kubwa. Al Ahly ni timu nzuri na hatari.

“Lakini tumefanya kazi ya kuiangalia na kufahamu jinsi gani tutakwenda kucheza nao katika mechi hii,” alisema.

Pedro alisema kwamba kesho wataingia dimbani katika mchezo huo kwa kuwaheshimu wapinzani wao na kucheza kwa nidhamu kubwa ili kupata matokeo.

KOCHA WA SIMBA

Kocha wa Simba, Steve Barker alisema wanaenda kucheza mchezo ambapo wameweka mkakati’ kushinda dhidi ya wenyeji Esperance De Tunis.

Barker alifafanua kuwa wanakwenda kucheza mechi hiyo kwa uangalifu mkubwa kwa sababu wanahitaji kumaliza dakika 90 kwa kupata pointi tatu ambazo ni muhimu.

“Itakuwa ni mechi ngumu na ya tofauti sana, tunakwenda kucheza na timu ambayo ni nzuri sana ikiwa nyumbani kwao, tutapambana mwanzo mwisho kuhakikisha tunapata matokeo  mazuri na kutinga robo fainali,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema wachezaji wake wanatakiwa kuwa makini, hasa wakiwa na mpira na kipindi ambacho hawana mpira.

MSIMAMO

Katika msimamo wa michuano hiyo, timu ya Yanga  ipo nafasi ya pili katika kundi B ikiwa na pointi nne sawa na Al Ahly inayoongoza kundi zikicheza mechi mbili.

Kwa upande wa Simba ikiburuza mkia katika kundi D, haijashinda mchezo wowote huku  Esperance ikiwa na pointi mbili ikipata sare katika mechi mbili za awali na kushika nafasi ya tatu.

Previous Post

FIFA YADHAMIRIA KUWEKA NGUVU TANZANIA

Next Post

AHMED ALLY NA KAMWE WANENA

Next Post
AHMED ALLY NA KAMWE WANENA

AHMED ALLY NA KAMWE WANENA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM YACHANJA MBUGA

CCM YACHANJA MBUGA

11 months ago
MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

1 month ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?