• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TCPM – TABORA SIO TISHIO KWA SEKTA BINAFSI – NDEJEMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TCPM – TABORA SIO TISHIO KWA SEKTA BINAFSI – NDEJEMBI
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM Tabora kinachomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO kupitia kampuni tanzu ya TCPM haukusudii kuathiri wala kudhoofisha uwekezaji wa sekta binafsi bali unaongeza uzalishaji wa nguzo za zege ili kukidhi mahitaji yaliyopo ambayo bado hayajatosheleza uhitaji wa nguzo hizo nchini.

Ameeleza hayo Februari 15, 2026 wakati akikagua mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM Tabora, ambao umefikia asilimia 95 ya utekelezaji. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha wastani wa nguzo za zege 120 kwa siku.

“Kiwanda hiki si tishio kwa sekta binafsi; kinakuja kuongeza nguvu katika kazi ambazo tayari zilikuwa zinafanywa na sekta binafsi ya kuzalisha nguzo za zege,” amesema Ndejembi.

Ndejembi amefafanua kuwa TANESCO kwa mwaka 2025 ilikuwa na uhitaji wa nguzo za zege 80,000, lakini zilizopatikana kupitia sekta binafsi ni nguzo 40,000 jambo lililosababisha kutokufikiwa kwa malengo ya mahitaji hayo.

Ameeleza kuwa pamoja na Serikali kujenga kiwanda hicho, bado kuna fursa kwa sekta binafsi kuwekeza katika viwanda vya nguzo za umeme kutokana na mpango wa TANESCO wa kuendelea kufanya maboresho kwa kuondoa nguzo za miti na kutumia nguzo za zege katika usambazaji wa umeme nchini.

Aidha, Ndejembi ameitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kusimamia kikamilifu ukamilishaji wa kiwanda hicho ili mitambo itakapowashwa iweze kufanya kazi kwa ufanisi na ubora kulingana na mpango na malengo ya Kiwanda hicho.

Kadhalika, amewataka wafanyakazi waliopata ajira na watakaoajiriwa kutunza miundombinu na mitambo ya kiwanda hicho pamoja na kuweka mpango madhubuti na endelevu wa uendeshaji ili kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange amesema utekelezaji wa mradi wa kiwanda hicho cha nguzo za zege, kinachomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, hadi kukamilika kwake utagharimu Shilingi bilioni 7.9.

Twange ameeleza kuwa ujenzi wa kiwanda hicho upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji, ambapo kufikia tarehe 20 Februari 2026 mkandarasi atakuwa amekamilisha kazi zote, tayari kwa kuanza uzalishaji.

Previous Post

TRA IMEANZA KUTEKELEZA  MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KARATU

Next Post

YANGA YAANZA KUCHONGA

Next Post
YANGA YAANZA KUCHONGA

YANGA YAANZA KUCHONGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

2 months ago
SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

7 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?