• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YAANZA KUCHONGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 16, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA YAANZA KUCHONGA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetamba kuwa unakwenda kujenga uwanja wenye hadhi ya kimataifa ambao utatumika katika michuano mbalimbali na shughuli za kijamii.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa klabu hiyo, Hersi Said kupitia mtandao wa klabu hiyo kuwa wanakwenda kuweka historia kwa kujenga uwanja ambao utatumika katika majukumu mbalimbali ambayo yatasaidia jamii.

“Uwanja ambao tunakwenda kujenga utakuwa wenye hadhi ya kimataifa ndiyo maana tumefuata kanuni na sheria za CAF zinavyosema kipindi unataji uwanja uwe, pia tunakwenda  kujenga uwanja ambao sio tu unahudumu mpira wa miguu pekee bali ni mradi ambao utakwenda kubeba majukumu mengine ya kijamii.

“Utakuwa na uwezo wa kutumika kwa lengo la hafla na shughuli mbalimbali,tunakwenda kujenga uwanja ambao unaakisi mandhari ya ubunifu utakaomudu mahitaji mbalimbali ya kijamii, sanaa, burudani na michezo,” alisema.

Rais huyo alisema mradi huo ni wa Yanga na GSM sio mali ya mtu bali ni mali ya taasisi hizo mbili.

“Mradi huu sio mali ya mtu bali ni mali ya taasisi hizi mbili Yanga na GSM, pia mradi utaendelea kujengwa iwe mimi ni Rais wa Yanga ama vinginevyo, GSM na Yanga wanao wajibu wa kuhakikisha kuwa mradi huu unakamilika chini ya kiongozi yoyote ambaye atakuwa Rais wa Yanga.

“Nimejenga msingi bora na imara ambao utafanikisha jambo hili bila kumtegemea mtu,  ikitokea mimi sio Rais wa Yanga, atakayechukua wadhifa huu anapaswa kujua analo jukumu la kuhakikisha ndoto ya ‘wananchi’ inatimia,” alisema.

Aidha, Hersi alisema wanatambua  kiu ya mashabiki wao wanatamani kuona klabu yao  ikiwa na kiwanja chao.

Aliwahakikishia wanachama, wapenzi, wadau wa Yanga kuwa wanakwenda kujenga uwanja bora na wa kisasa ambao utaweka historia nchini na nje ya mipaka yetu.

” Tunahitaji wiki moja kukamilisha mahitaji na malengo ambayo tumeafikiana leo,  baada ya kikao cha pili kikao cha tatu tunakwenda kuweka historia GSM amesema siku anayosaini mkataba atahakikisha kazi inaanza mara moja,  yupo tayari na anayo hamu kubwa ya kuanza na kukamilisha historia hii kubwa kwa klabu yetu,” alisema.

Rais huyo aliongeza kuwa wamejadili na kupitisha mchoro ambao wanahitaji kujengwa uwanja huo.

Pia,alisema wameridhia kwa pamoja kuwa mchoro huo umekidhi mahitaji yao na matakwa ya CAF.

“Tukishapata gharama zote za ujenzi wa kiwanja na tukaridhia, hatua ni ya mgawanyo wa majukumu na manufaa ya mradi huu kwa pande zote, kisha tunakwenda kusaini mkataba na mbia wetu GSM,” alisema.

Previous Post

KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TCPM – TABORA SIO TISHIO KWA SEKTA BINAFSI – NDEJEMBI

Next Post

KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU

Next Post
KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU

KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

LUKUVI KUAGWA MIKOA MITATU

LUKUVI KUAGWA MIKOA MITATU

3 weeks ago
TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?