• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 16, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU
0
SHARES
14
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba,Steve Barker amekoleza moto wachezaji wake kwa kuwataka waweke akili yao katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Barker amesema hayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam,muda mfupi baada ya kumalizika mchezo kati ya Simba na Stade Malien.

Katika mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilishinda 1-0, tayari Wekundu wa Msimbazi wametolewa kwenye mashindano hayo.

“Nimefurahishwa na kiwango kizuri ambacho wachezaji wangu wamekionesha katika mechi hiyo.

“Pongezi kwa kucheza mchezo mzuri katika michuano hiyo ya kimataifa,hivi sasa michuano hii tumemaliza, tunarudi kupambana kusaka ubingwa wa ligi kuu,” alisema.

Barker alifafanua kuwa hivi sasa, wachezaji wake wanatakiwa kubadilisha mawazo yao na kuweka kichwani michezo ya ligi kuu na Kombe la FA.

“Tunapaswa kuwa imara na  kuweka nguvu mpya ya kupambana katika ligi, lengo kubwa ni kufanya vizuri na kutimiza malengo tuliojiwekea ya kutwaa ubingwa na michuano ya FA,” alisema.

Hata hivyo, kocha huyo alisema ana imani wachezaji wake watafanya vizuri zaidi kwa vile wameanza kuelewa mfumo anaotaka wacheze.

Kwa upande wa mwakilishi wa wachezaji, Shomari Kapombe aliwashukuru viongozi wa Simba kwa jitihada kubwa walizozifanya katika timu hadi kufika hapo walipo.

“Natanguliza shukrani zetu kwa niaba ya wachezaji wenzangu kwa viongozi,mashabiki wetu, wamefanya mambo mengi makubwa, haikuwa matarajio yetu kama wachezaji kufikia hatua hii, imetokea bahati mbaya, tunaweza kusema ni matokeo ya mpira ambayo yanaweza kutokea muda wowote.

“Hili tumechukua kama funzo kwetu, tunakwenda kujiweka sawa katika msimu huu wa ligi, kikubwa nawaomba viongozi waendelee kuwa pamoja na sisi,tunatarajia kufanya vizuri katika ligiili m simu ujao turudi tena Ligi ya Mabingwa Afrika, msimu ujao,” alisema.

Kapombe aliwaomba viongozi wa klabu hiyo, kuendelea kuongeza nguvu zaidi katika timu ili ifanye vizuri.

Previous Post

YANGA YAANZA KUCHONGA

Next Post

RONALDO  AWASHA MOTO

Next Post
RONALDO  AWASHA MOTO

RONALDO  AWASHA MOTO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAKONDA WEMBE ULE ULE AFCON

MAKONDA WEMBE ULE ULE AFCON

5 months ago
NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

1 month ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?