• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA ITAKAVYONUFAIKA KIUCHUMI, MKUTANO WA IPU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 18, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA ITAKAVYONUFAIKA KIUCHUMI, MKUTANO WA IPU
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA EMMANUEL MOHAMED

BUNGE la Dunia (IPU) ni taasisi ya kimataifa inayojumuisha mabunge ya nchi mbalimbali duniani kwa maneno mengine ni jukwaa maalumu kwa wabunge kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa.

IPU ilianzishwa mwaka 1889 ambapo makao makuu yake yapo mjini Geneva, nchini Uswisi inajumuisha mabunge ya nchi 179 na ina zaidi ya idadi ya wabunge 1,300.

Miongoni mwa malengo ya kuanzishwa kwa IPU ni kuchochea ushirikiano kati ya mabunge ya dunia kwa kubadilishana mawazo na uzoefu, kusaidia kutatua changamoto za kimataifa zikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, vita, umaskini na mizozo ya kijamii.

IPU hufanya mikutano yake ya kimataifa mara kwa mara ambapo wabunge kutoka nchi mbalimbali hukutana kujadili masuala ya kipaumbele ya kimataifa, mikutano hiyo inatoa fursa ya kubadilishana mawazo na kujifunza kutoka katika mifumo ya kisiasa ya nchi nyingine.

Kwa mara nyingine Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa 153 wa IPU ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 5 hadi Oktoba 9 mwaka huu jijini Arusha ambapo utakutanisha wageni zaidi 2,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Hivi karibuni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alithibitisha utayari wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa IPU, Martin Chungong Ikulu jijini Dar es Saalam ambapo alisema serikali imejipanga kikamilifu maandalizi kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na taasisi hiyo.

Kufanyika kwa mkutano huo utaleta faida nyingi katika sekta ya utalii, ambapo Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Epharim Mafuru anataja faida hizo ikiwemo fursa ya kipekee ya Tanzania kutangaza vivutio vya utalii kupitia viongozi wabunge hao wa IPU.

“Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania na kamati ya kitaifa iko kazini kuratibu maeneo ambayo yatakayopelekwa viongozi hao,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema lengo la kuwapeleka viongozi hao katika vivutio hivyo ni kuwaonyesha vivutio hivyo vya kipekee ili watakaporejea kwao wawe mabalozi wazuri kutangaza vivutio hivyo.

“Kwa ujumla, mkutano wa wabunge duniani unakuwa fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa, kuongeza watalii, kukuza uchumi wa utalii na kuimarisha nafasi ya nchi katika soko la utalii duniani,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema mara nyingi wageni wanaohudhuria mikutano ya aina hiyo hutumia fedha nyingi katika hoteli, malazi, usafiri na safari za kitalii, migahawa na chakula ununuzi wa bidhaa za utamaduni na kwamba biashara nyingi zinazohusiana na utalii hunufaika.

“Washiriki hawa wakifika katika vivutio vyetu watachangia kuongezeka kwa idadi ya wageni ambapo itamaanisha kuongezeka kwa mahitaji ya huduma mbalimbali hatua ambayo huongeza ajira kwa waongoza watalii, madereva wa watalii, wafanyakazi wa hoteli, wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali wa bidhaa za utamaduni,”alisema.

“Washiriki wa mikutano mikubwa ya aina hiyo mara nyingi huamua kuongeza siku za kukaa nchini kutembelea maeneo ya utalii, wengine hurudi tena baadaye kama watalii pamoja na familia au marafiki, hivyo mkutano huu utatufaidisha sekta ya utalii,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk. Mohammed Maguo, alisema kitendo cha Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni fursa muhimu ambayo itajitangaza vyema.

Pia, alisema mkutano huo utatoa tafsiri kubwa ya kuleta watalii na kutengeneza uhusiano mzuri wa kidiplomasia ambao utakuwa chachu ya Tanzania kutangazika.

“Tunaamini wananchi wa jiji la Arusha wataendelea kunufaika zaidi na ujio huo wa wageni kwa kuwa watahitaji huduma za hoteli, usafiri, chakula na burudani hivyo watatumia fursa hiyo kujikwamu kiuchumi,” alisema.  

Pia, alisema mbali na hilo wageni hao watahitaji kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Serengeti, Ngorongoro, mlima Kilimanjaro na Tarangire.

Naye Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi, Saidi Msonda, alisema mkutano huo utatoa msukumo mkubwa kwa sekta ya huduma, ikiwemo hoteli, usafiri na biashara ndogo ndogo.

“Ujio wa wageni kutoka mataifa mbalimbali unatarajiwa kuongeza mzunguko wa fedha, hasa katika jiji la Arusha na hata ambako baadhi ya wageni wanaweza kutembelea kwa shughuli za ziada na utalii,” alisema.

Alisema fursa hiyo inaweza kufungua milango ya uwekezaji mpya, baada ya wawekezaji kushuhudia mazingira ya kisiasa yaliyo tulivu na miundombinu inayokua kwa kasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti, Sera na Uchumi (REPOA), Dk. Donald Mmari, alisema Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo utaleta manufaa makubwa nchini yakiwemo, kuleta wageni ambao watatumia fedha zao za kigeni ambazo zitaleta chachu ya uchumi wa nchi kuzidi kukua.

Alisema mkutano huo utaleta tafsiri ya kuivutia nchi kuendelea kutangazika na kuwavutia wageni wengine kuzidi kuja nchini.

Previous Post

MANDONGA AJA KIVINGINE

Next Post

MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI

Next Post
MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI

MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NYOTA YANGA WAPEWA TANO

NYOTA YANGA WAPEWA TANO

6 days ago
SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

1 month ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?