• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 3, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA, Zanzibar

WAKATI Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves akiahidi kuboresha zaidi aina ya uchezaji ili kukaribia ubingwa, Kocha wa Simba, Steve Barker anaamini timu yake ina nafasi ya kuwapiku wapinzani wake katika mbio za taji hilo msimu huu.

Makocha hao walitoa kauli hizo juzi muda mchache baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja.

Baada ya matokeo hayo, sasa Yanga inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 29  baada ya kucheza mechi 11, JKT Tanzania  ipo nafasi ya pili kwa alama 28, imecheza mechi 17 huku Simba ikifuatua kwa alama 24 imeshuka dimbani mara 11.

Ili Simba kuipiku Yanga inapaswa kwanza kufuta utofauti wa alama tano dhidi yake katika mechi 19 zilizosalia.

Akizungumza juzi, Kocha wa Simba, Barker alisema ikiwa kikosi chake kitaendelea kuonyesha kiwango kama kilichoonyesha dhidi ya Yanga anaamini bado watakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa taji.

“Bado kuna mechi nyingi za kucheza, kweli wametuzidi alama tano lakini bado kuna mechi lakini pia  Yanga inaweza kufanya makosa.

Kama tutaendelea kucheza kama tulivyocheza leo(juzi) na kuepuka kufanya makosa basi bado tuna nafasi kubwa tukawa mabingwa,” alisema.

Pia, Barker aliongeza kuwatimu yake ilikuwa bora kiwanjani hasa  kipindi cha kwanza, kwa kutengeneza nyingi walikosa kufunga mabao.

Naye Kocha wa Yanga, Pedro alisema ataendelea kukiboresha kikosi chake kimbinu kuzikabili kila timu wanazokutana nazo.

“Tutazidi kujipanga kuhakikisha tunacheza vyema zaidi katika aina hii ya mechi. Lengo ni kuendelea kupata matokeo mazuri,” alisema.

Pia, Pedro alisema katika mchezo wa juzi, Simba ilianza vyema lakini baadaye kikosi chake kilirejea katika staili yake na kucheza soka safi.


Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo ikifanya hivyo kuanzia 2021/2022, 2022/2023, 2023/2024 na 2024/2025.

Mara ya mwisho Simba kubeba taji hilo ulikuwa msimu wa 2020/2021 na tangu hapo haijatwaa taji lolote kubwa.

Previous Post

DIARRA, LOEMBA, OURA WALIVYOTIKISA DABI YA K’KOO

Next Post

AHMED ALLY AJIVUNIA GUEYE

Next Post
AHMED ALLY AJIVUNIA GUEYE

AHMED ALLY AJIVUNIA GUEYE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AWAHAKIKISHIA WAKULIMA NCHINI KUIMARISHA MASOKO, KUTAFUTA BEI NZURI YA MAZAO

DK. SAMIA AWAHAKIKISHIA WAKULIMA NCHINI KUIMARISHA MASOKO, KUTAFUTA BEI NZURI YA MAZAO

7 months ago
FEI TOTO AAHIDI MAKUBWA CAFCC

FEI TOTO AAHIDI MAKUBWA CAFCC

5 months ago

Popular News

  • KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • LAZARUS CHAKWERA AMALIZA ZIARA YA SIKIU 9 NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?