• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

UKAME BASI MSIMBAZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 5, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
UKAME BASI MSIMBAZI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA, Pemba

BAADA ya kusubiri kwa miaka mitano sasa, Simba imetwaa taji lake kubwa la kwanza kufuatia kuifunga Azam FC bao 1-0 katika fainali ya Kombe la FA.

Simba ilivunja mwiko huo wa muda mrefu katika mtanange huo uliopigwa jana kuanzia saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Gombani, Pemba.

Bao la kujifunga la Yahya Zayd dakika ya 61 katika harakati za kuokoa faulo iliyopigwa na Neo Maema lilitosha kuipa ushindi Simba.

Dakika sita baadaye, kiungo nyota wa Azam FC, Feisal Salum maarufu Fei Toto, alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumshambulia kwa mikono Libasse Gueye wa Simba baada ya vuta nikuvute.

Baada ya kuonyeshwa kadi hiyo, Fei Toto na baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi la Azam FC walionyeshwa kutofurahishwa na uamuzi huo kabla ya mchezaji huyo kuondoka uwanjani.

Licha ya kupata kadi nyekundu, Azam FC iliendelea na aina yake ya soka huku ikitengeneza baadhi ya nafasi ambazo ilishindwa kuzitumia kwa umakini.

Kabla ya jana, Wekundu hao wa Msimbazi mara ya mwisho kubeba taji kubwa (Ligi Kuu Bara au Kombe la FA) ilikuwa miaka mitano iliyopita, ikitwaa FA mwaka 2021 kwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Simba ilikuwa ya kwanza kuingia uwanjani kupasha misuli joto ikifanya hivyo saa 10:16 jioni na kutoka saa 10:41 wakati Azam FC ikiingia saa 10:17 na kutoka saa 10:41.

KOCHA WA SIMBA

Akizungumza baada ya mchezo huo, Steve Barker alisema anashukuru kushinda taji hilo na anawashukuru viongozi, wanachama na wachezaji kujituma na kupata ushindi huo.

MAGORI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Crescentius Magori amesema mwaka huu walikutana na changamoto nyingi na wana imani mwanga wa mataji umeanza kurudi katika klabu yao.

AHMED ALLY

Ahmed Ally ambaye ni msemaji wa klabu ya SImba alisema ana furaha baada ya kukosa vikombe katika kipindi cha miaka minne mfululizo.

“Tumesubiri kwa muda mrefu, kama tungekosa hili kombe ingekuwa miaka mitano, tumejipata msimu huu tumechukua kombe hili, tunamshukuru Mungu,”alisema  

Pia, alitangaza leo kuwepo paredi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na watapita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo mitaa ya Twiga na Jangwani  ambapo alisema watakuwa na jambo lao nusu saa na kisha kufika fukwe za Coco Beach.

CLATOUS CHAMA

Clatous Chama alisema mchezo ulikuwa wa ushindani sana na iliwachukua muda kutwaa taji hilo.

“Mchezo ulikuwa mgumu, ukweli Azam ni timu nzuri na tumeshindana nao, tumeshinda tunashukuru Mungu,” alisema Chama.

KIBA DAKIKA NNE TU

Msanii nyota wa bongo fleva, Ali Kiba ametumia dakika nne kufanya onyesho la muziki kabla ya mchezo wa fainali ya Kombe la FA kati ya Simba na Azam FC.

Katika mtanange huo uliopigwa Uwanja wa Gombani, Pemba, Kiba ametumia dakika hizo kuimba nyimbo mbili pekee ambazo ni Utu na Finale.

Simba: Mamadou Kassali, David Duchu, Nickson Kibabage, Ismail Toure, Rushine De Reuck, Yusuph Kagoma, Libasse Gueye, Neo Maema, Elie Mpanzu, Clatous Chama na Anicet Oura.

Azam FC: Aishi Manula, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Lameck Lawi, Fuentes Mendoza, Himid Mao, Abdul Sopu, Yahya Zayd, Jephte Kitambala, Feisal Salum na Idd Selemani.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA, CHAPO WAANIKA FURSA UCHUMI

Next Post

DK. NCHIMBI : DITF 2050 IWE KITOVU CHA UBUNIFU NA BIASHARA ZA KIMATAIFA

Next Post

DK. NCHIMBI : DITF 2050 IWE KITOVU CHA UBUNIFU NA BIASHARA ZA KIMATAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TAASISI ZINAZOFANYA VIBAYA KUANIKWA

TAASISI ZINAZOFANYA VIBAYA KUANIKWA

4 months ago
DK. SAMIA AAHIDI WAKULIMA DAWA YA KUPULIZIA MIKOROSHO BILA MALIPO

DK. SAMIA AAHIDI WAKULIMA DAWA YA KUPULIZIA MIKOROSHO BILA MALIPO

10 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?