• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA, CHAPO WAANIKA FURSA UCHUMI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 3, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA, CHAPO WAANIKA FURSA UCHUMI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo, wamesisitiza kutumika vyema kwa fursa  zinazotokana na rasilimali zilizopo katika mataifa hayo, kuinua na kuimarisha uchumi wa nchi hizo na Afrika kwa ujumla.

Pia, wamesema Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba); ni kielelezo cha kuendelea kuaminika na kukubalika kwa Tanzania kama lango na kiungo cha uchumi wa Afrika Mashariki na Afrika.

Waliyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa ufunguzi wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), uliohudhuriwa na viongozi na waoneshaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

RAIS CHAPO

Rais Chapo alisema nchi za Afrika zinatakiwa kuharakisha mageuzi ya kiuchumi kwa kuwekeza katika viwanda, kuongeza thamani ya rasilimali zake na kuimarisha biashara ya ndani badala ya kuendelea kutegemea usafirishaji wa malighafi.

Alisema Afrika ina kila sababu ya kujenga uchumi unaotegemea viwanda, ubunifu, teknolojia, uchumi wa kidijitali na akili bandia kuongeza ushindani katika soko la dunia.

Rais Chapo alisema Bara la Afrika haliwezi kuendelea kusafirisha malighafi na baadaye kuagiza bidhaa zilizotengenezwa kutokana na malighafi hizo, akisisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya rasilimali ndani ya nchi za Afrika.

Pia, alisema Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) linatoa fursa ya kuunganisha masoko ya bara hilo, ingawa mafanikio yake yatategemea uwekezaji katika miundombinu ya barabara, reli, bandari, nishati na mifumo ya kidijitali kurahisisha biashara na usafirishaji.

Rais Chapo, alisema Tanzania na Msumbiji zina nafasi ya kipekee kutokana na ukaribu wake wa kijiografia, rasilimali nyingi na miundombinu ya usafirishaji inayoweza kuimarisha biashara kati ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alitaja maeneo yenye fursa kubwa za ushirikiano kuwa ni nishati, kilimo cha biashara, maendeleo ya Bonde la Ruvuma, viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, madini, utalii, uchumi wa buluu na miundombinu.

 Chapo aliwahimiza wafanyabiashara wa Tanzania, Afrika na duniani kuitazama Msumbiji kama mshirika wa kuaminika kwa uwekezaji, huku akitoa mwaliko wa kushiriki Maonesho hayo ya Sabasaba, kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Alisisitiza kuwa, mipaka ya Afrika inatakiwa kuwa njia za kukuza biashara na ustawi badala ya kuwa vizuizi, akieleza kuwa mataifa ya Afrika kujenga uchumi uliounganishwa kwa manufaa ya wananchi wake.

Akizungumzia uhusiano wa Tanzania na Msumbiji, alisema nchi hizo zimejenga urafiki wa kihistoria, ulioanza katika harakati za ukombozi na sasa zinatakiwa kuutumia msingi huo kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Pia, alisema maono ya waasisi wa mataifa hayo, yalilenga uhuru wa kisiasa, huku kizazi cha sasa kikibeba jukumu la kuhakikisha Afrika inafikia uhuru wa kiuchumi kupitia uwekezaji, viwanda na biashara.

Aidha, aliipongeza Tanzania kwa Kuadhimisha Miaka 50 ya Maonesho ya Sabasaba na kuwa, yameendelea kuwa jukwaa muhimu la biashara, ubunifu, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi barani Afrika.

 Chapo alisisitiza kuwa, dhamira ya Msumbiji ni kuendelea kushirikiana na Tanzania kujenga uchumi imara na Afrika yenye ushindani zaidi.

Alisema nchi hizo zitaendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kujenga uchumi wenye ushindani, ustahimilivu na unaowanufaisha wananchi wa mataifa hayo mawili.

Alieleza kuwa, Tanzania imepiga hatua kubwa katika mabadiliko ya kiuchumi na sasa imekuwa moja ya majukwaa muhimu barani Afrika ya kukuza biashara, ubunifu na uwekezaji. 

“Tanzania na Msumbiji zimekuwa washirika tangu enzi za mapambano ya ukombozi wa Afrika na urafiki wetu ulijengwa katika mshikamano na mapambano ya pamoja, si kwa maslahi ya biashara pekee, hivyo kizazi cha sasa kina wajibu wa kutimiza ndoto za waasisi wa mataifa hayo kuhakikisha kinapata uhuru wa kiuchumi, kama walivyopata uhuru wa kisiasa,” alisema Chapo. 

Alieleza kuwa, uchumi wa nchi hizo, unakamilishana badala ya kushindana, jambo linalotoa nafasi kubwa ya kuvutia uwekezaji na kuongeza biashara kati ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

 Rais Chapo alisema Afrika inatakiwa kuacha kuuza malighafi na badala yake kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani ya rasilimali zake na kuimarisha matumizi ya sayansi, teknolojia, uchumi wa kidijitali na akili unde.

Pia, alisema Bandari za Dar es Salaam na Pemba zinatakiwa kushirikiana kama mtandao wa pamoja wa usafirishaji; badala ya kushindana kupunguza gharama za biashara na kuongeza ushindani wa ukanda huo katika soko la kimataifa.

Hivyo, aliwahimiza wafanyabiashara wa Tanzania, Afrika na duniani kuwekeza Msumbiji, akieleza kuwa, nchi hiyo ina fursa nyingi katika sekta za nishati, kilimo, madini, utalii, viwanda, uchumi wa kidijitali, uchumi wa buluu na miundombinu.

RAIS DK. SAMIA

Awali, akimkaribisha Rais Chapo, Rais Dk. Samia, alisema Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), yameendelea kuwa nguzo muhimu ya kukuza biashara, uwekezaji na viwanda nchini, huku akiitaja Tanzania kuwa, kitovu cha biashara na lango la masoko ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Bara la Afrika na dunia.

Alimshukuru Rais Chapo, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, kwani ushiriki wake unaonesha kuendelea kuimarika kwa uhusiano wa kindugu, ujirani mwema na ushirikiano wa kweli kati ya nchi hizo.

Rais Dk. Samia alisema Rais Chapo si mgeni nchini Tanzania, kwani amewahi kutembelea Tanzania mara kadhaa, ikiwemo kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Msumbiji na baada ya kuingia madarakani kwa ziara rasmi ya kiserikali. 

Alisema uwepo wake katika Jubilei ya Dhahabu ya Sabasaba, unaongeza ukurasa mwingine wa historia ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Samia alieleza kuwa, mara ya kwanza kwa Rais wa Msumbiji kuwa mgeni rasmi wa Sabasaba, ilikuwa mwaka 1999 ambayo yalifunguliwa na aliyekuwa Rais wa Msumbiji, Joaquim Chissano na mwaka 2024 yakafunguliwa na Rais Filipe Nyusi, jambo linaloonesha umuhimu wa uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili. 

Pia, alisema uhusiano wa Tanzania na Msumbiji umejengwa katika misingi ya harakati za ukombozi zilizoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na waasisi wa Msumbiji akiwemo Hayati Eduardo Mondlane, Hayati Samora Machel na kwamba, jukumu la viongozi wa sasa ni kuhakikisha historia hiyo inatafsiriwa katika maendeleo ya kiuchumi.

“Sisi tuliopo leo wajibu wetu ni kuidumisha historia hiyo na kuhakikisha haiishi katika kumbukumbu pekee, bali inatafsiriwa kukuza uzalishaji, biashara, uwekezaji, viwanda, ajira, usafirishaji na kuimarisha ustawi wa watu wetu,” alisema. 

Alisema kwa kipindi cha miaka 50, Sabasaba imekuwa daraja muhimu la kuwaunganisha wazalishaji, wanunuzi, wafanyabiashara, wawekezaji na masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Rais Samia aliongeza kuwa, maonesho hayo yamekuwa sehemu ya maisha ya Watanzania wengi na kuwa, baadhi ya wafanyabiashara walianzia biashara ndogo kupitia Sabasaba na baadaye kukua na kuwa wakubwa.

Rais Dk. Samia alisema ongezeko la ushiriki wa kampuni na mataifa mbalimbali katika maonesho hayo linaonesha kuwa, Tanzania inaendelea kuaminika kama kituo kikuu cha biashara na uwekezaji, huku akiwapongeza waandaaji kwa uboreshaji wa miundombinu, matumizi ya teknolojia na uendeshaji wa maonesho hayo.

Aliwataka waandaaji kuendelea kuwa, wabunifu kuyafanya maonesho hayo yaendelee kukua na kufikia viwango vikubwa zaidi vya kimataifa.

 “Nitoe rai kwenu kuwa wabunifu zaidi tuyakuze maonesho haya katika viwango na hatua kubwa zaidi za kimataifa,” alisema.

KAPINGA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, alisema Sabasaba, imeendelea kuwa kioo kinachoonyesha safari ya uchumi wa Tanzania kwa kuonesha ilikotoka, iliko na mwelekeo wake wa baadaye.

Alisema maonyesho hayo yanaonyesha kuwa, uchumi wa Tanzania unajengwa katika uwezo wa kuzalisha, kushindana na kuuza bidhaa na huduma katika masoko ya dunia. 

Kapinga alisema maonyesho ya mwaka huu yanafanyika katika Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, yakiongozwa na kaulimbiu ya kuanza na soko kabla ya uzalishaji wa bidhaa.

Alieleza kuwa, dunia ya sasa inahitaji kuzalisha bidhaa zinazohitajika na soko na kwamba, Tanzania imejipanga kutumia maonyesho hayo kama jukwaa la kuongeza ushindani wa viwanda, kupanua mauzo ya nje na kuunganisha sekta binafsi na minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa.

Waziri Kapinga alisema kupitia diplomasia ya uchumi iliyopewa msukumo na Rais Dk. Samia, Tanzania imefungua masoko mapya, kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuongeza imani ya wawekezaji.

Pia, alisema katika mwaka uliopita mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi yalifikia takribani dola za Marekani bilioni 17, huku mauzo ya bidhaa pekee yakivuka dola bilioni 10, sekta ya madini ikiongozwa na ongezeko la mauzo ya dhahabu na mazao ya biashara na nafaka yakiongeza mchango wake kutokana na uzalishaji na upatikanaji wa masoko.

Judith alisema wizara itahakikisha maonyesho hayo yanakuwa jukwaa la kudumu la maendeleo ya biashara kwa kuwaunganisha wazalishaji na wanunuzi wa kimataifa, kutoa taarifa za masoko kwa wakati, kuvutia uwekezaji wenye tija na kuongeza mauzo ya bidhaa zenye thamani kubwa zinazobeba chapa ya “Made in Tanzania.”  

Alisisitiza kuwa, ushindani wa dunia ya sasa unategemea maarifa, ubunifu na tija.

 ZANZIBAR

Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff wa SMZ, aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Viwanda na Biashara na TanTrade, kwa kufanikisha Maonesho ya 50 ya Sabasaba, akisema yamekuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, uwekezaji, teknolojia na ushirikiano wa kiuchumi ndani na nje ya Tanzania.  

Alisema kupitia maonesho hayo, Zanzibar imeendelea kupata fursa ya kutangaza vivutio vya uwekezaji, bidhaa zinazozalishwa nchini na kuimarisha uhusiano wa kibiashara na washirika mbalimbali wa maendeleo.

TAN TRADE

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Dk. Latifa Hamis, alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 26,000 na kuingiza zaidi ya sh. bilioni 17, kupitia mauzo na mikataba ya papo kwa hapo hatua inayolenga kuchochea ukuaji uchumi wa Tanzania.

Alisema zaidi ya waoneshaji 4800, wanashiriki maonesho hayo huku biashara 3752, zikitangazwa na idadi ya watembeleaji ikitarajiwa kufikia 624,380.

Previous Post

TUTUMIE AFCON KAMA FURSA YA KUJITANGAZA KIMATAIFA – DK. YONAZI

Next Post

UKAME BASI MSIMBAZI

Next Post
UKAME BASI MSIMBAZI

UKAME BASI MSIMBAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

8 months ago
MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA HELKOPTA YATAMBULIWA

MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA HELKOPTA YATAMBULIWA

7 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?