• ePaper
Wednesday, September 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAKATIBU WAKUU VYAMA VYA UKOMBOZI WAJADILI HALI YA KISIASA KUSINI MWA AFRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 5, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
MAKATIBU WAKUU VYAMA VYA UKOMBOZI WAJADILI HALI YA KISIASA KUSINI MWA AFRIKA
0
SHARES
16
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza Kikao cha 12 cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambapo, pamoja na mambo mengine, vimejadili hali ya siasa, ukombozi wa kiuchumi na kuboresha hali za wananchi katika nchi zao.

Kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 5 Machi 2026, Kibaha, mkoani Pwani, kilihusisha Makatibu Wakuu wa Vyama 6 vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambavyo ni ANC (Afrika Kusini), CCM (Tanzania), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe) na MPLA (Angola).

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Asha-Rose Migiro, amesema kuwa katika kikao hicho wamepitia maazimio ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Vyama hivyo uliofanyika mwaka jana, nchini Afrika ya Kusini.

Alisema mijadala ilijikita kuangalia hali ya kisiasa katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, hususan kulinda uhuru wa kisiasa na kiuchumi, kutathmini malengo ya harakati za ukombozi pamoja na kuendelea kulinda na kuimarisha uhuru uliopatikana.

Dkt. Migiro amesema jukumu kubwa la vyama hivyo ni kuimarisha mshikamano na umoja wao pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili kanda hiyo ikiwemo mabadiliko ya tabianchi. Aidha, walijadili namna ya kutatua migogoro katika nchi wanachama na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Katika kikao hicho pia walifanya mapitio ya maendeleo yaliyopatikana katika nchi zao, ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za jamii, kuboresha miundombinu pamoja na kuweka mikakati ya kujenga uchumi stahimilivu na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na umuhimu wa kuongeza ajira kwa vijana, kuwawezesha wanawake pamoja na kujenga uchumi jumuishi na stahimilivu kwa maendeleo ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Previous Post

SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

Next Post

ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

Next Post
ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

10 months ago
MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

10 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?