• ePaper
Saturday, May 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 12, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

KOCHA Mkuu wa Young Africans, Pedro Goncalves, ametamba kuwa wamelenga kupata ushindi dhidi ya Prisons licha ya kukabiliwa na majeruhi kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Clement Mzize.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Pedro alisema kikosi chake kimejiandaa vizuri huku akili zao zikilenga kufanya vizuri na kufikia malengo ya klabu.

“Tutakuwa na mazoezi ya mwisho kujiandaa na mechi dhidi ya Tanzania Prisons. Tunajua tunakwenda kucheza na timu ngumu ambayo imetoka kupoteza  mechi dhidi ya Simba na baadaye kupata sare na Azam FC.

“ Tuna uhakika mchezo utakuwa mgumu, lakini tupo hapa kwa ajili ya alama tatu na tunaamini tutazipata,” alitamba kocha huyo.

Kipa wa Yanga, Hussein Masalanga alisema wachezaji wote wamejiandaa vizuri na wanafahamu umuhimu wa kushinda mchezo huo.

“Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri na tunajua umuhimu wa mchezo huu. Tunajua tunakwenda kucheza na timu ngumu yenye wachezaji wazuri, lakini tutawaheshimu na kupambana kwa sababu lengo letu ni pointi tatu,” alisema Masalanga.

Juzi, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Ajabu Kifukwe, alisema kuwa kikosi chao  chote kipo fiti kuivaa Yanga.

Aliongeza kuwa maandalizi ya timu yamekamilika na wachezaji wako katika hali nzuri ya kiufundi kuelekea mchezo huo muhimu.

Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa na poin ti 32 baada ya kushuka dimbani mara 12 katika ligi hiyo huku Prisons ikiwa na alama 13 baada ya kucheza mechi 15 za ligi hiyo.

Lakini kauli ya kocha wa Yanga, Pedro Goncalves  imekuja baada ya hivi karibuni, Clement Mzize kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini ambapo atakuwa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu.

Mzize anatarajiwa kurudi dimbani msimu ujao wa 2026/2027.

Wakati huo huo, beki wa Yanga, Dickson Job amefanyiwa upasuaji wa goti, jana, baada ya kuumia katika mchezo wa ‘dabi’ dhidi ya  Simba.

Job alipata majeraha hayo kipindi cha kwanza katika mechi ya ‘Kariakoo Dabi’ dhidi ya Simba iliyochezwa Machi Mosi, mwaka huu viwani Zanzibar.

Katika mchezo huo, Job alipata majeraha hayo baada ya kugongwa na kiungo wa Simba, Inno Loemba wakati wakiwania mpira na kushindwa kuendelea kucheza mechi hiyo iliyomalizika kwa matokeo ya  suluhu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa nahodha huyo msaidizi amefanyiwa operesheni asubuhi ya leo(kesho) kwa mujibu wa madaktari hali yake inaendelea vizuri.

 “Nahodha wetu Dickson Job amefanyiwa operesheni asubuhi ya leo(jana) nchini Afrika Kusini na ‘Alhamdulillah’ jambo limekwenda vizuri kabisa,”  alisema.

Kamwe alisema taarifa ya awali kutoka Afrika Kusini, imeeleza kuwa beki huyo atakaa  nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitatu akiuguza jeraha hilo.

Ofisa habari huyo aliwaomba mashabiki na wapenzi wa soka nchini kumuombea mchezaji huyo ili apone kwa haraka.

Hayo ni majeraha ya kwanza makubwa kwa Job, tangu asajiliwe na timu hiyo aliyojiunga nayo Januari 11, mwaka  2021 akitokea timu ya Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro.

Previous Post

DK. MIGIRO: NCHI YETU IMEDHAMIRIA KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA

Next Post

TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

Next Post
TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI

WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI

1 month ago
WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?