• ePaper
Saturday, May 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI imeihakikishia jumuiya ya kimataifa kuwa, matokeo ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, mwaka jana, yataongeza uwajibikaji, umoja na maridhiano nchini Tanzania.

Pia, serikali imesisitiza Tume hiyo chini ya Jaji Mohamed Chande, iko huru katika kazi zake hatua ambayo italeta matokeo makubwa na chanya.

Akiwasilisha mada katika Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), mjini Geneva, Uswisi, juzi, Mkurugenzi Msaidizi wa Taarifa za Haki za Binadamu kutoka.

Wizara ya Katiba na Sheria, Beatrice Mpembo, alisema uamuzi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume hiyo umelenga kuweka uwazi, imani ya wananchi na uwajibikaji kwa kuangalia matukio yote ya Oktoba 29, mwaka jana, baada ya Uchaguzi Mkuu.

Beatrice alifafanua, Novemba 18,  mwaka jana, Rais Samia aliunda Tume hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, kwa lengo la kupata undani wa matukio ya Oktoba 29, chanzo na kilichoendelea baada ya kuibuka vurugu.

“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliunda Tume kama chombo huru, maalumu cha uchunguzi na usimamizi kwa lengo la kuishauri serikali hatua zinazopaswa kuchukuliwa,” alifafanua Beatrice.

Aliongeza, Tume hiyo inachunguza visababishi, madai ya vijana, vitendo vya upinzani, kuona kama kulikuwa na ufadhili wa vurugu kutoka nje  na kuthamini kazi ya vyombo vya usalama katika kuleta utulivu wakati wa vurugu hizo.

MATARAJIO

Alifafanua, matokeo ya Tume yataimarisha amani, utulivu, kuponya mpasuko wa kijamii, kuleta majadiliano ya kitaifa, kushughulikia malalamiko ya kihistoria, kuzuia migogoro, kuimarisha utawala wa kidemokrasia na umoja wa kitaifa.

Tayari serikali imekwisha chukua hatua madhubuti ikiwemo  msamaha kwa vijana 1,787 waliohusika katika matukio ya Oktoba 29, kwa kushawishiwa na kuunda Wizara maalumu ya Vijana.

Tume ya Jaji Chande inaheshimika kimataifa kutokana na rekodi ya Mwenyekiti huyo katika anga za haki za binadamu na sheria za kimataifa, ilipewa kazi kwa siku 90 baadaye ikaongezewa siku 42 hadi mwezi ujao.

Previous Post

YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO

Next Post

WAZIRI KAIRUKI ASISITIZA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MAWASILIANO

Next Post
WAZIRI KAIRUKI ASISITIZA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MAWASILIANO

WAZIRI KAIRUKI ASISITIZA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MAWASILIANO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MATOKEO YAMSIKITISHA KOCHA YANGA

MATOKEO YAMSIKITISHA KOCHA YANGA

2 months ago
TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

2 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?