• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MBARAWA AIPONGEZA TASAC KUSIMAMIA NA KUDHIBITI USAFIRI MAJINI KWA UFANISI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MBARAWA AIPONGEZA TASAC KUSIMAMIA NA KUDHIBITI USAFIRI MAJINI KWA UFANISI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema serikali kupitia taasisi zake inaendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu ya usafiri na huduma za uokoaji majini ili kulinda usalama wa wananchi na mali zao na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Waziri Mbarawa, ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam aliposhiriki futari iliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania-TASAC, iliyowakutanisha wadau wa sekta ya usafiri majini kwa ili kuimarisha ushirikiano na kujadili mustakabali wa sekta hiyo.

Amewahimiza wadau wa sekta ya usafiri majini kushirikiana na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa salama, yenye ufanisi na inayotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

Aidha, Waziri Mbarawa, ameipongeza TASAC kwa kuendelea kusimamia na kudhibiti shughuli za usafiri majini nchini kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama wa vyombo vya majini, kulinda mazingira ya bahari na maziwa, pamoja na kusimamia utekelezaji wa sheria na mikataba ya kimataifa inayohusu usafiri majini.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ya uchukuzi pamoja na usimamizi wa sekta mbalimbali ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Salum, amesema hafla hiyo ya futari imelenga kuimarisha mshikamano, kujenga mahusiano imara na kuthamini ushirikiano uliopo kati ya TASAC na wadau wa sekta ya usafiri majini.

Kupitia ushirikiano huo, amesema wadau wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha sekta ya usafiri majini inakuwa salama, yenye tija na inachangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Mussa Mandia, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi zake na wadau wa sekta binafsi katika kuendeleza sekta ya usafiri majini na kuhakikisha inakuwa salama, yenye ufanisi na yenye mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.

Previous Post

UWEKEZAJI WA SHILINGI BILIONI 50 KITUO CHA MPOMVU WAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME KANDA YA ZIWA

Next Post

MAFWELE NA WENZAKE 42 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUGHUSHIVIBALI VYA KUMILIKI SILAHA

Next Post
MAFWELE NA WENZAKE 42 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUGHUSHIVIBALI VYA KUMILIKI SILAHA

MAFWELE NA WENZAKE 42 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUGHUSHIVIBALI VYA KUMILIKI SILAHA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

2 months ago
SIMBA YAPEWA MCHONGO

SIMBA YAPEWA MCHONGO

5 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?