• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema Tanzania ina mtandao mkubwa zaidi wa barabara kulinganisha na nchi yoyote ukanda wa Afrika Mashariki.

Pia, Ulega amesifu jitihada za Watanzania kujenga taifa lao kwa nguvu na maarifa yao.

Akizungumza Dar es Salaam, Ulega alisema kwa ujumla Tanzania ina mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 182,000 ambapo kilometa 16,000 zikiwa za lami.

Ingawa hakutaja mtu au tukio lolote, maelezo ya Ulega ni kama majibu dhidi ya madai yaliyotolewa juzi na Rais wa Kenya, William Ruto.

Rais Ruto, alidai Kenya ina mtandao mkubwa zaidi wa barabara za lami, ukilinganisha na nchi nyingine jirani.

“Wenzetu wamesema wana kilometa 20,000 za lami. Na wanasema kiwango hicho ni kikubwa kuliko barabara za lami zote zilizopo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Hata hivyo, sisi peke yetu tuna kilometa 16,000. Jirani zetu Uganda wana kilometa 6,100.

“Ukijumlisha kilometa za lami za Tanzania na Uganda, tayari unakuwa umevuka kiwango cha lami cha Kenya. Kwa hiyo, zile takwimu kuhusu sisi na wenzetu wa Afrika Mashariki hazikuwa sahihi,” alisema Ulega.

Akitoa taarifa zaidi, Ulega alisema kuna mtandao wa kilometa 5,100 ambazo zinajengwa nchi nzima na kuna mikataba ya ujenzi wa kilometa 3,700 za lami, ambazo zimesainiwa, zinasubiri kuanza ujenzi wake.

“Jambo zuri zaidi kuhusu Tanzania wakati tunapata Uhuru, tulikuwa na kilometa za lami zisizozidi 600. Zaidi ya kilometa 15,000 tumezijenga wenyewe kwa nguvu zetu.

“Kuna jirani zetu walikuta wakoloni wamewajengea maelfu ya kilometa za barabara. Sisi waasisi wetu walijua hatuna mjomba wala shangazi wa kutujengea, na tumefanya tulichofanya kwa nguvu na maarifa yetu wenyewe, alisema Ulega.

Juzi, Rais Ruto alitumia takwimu za barabara Kenya, akijaribu kujenga hoja kwanini bei ya mafuta nchini kwake ni kubwa kuliko Tanzania, ingawa nchi zote mbili zina bandari.

“Bei ya mafuta Kenya, inaakisi ukweli tunahudumia mtandao mkubwa zaidi wa barabara za lami kuliko nchi zote za jirani ukiziunganisha kwa pamoja. Sisi tuna mtandao mkubwa zaidi kuliko wengine.

“Zaidi ya kilometa 20,000 tulizonazo, tunajenga kilometa nyingine za lami 6,000. Nchi nyingine zimetumia miaka 60 kujenga kilometa 6,000 za lami.”

Ulega alizungumza hayo jijini Dar es Salaam jana, katika tukio la kusainiwa mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya Bonde la Mto Msimbazi.

Previous Post

NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

Next Post

BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

Next Post
BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAISHA HAYANA ‘EXTRA TIME’, TIMIZA WAJIBU WAKO 2026

MAISHA HAYANA ‘EXTRA TIME’, TIMIZA WAJIBU WAKO 2026

4 months ago

Tume ya Uchaguzi itangaza ratiba mpya ya uchaguzi

8 months ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?