• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH, Dodoma

BAADA ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kutekeleza ahadi aliyoitoa katika kampeni za uchaguzi mkuu, mwaka jana kwa kutoa sh. bilioni 200 za uwezeshaji vijana, serikali imeweka wazi mikakati sita itakayoinua mitaji ya biashara na kampuni changa kupitia programu ya kitaifa ya uwezeshaji vijana kiuchumi.

Mwongozo wa utekelezaji programu hiyo, umejikita kuweka viwango vya ufanisi, uwazi, uwajibikaji kwa wakopaji na wakopeshaji wa fedha hizo, kuainisha utaratibu wa utoaji, usimamizi na urejeshaji mikopo, sifa za wakopaji, mifumo ya ufuatiliaji na tathmini.

Katika kutekeleza programu hiyo, fedha hizo zitatolewa kupitia sekta zinazowagusa vijana kupitia kilimo, madini, mifugo, uvuvi, viwanda, biashara, habari, utamaduni, sanaa, michezo, elimu, sayansi na teknolojia, mawasiliano na teknolojia ya habari, maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa uamuzi wa kuanzisha wizara hiyo, kwani anatambua nafasi na mchango mkubwa wa vijana katika maendeleo ya taifa.

FURSA ZA MIKOPO

Nanauka alisema hadi kufikia Aprili, mwaka huu, maombi 30,384 ya mikopo yenye kuhusisha miradi ya vijana yamepokelewa na yanaendelea kufanyiwa uchambuzi.


“Katika utekelezaji wa programu ya kitaifa kuwezesha vijana kiuchumi, kiasi cha sh. bilioni 48.6 kimetolewa kwa awamu ya kwanza katika sekta za uzalishaji na huduma ambazo ni kilimo, mifugo, uvuvi, biashara, viwanda vidogo, sanaa, ubunifu, maendeleo ya jamii, teknolojia na huduma za kidijitali.


Aliongeza: “Uwekezaji katika sekta hizo umezingatia maeneo yenye fursa kubwa za ajira na uzalishaji mali ambapo vijana wengi wanajishughulisha.”

Waziri huyo, alibainisha kuwa, awamu ya kwanza utekelezaji wa programu itakapokamilika, inatarajia kunufaisha vijana 10,000.

Pia, alisema katika awamu ya pili ya utekelezaji programu hiyo, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imepokea sh. bilioni 2.5 ambazo zinatarajiwa kunufaisha vijana 888 kupitia miradi 36 katika sekta za viwanda, biashara ndogo, kilimo, uvuvi na mifugo ambapo ajira 4,440 zinatarajia kuzalishwa.

“Wizara itaendelea kuhakikisha mikopo inayotolewa inawanufaisha makundi yote ya vijana kwa usawa bila kujali itikadi zao au maeneo yao ya kijiografia,” alibainisha.

BENKI YA VIJANA

Waziri huyo alisema wizara yake itafanya utafiti wa uanzishwaji benki ya vijana kwa lengo la kuchambua kwa kina kuwepo taasisi maalumu ya kifedha itakayojikita katika mahitaji ya vijana.

Alisema dhamira ya serikali ni kuweka msingi wa mfumo wa kifedha unaoendana na mazingira, uwezo wa vijana hususan wale wanaoanza shughuli za kiuchumi ili kuondoa vikwazo vilivyopo katika upatikanaji mitaji.

“Benki ya vijana itakuwa chombo muhimu cha kimkakati kitakachowezesha upatikanaji huduma za kifedha zilizo rafiki kwa vijana, kuchochea ubunifu wa bidhaa za kifedha zinazolingana na mahitaji yao, kupanua wigo wa uwekezaji vijana na kuongeza ajira,” alisisitiza.

UTOAJI MAFUNZO

Katika kuimarisha ukuzaji biashara na uwezeshaji vijana kiuchumi, alisema serikali itaendelea kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu ujasiriamali na ujuzi wa usimamizi biashara kwa vikundi vya vijana nchini.


Pia, alisema wizara itakarabati vituo vitatu vya mafunzo kwa vijana vya Sasanda, Ilonga na Marangu kutoa mafunzo ya muda mfupi katika fani za kilimo biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na ujasiriamali.

Alisema serikali itafanya utafiti wa uanzishwaji vituo vya ubunifu vya kitaifa kwa vijana na kuanzisha vituo vya ubunifu kwa vijana (VIJANA Hub).

JUKWAA LA VIJANA

Akizungumzia majukwaa ya vijana, alisema majukwaa hayo, yalizinduliwa katika mikoa sita ambayo ni Dar es Salaam, Singida, Mwanza, Shinyanga, Mtwara na Tabora.

Kupitia majukwaa hayo, alisema vijana 7,500, walihudhuria huku zaidi ya washiriki 20,000,000 walifuatilia kupitia mitandao ya kijamii.

Alisema lengo la majukwaa hayo ni kukutanisha vijana wa makundi mbalimbali wajadili kwa kina masuala yanayohusu maendeleo ya vijana katika ngazi mbalimbali za vijijini na mijini kisha kutoa mapendekezo namna bora ya ushiriki katika ujenzi wa taifa.

UCHAMBUZI WA FURSA

Kwa mujibu wa Nanauka, uchambuzi wa fursa utafanyika kwa lengo la kubaini na kutambua fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali na kukusanya taarifa muhimu zitakazowezesha kuwashirikisha vijana kuhusu fursa hizo.

Alisema hatua hiyo italenga kuhakikisha vijana wanapata uelewa sahihi wa rasilimali na nafasi zilizopo katika mazingira yao,  wazitumie kikamilifu kwa maendeleo yao binafsi na ya jamii.

MAKUZI KWA VIJANA

Nanauka alisema wizara itaendelea kuandaa na kuratibu utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Mafunzo ya Stadi za Maisha.

“Kuandaa programu ya kitaifa ya kushughulikia masuala ya ustawi wa vijana, kuandaa mwongozo wa msaada wa kisaikolojia kwa vijana na kuratibu utoaji wa huduma ya msaada wa kisaikolojia kwa vijana,” alisisitiza.

MAOMBI YA FEDHA

Nanauka aliliomba Bunge katika mwaka 2026/27 kuidhinishiwa sh. bilioni 35.9 ambapo kiasi cha sh. bilioni 30.1 ni kwa matumizi ya kawaida.

Alifafanua kuwa, sh. bilioni 1.2 ni kwa ajili ya mishahara na sh. bilioni 28.8 kwa matumizi mengineyo.

Vilevile, alisema kiasi cha sh. bilioni 5.8 zitatumika katika utekelezaji miradi ya maendeleo.

Kati ya fedha hizo, sh. bilioni tano ni fedha za ndani za maendeleo na sh. milioni 853 ni fedha za nje za maendeleo.

MAONI YA KAMATI

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Regina Malima, alisema kamati hiyo inashauri serikali iandae kanzidata itakayobainisha na kuonesha idadi ya vijana waliopo katika ajira rasmi na ambao wamejiari katika sekta binafsi na isiyo rasmi.

Alisema hatua hiyo itawezesha kutambua mchango wa vijiana katika kuchangia pato la taifa.

“Serikali iendelee kuanisha fursa za ajira katika utumishi wa umma, sekta binafsi ndani na nje ya nchi ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini,” alisisitiza.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ABADILI MATUMIZI YA FEDHA

Next Post

ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

Next Post
ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AKABIDHIWA NYARAKA ZA KAZI

RAIS DK. SAMIA AKABIDHIWA NYARAKA ZA KAZI

6 months ago
AMANI YAWAIBUA WABUNGE

AMANI YAWAIBUA WABUNGE

4 months ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?