• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WARIZI SANGU AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE MTAKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WARIZI SANGU AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE MTAKA
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka leo Machi 20, 2026, katika Ofisi za PSSSF, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, katika kikao cha viongozi hao wamejadili kuhusu hatua za maandalizi kuelekea sherehe za Mei Mosi, 2026 amabazo zitafanyika kitaifa Mkoani Njombe.

Akizungumza Waziri Sangu amesema, Mei Mosi ni moja ya tukio kubwa na linaweza kuwa ‘brand’ mkoa unaoadhimisha vizuri au vibaya, hivyo ametaka uratibu wa shughuli mbalimbali katika maadhimisho hayo kufuatilia kwa karibu ili wafanye vizuri.

“Nikushukuru kwa kikao hiki nadhani sasa tutakwenda pamoja kila hatua na mimi nitahakikisha kwa upande wangu ninatekeleza wajibu wangu ipasavyo ili kufanikisha jambo hili” amesema Sangu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alisema lengo la kukutana nae ni kumjulisha kuhusu uenyeji wa mkoa wake kwenye sherehe za Mei Mosi kwa mwaka huu wa 2026.

“Baada ya kupokea barua ya Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuhusu sherehe za Mei Mosi mwaka huu 2026, kama viongozi wa mkoa tukaona ni vema kukutana na wewe Waziri mwenye dhamana ili kukujulisha kuhusu wenyeji wa mkoa wetu kwenye sherehe za mwaka huu,” amesema Mtaka

Vilevile, amesema Mei Mosi ya mwaka huu 2026 itakuwa ya Kazi, lakini Kazi inayojenga misingi ya utu kwa watumishi wa umma na binafsi.

Katika kikao hicho alishiriki pia Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Dk. Stephen Nindi na viongozi wengine wa mkoa huo.

Previous Post

PALE PANAPOUMA ZAIDI

Next Post

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

Next Post
SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII

RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII

7 months ago
WANASIASA WAELEZA IMANI YAO TUME YA JAJI CHANDE

WANASIASA WAELEZA IMANI YAO TUME YA JAJI CHANDE

4 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?