• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YATAMBIA REKODI LIGI KUU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 4, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
YANGA YATAMBIA REKODI LIGI KUU
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

LICHA ya kusuasua katika mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Yanga imejivunia rekodi yake ya kutofungwa mchezo wowote katika michuano hiyo hadi sasa.

Yanga ambayo ndiyo kinara wa Ligi Kuu Bara msimu huu, hadi sasa haijapoteza mechi yoyote ikishinda mehi 11 na kutoka sare tano katika mechi 16 ilizocheza, ikivuna pointi 38.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ally Kamwe alisema msimu huu timu yao imefanya vizuri zaidi  ya msimu uliopita.

“Nawapongeza wachezaji wa timu yetu, wameonyesha juhudi kubwa katika kusaka matokeo mazuri, licha ya  kukabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo, pamoja na kukabiliwa na wachezaji wengi kuwa majeruhi,”alisema.

Kamwe alisema anajua mzunguko wa pili, utakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu huwa inajipanga kupata matokeo mazuri.

“Pamoja na kusuasua katika mechi tatu mfululizo tulizocheza hivi karibuni, lakini tunajivunia rekodi nzuri tulioyoiweka kwa kumaliza mzunguko wa kwanza bila ya kupoteza mchezo wowote,” alisema.

Kamwe alisema hivi sasa timu yao inaendelea na maandalizi kwa mechi zake za mzunguko wa pili na wanachohitaji ni  kupata ushindi katika mechi zilizobakia.

Ofisa huyo alisema msimu huu wamefanya vizuri zaidi tofauti na ilivyokuwa katika msimu uliopita kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kutoka kwa viongozi, wanachama, wadau na wachezaji kwa ujumla.

Yanga kesho saa 12:30 jioni itashuka dimbani kupambana na Tanzania Prisons katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Previous Post

KARIA ATAKA WANAMICHEZO KUDUMISHA AMANI

Next Post

BILIONI 400/- KUJENGA ARENA YA KISASA

Next Post
BILIONI 400/- KUJENGA ARENA YA KISASA

BILIONI 400/- KUJENGA ARENA YA KISASA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

7 months ago
MWIGULU ASISITIZA UHURU WA KUABUDU

MWIGULU ASISITIZA UHURU WA KUABUDU

4 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?