Na MWANDISHI WETU, Arusha
BAADA ya kufanya vizuri, winga wa TRAUnited, Ramadhan Chobwedo amezitikisa timu za Simba na Yanga na kuanza kumfuatilia.
Taarifa iliyopatikana, imeeleza kuwa nyota huyo inasemakana tayari ameingia mkataba wa awali na klabu ya Simba.
Simba juzi iliambulia suluhu katika mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Baada ya kumalizika pambano hilo, inasemekana viongozi wa Simba walifanikiwa kumpatia mkataba wa awali mchezaji huyo lengo likiwa ni kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
“Chobwedo tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa awali kujiunga na Simba baada ya msimu huuutakapomalizika,”alisema kiongozi moja wa Wekundu wa Msimbazi ambaye hakupenda kutajwa jina lake.
Alipoulizwa Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema Chobwedo ni mchezaji mzuri na kila timu inatamani kuwa naye.
Aliongeza kuwa kama kocha wao, Steve Barker atampendekeza basi viongozi watafanya mazungumzo ya kumsajili.
“Ni mchezaji mzuri na mwenye nguvu kila timu inatamani kuwa na mchezaji kama huyo, lakini niwaambie tu kuwa hawatasajili mchezaji yeyote hadi mwalimu wao Steve Barker atakapotoa mapendekezo,” alisema Ahmed.
Lakini taarifa zaidi zimeeleza kuwa mchezaji huyo anafuatiliwa na Yanga ambapo juzi walituma watu wao kuangalia kiwango cha nyota huyo.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa Yanga nao jana usiku walikuwa wanajaribu kuzungumza na Chobwedo.
Awali imedaiwa kuwa Chobwedo alikuwa anatembea na mkataba wa Singida BS.
Ofisa Habari wa TRA, Christina Mwagala alipoulizwa alisema mawazo yao yapo kwa ajili ya mchezo dhidi ya Namun go FC wa Kombe la FA.
“Mambo ya usajili muda wake bado, nafahamu Chabwedo bado mchezaji wetu, hivi sasa tunaangalia safari ya kwenda Ruangwa kucheza na Namungo FC,”alisema kwa ufupi kiongozi huyo.
Wakatihuohuo, ChobwedoalisemakuwaSimba ina bahati kwani walijipanga kuifunga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao jijini Arusha, alisema kila mchezaji alipenda kushinda mchezo huo lakini imekuwa bahati mbaya.
“Simba wana bahati sana, tulijipanga vizuri kuwafunga, lakini wana bahati kwa vile tumewakosa, bao letu lilikataliwa,” alisema.
Hata hivyo, mchezaji huyo wa TRA amesema ana imani timu yao itaendelea kufanya vizuri kutokana na kikosi imara walicho nacho.
Pia, amekiri kuwa ligi hiyo ni ngumu kutokana na timu nyingi kujipanga vizuri msimu huu.
“Ukweli ligi yetu ni ngumu, kila timu inapenda kufanya vizuri, mara nyingi zikiwa nyumbani,”alisema Chobwedo.




