• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

ROSTAM ANUNUA SONGO SONGO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
ROSTAM ANUNUA SONGO SONGO
0
SHARES
55
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Taifa Gas Tanzania Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz, imeingia makubaliano ya kununua sehemu ya hisa katika biashara ya gesi ya Orca Energy Group Inc. nchini Tanzania, hatua inayotajwa kuwa ya kihistoria katika sekta ya nishati.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 13, 2026, Taifa Gas itanunua asilimia 49 ya hisa za kampuni ya PAE PanAfrican Energy Corporation (PAEM), huku kampuni ya Amber Energy Investment L.L.C-FZ ikichukua asilimia 51 iliyobaki.

Makubaliano hayo yanahusisha uuzaji wa asilimia 100 ya biashara ya Orca nchini Tanzania, ikiwemo haki zake zote katika mradi wa gesi wa Songo Songo, ambao ni mhimili muhimu wa uzalishaji wa gesi kwa matumizi ya umeme na viwanda.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya umiliki katika sekta ya gesi, ambapo wawekezaji wa ndani wanaanza kuchukua nafasi kubwa zaidi katika rasilimali za kimkakati.

Akizungumzia maendeleo hayo, Rostam alisema mpango huo umechukua muda mrefu kuandaliwa na unalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika zaidi na rasilimali zake za asili.

Alisema kuongezeka kwa umiliki wa Watanzania kutasaidia kuimarisha uchumi wa ndani na kuongeza uwekezaji katika sekta ya viwanda inayotegemea nishati ya gesi.

Aidha, alibainisha kuwa mradi wa Songo Songo umechangia kwa kiasi kikubwa mapato ya serikali, ajira na maendeleo ya ujuzi kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Orca imeeleza kuwa uamuzi wa kuuza biashara yake umetokana na tathmini ya kina ya changamoto za uendeshaji nchini.

Kutokana na hali hiyo, Orca imeona ni busara kuuza biashara hiyo ili kulinda maslahi ya wanahisa wake.

Shughuli za Orca nchini zilikuwa zinaendeshwa kupitia kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Limited, ambayo inashikilia haki na wajibu katika makubaliano ya uzalishaji gesi kati yake, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Serikali.

Baada ya kukamilika kwa mauzo hayo, Orca haitakuwa tena na umiliki wowote katika biashara yake ya Tanzania wala wajibu wowote unaohusiana na shughuli hizo.

Hata hivyo, kukamilika kwa makubaliano hayo kunategemea kupatikana kwa idhini za kisheria kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Tume ya Ushindani na Waziri mwenye dhamana ya mafuta.

Wachambuzi wa masuala ya nishati wanasema hatua hiyo inaweza kuongeza ushiriki wa wazawa, kuimarisha ushindani na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya gesi nchini Tanzania.

Previous Post

IGP MSTAAFU MANGU AWAASA WATANZANIA KUEPUKA VISHAWISHI VYA KUVUNJA AMANI

Next Post

GWAJIMA AKATA MZIZI WA FITNA ‘ISHU’ BEGA NA NYETI KUTOWEKA

Next Post
GWAJIMA AKATA MZIZI WA FITNA ‘ISHU’ BEGA NA NYETI KUTOWEKA

GWAJIMA AKATA MZIZI WA FITNA ‘ISHU’ BEGA NA NYETI KUTOWEKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SMZ KUTENGA TRIL. 1/- BAJETI WIZARA YA ELIMU

SMZ KUTENGA TRIL. 1/- BAJETI WIZARA YA ELIMU

4 months ago
TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA

TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?