• ePaper
Tuesday, May 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 14, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa, Makala
0
TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ASHURA  ASSED

VIONGOZI wa dini ni mhimili muhimu, wenye ushawishi na nguvu ya kuleta mabadiliko katika jamii.

Amani ni nguzo imara inayojenga umoja, utulivu, na ustawi wa jamii kuanzia ngazi ya familia.

Jamii inatakiwa kuwa ni mfereji wa darasa la maadili mema na heshima, kuimarisha msingi mkuu wa amani.

Kudumisha amani ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii bila hivyo hakuna jambo linalofanyika ,amani ndiyo muhimili wa maendeleo ya kila kitu.

Hivi karibuni kwa nyakati tofauti viongozi hao walizungumza na mwandishi wa makala hii kuhusu tume ya uchunguzi iliyoundwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuchunguza vurugu za Oktoba 29,  wakielezea matumaini yao juu ya tume hiyo, katika kudumisha amani na mshikamano kwa Watanzania.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo, Walid Alhad Omary Kawambwa, amewataka viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele katika nafasi zao, kuhubiri umuhimu wa amani na matunda yake.

Sheikh Walid ameitaka jamii kuelewa kuwa viongozi wa dini wanapohamasisha amani na usalama nchini wanaona mbali, kwa amani itawapa fursa ya kufanya ibada.

 “Viongozi wa dini tuna wajibu wa kuhamasisha amani na usalama wa taifa, kwa kuwa ujumbe waliopewa Mitume ni kufundisha na kuhimiza amani, viumbe waweze kumuabudu Mola vizuri kwa utulivu, hivyo tunapohimiza amani ‘siyo wapambe wa mtu ni kutekeleza wajibu wetu na kutetea vizazi vya taifa hili na lijalo,”alisema Sheikh Walid.

Alisema amani ndiyo chemchem ya kila aina ya maendeleo ambayo kila mwananchi anajivunia.

“Bila nyinyi viongozi wa dini, ambao mmekuwa mkihubiri amani ya viongozi wetu misikitini na makanisani, kufanya kazi hiyo na kusoma dua ya Taifa letu tusingefika hapa tulipofika

“Sisi viongozi wa dini ni kundi muhimu kwa vile tuna wafuasi wengi, tukizungumza na waumini wetu maneno yanawaingia moyoni, yanakaa na yanaaminika,”alisema.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Sheik, Alhad Dk. Musa Salim, alisema kila mmoja, anayo nafasi ya kujenga nchi kupitia umoja na amani kudumisha maendeleo.

Alisema uvunjifu wa amani, unaweza kusababisha njaa na vifo, ndiyo maana inatakiwa kulindwa kwa nguvu zote, ni vyema Tanzania ikaendelea kushirikiana na mataifa mengine jirani, kuimarisha amani na ushirikiano,

“Tunatakiwa kutoa matamko yanayoondoa taharuki au mgawanyiko ni muhimu viongozi dini kuhamasisha maridhiano na subira , kuwa mstari wa mbele kuongoza jamii na kushauri kwa hekima kudumisha amani na mshikamano.

Kwa mujibu wa Shekh huyo, vitabu vitakatifu vinatoa mafunzo yanayohimiza uvumilivu na amani, akisisitiza kuwa hasira haijawahi kujenga jamii yenye amani, hivyo viongozi wa dini wanayo fursa ya kushauri na kusuluhisha mapema mgogoro isiyo na tija kujenga amani ya nchi.

“Nchi inapokumbwa na changamoto, viongozi wa dini wanapaswa kushauri kwa hekima na  busara, maana vitabu vitakatifu vinatukumbusha kuwa tusifanye haraka kukasirika rohoni, maana hasira hukaa vifuani mwa wapumbavu na  haijawahi kujenga hekima na busara.

Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste, Jimbo la Kiwalani, Peter Mshasha alisema, Tanzania imeendelea kujivunia sifa ya kuwa taifa lenye amani. Upo mshikamano na ustahimilivu wa kijamii licha ya changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika jamii.

Alisema, msingi wa utulivu huo kwa miaka mingi umejengwa juu ya uvumilivu, kuheshimiana na uwezo wa viongozi wa kisiasa, kijamii na kidini kusimamia maridhiano pale migogoro inapojitokeza.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo, maisha ya kuishi pamoja kwa amani ni dhana inayosisitiza uvumlivu, kuheshimiana bila ubaguzi wa rangi, kabila, jinsia, dini, itikadi na kushirikiana kati ya watu wa asili,  tamaduni na mataifa tofauti, 

Ni muhimu kutatua migogoro kwa njia ya amani bila vurugu, hivyo misingi ya maisha hayo ni haki za binadamu, usawa na mshikamano wa kijamii na ulinzi wa amani ni jukumu la kila mmoja.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kujenga taifa lenye mshikamano, kutokama na maridhiano. Hata hivyo mafanikio hayo yanahitaji kuendelezwa kwa kuzingatia misingi ya maridhiano, kuheshimiana na kusimamia haki kwa busara,”alisema.

Alisema, tume iliyoundwa na Rais Dk. Samia ya kuchunguza vurugu za Oktoba 29, mwaka jana ni hatua muhimu katika kutafuta amani haipaswi kubezwa, inatakiwa kuendelea kuwa sehemu ya utamaduni wa kitaifa.

Kuhusu Tume iliyoundwa na Rais Dk. Samia ya kuchunguza vurugu za Oktoba 29, mwaka jana, alisema ni dhamira njema ya Rais Dk. Samia ya kudumisha amani na kuliweka taifa pamoja katika njia inayofaa.

Alisemia tume hiyo ina umuhimu mkubwa, katika kubaini chanzo cha changamoto hiyo na kukiziba kwani kipindi hicho kilikuwa ni kigumu kwa wananchi.

Alisema matarajio ya viongozi wa dini ni kuona tume hiyo ikija na majibu ya kina yatakayosaidia siyo kujua chanzo cha vurugu hizo, bali kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia matukio kama hayo kutojirudia siku zijazo.

Mchungaji Mussa Mchomi kutoka Kanisa la Pentecost, Jimbo la Kinyerezi alisema, matokeo ya uchunguzi huo yakitekelezwa kwa misingi ya haki  yataimarisha amani ya kila, sekta hali itakayochochea kukua kwa ufanisi wa Watanzania.

Akizungumzia matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba 29, Mchungaji Mchomi alisema miundombinu iliharibiwa, ikiwemo vituo vya mwendo kasi, vituo vya polisi viliharibiwa, hali iliyosababisha matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya ukarabati.

Alisema fedha zinazotumika kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa, hali hiyo inarudisha nyuma jitihada za kukuza uchumi na kuboresha huduma kwa wananchi.

Mfanyabiashara wa nafaka kutoka soko la Tandika Hassan Juma, alisema tume hiyo imeundwa na watu wenye heshima, anaamini haiwezi kusema uongo hivyo wananchi wanapaswa kusubiri matikeo yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.

Alisema ni muhimu wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha unapohitajika kwa tume kupata suluhisho la kudumu litakalosaidia kuimarisha amani ya nchi.

Juma alisema wajumbe wa tume hiyo wamechaguliwa kwa kuzingatia uadilifu, taaluma na uzoefu unaohitajika katika kushughulikia masuala nyeti ya kitaifa.

Alisema ana matumaini kuwa mapendekezo yatakayotolewa yatasaidia siyo tu kudhibiti matukio ya vurugu, bali kujenga mazingira ya amani, mshikamano na maendeleo endelevu ya taifa.

Mama wawili ni mama lishe alisema, amani ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi, kwani kwa kipindi kile cha muda mfupi wa zile vurugu hakuna biashara iliyofanyika.

Alisema bila amani, shughuli nyingi za kiuchumi hukwama na kusababisha hasara kwa wananchi na taifa, hivyo ni muhimu kuhakikisha utulivu unadumishwa wakati wote  kwa maendeleo ya taifa.

TUME

Tume hiyo iliyoundwa Novemba 19, mwaka jana, ikioongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Chande ina  wajumbe saba.

Wajumbe hao ni Jaji Mkuu mstaafu, Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, IGP mstaafu, Said Mwema na Dk. Stargomena Tax, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Paul Meela, mwanadiplomasia na Luteni Jenerali wa Jeshi mstaaafu.

Novemba 20, mwaka jana, Rais Dk. Samia, aliizindua Tume hiyo na kuipa siku 90 za kufanya uchunguzi huo hadi Februari 20, mwaka huu.

Machi 11, mwaka huu, Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Parfait Onanga-Anyanga, alikutana na Rais Dk.Samia alipowasilisha salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Onanga-Anyanga alisema umoja huo unatambua na kupongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania, baada ya matukio ya Oktoba 29, mwaka jana.

Walipongeza uamuzi wa kuunda Tume hiyo na dhamira ya kufanya mazungumzo jumuishi ya kitaifa, kuendeleza mchakato wa mabadiliko ya kikatiba.

Mjumbe huyo alikuwepo nchini kusikiliza maoni ya wadau na kutathmini hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha utulivu wa kisiasa, mshikamano wa kitaifa na kuendeleza misingi ya utawala wa sheria kufuatia matukio ya uvunjifu wa amani ya kabla na wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka jana.

Katika mazungumzo yao, mjumbe huyo alisema UN inaendelea kuitambua Tanzania kama nchi yenye historia ya muda mrefu ya amani, utulivu wa kisiasa na mshikamano wa kitaifana kuthamini mchango wake katika juhudi za kulinda na kuimarisha amani barani Afrika.

Katika ziara yake, Onanga-Anyanga alikutana na kuzungumza na viongozi wa taasisi mbalimbali nchini, ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahakama ya Tanzania, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja viongozi wa vyama vya siasa.

Previous Post

DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

Next Post

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

Next Post
UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RUFANI YA SENEGAL KUSIKILIZWA

RUFANI YA SENEGAL KUSIKILIZWA

2 months ago
NADO, MASAGALA WATOA NENO STARS

NADO, MASAGALA WATOA NENO STARS

5 months ago

Popular News

  • MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAKONDA ASISITIZA KULINDWA KWA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA CHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?