• ePaper
Thursday, April 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 21, 2026
in Burudani, Habari, Kimataifa, Kitaifa, Michezo
0
‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

WALIMBWENDE kutoka zaidi ya nchi 130 duniani wanatarajiwa kuipamba Tanzania watakapochuana katika mashindano ya ‘Miss World’ yatakayofanyika mwakani.

Mashindano hayo makubwa ya urembo duniani yatafanyika nchini kwa mara ya kwanza huku serikali ikijidhatiti kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha hafla hiyo inabamba.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa uenyeji wa mashindano hayo yatakayofanyika mwakani nchini.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo warembo wa dunia wakiongozwa na Opal Suchata (Miss World), Hasset Dereje (Miss World Africa 2025) na Latricia Ian ambaye ni Miss World Tanzania 2026.

 “Serikali tuna mpango wa kuandaa mashindano haya mara mbili au tatu mfululizo kwa sababu tumeona baadhi ya nchi zimeandaa mara nyingi kama Afrika Kusini wameandaa mara nne.

“Tukio hili linakwenda kuweka historia kubwa kwani Tanzania tunakwenda kuwa mwenyeji wa mashindano ya Miss World ya 74, tunaweka historia kwa ukanda wa Afrika ni nchi ya pili ilianza Afrika Kusini na Afrika Mashariki tunakuwa wa kwanza,” alisema.

Makonda alisema kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kunalenga kuitangaza Tanzania kimataifa na kukuza sekta za utalii, sanaa na michezo.

“Mbali ya mashindano ya AFCON kufanyika Tanzania mwakani tutakuwa na tukio lingine kubwa la Miss World, hatua hii itafanya nchi kuwa kitovu cha matukio ya kimataifa, hii ni fursa kwa Watanzania kwani tunakwenda kuiweka nchi duniani.

“Kwani mashindano haya yanatazamwa na watu wengi duniani, zaidi ya bilioni mbili hivyo ni muda wa Watanzania kutumia fursa hii muhimu, kwa sababu sekta ya urembo inabeba ajira nyingi kwa vijana ikiwemo wapambaji kucha,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Miss World, Julia Morley, alisema mashindano hayo yataleta faida kubwa kwa Tanzania ikiwemo kukua kwa utalii nchini kutokana na idadi ya nchi ambazo zitashiriki.

“Mashindano haya yatashirikisha nchi 130, kutakuwa na wageni zaidi ya 200 hivyo Tanzania itapata fursa ya kukuza utalii wao, pia itajitangaza na kufahamika kutokana na televisheni zaidi ya 100 zitakuwa zinaonyesha tukio hili,” alisema.

Aliongezea kuwa, mashindano hayo yatadumu zaidi ya siku 28 kutokana na uwepo wa mashindano madogo madogo ambayo warembo watashiriki kabla ya kuingia fainali.

Previous Post

BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

Next Post

MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

Next Post
MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

1 month ago

GAMONDI AJA KIVINGINE KUIVAA MOROCCO AFCON

4 months ago

Popular News

  • NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATOA MAAGIZO ALAT

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIPOTI YA KUPONYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, MAFUNZO HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?