• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 21, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
MUDATHIR KUIKOSA SIMBA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KIUNGO nyota wa Yanga, Mudathir Yahya, anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaopigwa Mei 3, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mudathir ataukosa mtanange huo kufuatia jana Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), kumfungia kucheza mechi tatu na faini ya sh. milioni moja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji, Ibrahim Abraham katika mechi ya ligi hiyo iliyopigwa hivi karibuni katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TPLB, adhabu hiyo imetokana na kanuni ya 14.5 (5.2) ya ligi kuhusu udhibiti wa wachezaji.

Aidha, kamati hiyo iliitoza klabu ya Simba faini ya sh. milioni 10 kwa kosa la shabiki wa timu hiyo kumrushia chupa ya maji mwamuzi msaidizi namba mbili baada ya kunyoosha kibendera kuashiria mchezaji wa Simba kuotea katika mtanange dhidi ya Azam FC.

“Klabu ya Azam FC imetozwa faini ya sh. milioni tano kwa kosa la viongozi wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji kutumia mlango usio rasmi wa kuingia uwanjani kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:21 ya ligi.

“TRA United na Simba zimetozwa shilingi milioni tano kila moja kwa kosa la walinzi wa klabu hizo (Stewards) kupigana mara baada ya ya timu hizo kuwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, “ ilieleza.

“Vilevile klabu ya Singida Black Stars ya mkoani Singida imetozwa sh. milioni tano kwa kosa la viongozi wake wawili kuingia uwanjani na kumwaga vimiminika, viongozi hao walifanya tukio hilo lililotafsiriwa kama kitendo vinavyoashiria imani za kishirikina,” ilieleza taarifa hiyo.

Previous Post

‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWINYI APANIA KUPAISHA UCHUMI

DK. MWINYI APANIA KUPAISHA UCHUMI

7 months ago
ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

1 week ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?