• ePaper
Saturday, May 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

WATALAMU WATAJA KINGA ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 16, 2026
in Makala
0
WATALAMU WATAJA KINGA ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na JOE   NAKAJUMO

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limesema magonjwa yasiyoambukiza yanachukua nafasi ya kwanza duniani kwa kuua watu.

Miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza ni shinikizo la  damu, kisukari, matatizo ya figo,moyo,saratani na ini.

Haya yanaua kimya kimya. Yanachochewa zaidi na ulaji usiofaa wa vyakula vyenye mafuta mengi,chumvi nyingi,sukari kupita kiasi na nishati nyingi.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 41,hufariki kila mwaka duniani kutokana na magonjwa yasiyoambukiza,sawa na asilimia 74 ya vifo vyote. Kugharamia matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza,dunia kwa mwaka jana 2025, zilitumika zaidi ya dola za Marekani trilioni mbili kwa mwaka.

Kwa mfano,nchini Tanzania,ukibainika figo zimefeli,uchujaji damu unagharimu siyo chini ya sh.150,000 kwa kila awamu ya uchujaji na wastani wa awamu,siyo chini ya mara tatu kwa wiki.

Tanzania,Wizara ya Afya,inasema zaidi ya asilimia 34 ya vifo vinavyotokea,vinatokana na magonjwa yasiyoambukiza.Yanayoongezeka kwa kasi ni saratani,kisukari,shinikizo la damu,magonjwa ya moyo, afya ya akili,magonjwa ya figo, selimundu na baadhi ya magonjwa ya njia ya hewa.

SARATANI TANZANIA

Kwa ugonjwa wa saratani,Shirika la Afya Duniani,limetoa takwimu kwamba jumla ya wagonjwa wapya 42,000 hadi 45,000 wanapatikana kila mwaka nchini Tanzania. Saratani ziko za aina mbalimbali, zinazowakabili wanawake na wanaume.

Taarifa inasema saratani ya shingo ya kizazi inaongoza kwa asilimia 30 ya wagonjwa,ukilinganisha na asilimia 15 ya saratani ya titi. Saratani zingine ni tezi dume na utumbo mpana. 

Kwa ugonjwa wa saratani, takwimu zinaonyesha watu milioni 10 wanafariki kila mwaka duniani kwa kuugua saratani za aina  mbalimbali,milioni 18 hufa kwa magonjwa ya moyo,milioni nane wanakufa kwa presha na watu milioni tano hufa kutokana na magonjwa ya kisukari.

Mwezi Machi 2023, Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo,Hospitali ya Taifa Muhumbili,Dk. Hassan Mwamba,alikaririwa akisema utafiti ulionyesha  asilimia 30 ya vifo vyote duniani vinasababishwa na matatizo ya moyo, kutokana na matumizi ya chumvi ya mezani. Wanawake wakiongoza kwa kufa zaidi. Alisema Tanzania, kila mwaka katika vizazi hai 1,000, watoto wanane huzaliwa na matatizo ya moyo.

KEMIKALI SEHEMU ZA SIRI

Meneja wa Maradhi yasiyoambukiza, Zanzibar, Dk. Omar Mohamed Suleiman, alishauri wanawake kuacha tabia ya kutumia vitu vyenye kemikali kama chumvi na tumbaku kuweka sehemu zao za siri.

Alitoa ushauri baada ya kubainika miongoni mwa sababu za kupata saratani ya shingo ya kizazi ambayo inachukua  nafasi kubwa katika maradhi yasiyoambukiza Zanzibar ni matumizi ya kemikali.

Meneja huyo akizungumzia  maradhi yasiyoambukiza na madhara yake, alisema, asilimia kubwa ya wanawake hutumia vitu vyenye kemikali,mbali ya tumbaku na chumvi, pia huweka shabu, asali, ndimu na nyungu.

KANSA YA SHINGO YA KIZAZI

“Matumizi ya vitu hivyo, husababisha kuathirika kiasi kikubwa viungo vya  uzazi na kupata kansa ya shingo ya kizazi. Wanawake wengi wanafanya hivyo kwa kuweka kemikali sehemu zao za siri kwa lengo la kuwaridhisha wenza wao au marafiki wanapofanya tendo la ndoa, hawajui kama yapo madhara wanayoweza kuyapata,”alisema.

Dk. Suleiman alinukuu taarifa ya Wizara ya Afya Zanzibar kwamba kuanzia mwaka 2018 hadi 2024,jumla ya wanawake 32,000,walipimwa saratani ya shingo ya kizazi,kati yao 640 walipatikana na ugonjwa wa kansa ya kizazi ukiwa katika hatua mbalimbali na wanawake 141 walikuwa katika hatua mbaya.

Meneja alifafanua kwamba hali hiyo inaonesha saratani ya shingo ya kizazi ipo na miongoni mwa kichocheo chake kikubwa ni kuweka vitu katika  viungo vya uzazi.

HAIFAI KUJIFUKIZA UDI

Daktari huyo mtaalamu wa magonjwa yasiyoambukiza anadokeza kwamba wapo wanawake wenye kujifukiza udi ili wanukie mwilini. Anaonya ni hatari kwa kuwa moshi wake unakuwa na kaboni ambayo huingia sehemu ya siri na kusababisha athari kubwa.

Mtaalamu wa Afya ya Uzazi, Baba, Mama na Mtoto, Dk. Oscar Mwambapa alisema mwanamke anapoweka vitu vyenye kemikali ndani ya uke wake,vinaharibu mlango wa uzazi kwa kupata mchubuko.

Dk. Mwambapa alieleza kuwa wapo wadudu wanaolinda uke,hivyo kemikali inapoingia ndani,husababisha wadudu kupunguza nguvu za kulinda na kuruhusu kemikali kuingia ndani na kuleta madhara.

Mtalamu huyo alishauri wanawake wasiweke vitu vyenye kemikali ndani ya uke,wala kujisafisha na vitu vya aina yoyote vyenye kemikali na wanapaswa kujua kwamba uke huwa unajisafisha wenyewe. Hakuna haja ya kutumia vitu vitakavyoleta madhara makubwa katika uzazi.

USHAURI WA PROFESA JANABI

Kauli hizi za madaktari zinakumbusha ushauri wa Profesa Mohamed Janabi kuhusu mtindo wa maisha. Kwa sasa Profesa Janabi ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, lenye makao yake makuu, Brazaville, Jamhuri ya Congo. Alianza kuutumikia wadhifa huo,mwaka jana.

Profesa Janabi ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, amekuwa akishauri kwamba ni muhimu kwa jamii kujikita katika kujikinga  na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa yana usumbufu na gharama kubwa kuyatibu.

Alisema hajakataza watu kula,bali anachoshauri ni kula kwa kiasi na chakula bora. Suluhu ya magonjwa yasiyoambukiza ni kubadili mtindo wa maisha, kwa kulala sawasawa,kufanya mazoezi, kuongeza ulaji wa mboga mboga, matunda na kupunguza msongo wa mawazo, anashauri.

Mkurugenzi huyo mpya wa WHO Afrika, alifafanua kwamba magonjwa yasiyoambukiza yanasababishwa na mtindo wa maisha, hususan vyakula. Hivyo, kama mtu ana nia anaweza kuondokana na tatizo hilo.

RATIBA YA KULA

Naye Ofisa wa Lishe wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),Husna Yasin Faraji, alishauri kuhusu muda wa saa za chakula. Anasema  mwili wa binadamu unahitaji saa 10 hadi 12,kukaa bila kula chakula cho chote ili kuwa na mwenendo bora wa afya. Alisema mwili wa binadamu unatakiwa kupumzika kwa saa 10 hadi 12,bila kula, ndiyo maana inashauriwa chakula cha usiku kuliwa saa 12 jioni. Mpangilio mzuri wa muda wa kula ni kunywa chai saa 12 asubuhi, chakula cha mchana saa 6(sita) mchana na usiku saa 12 jioni. (Mawasiliano na Mwandishi WhatsApp 0784291434;email nakajumoj@gmail.com).

Previous Post

SAUTI YA WATANZANIA IHESHIMIWE -DK. SAMIA

Next Post

WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

Next Post
WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AMPA   ZAHIR ZORRO MILIONI 10/-

RAIS DK. SAMIA AMPA   ZAHIR ZORRO MILIONI 10/-

2 months ago
MAJALIWA : MRADI GESI YA LNG KUIKOMBOA LINDI KIUCHUMI

MAJALIWA : MRADI GESI YA LNG KUIKOMBOA LINDI KIUCHUMI

7 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?