• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 28, 2026
in Habari, Kitaifa
0
VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST

NABII Mkuu na Mstahiki Meya wa Amani, Profesa GeorDavie K. Moses, amezindua vitabu viwili—The Kingdom Business na Kuenenda na Viwango vya Utukufu wa Serikali Tukufu ya Ufalme wa Mungu—akisisitiza umuhimu wa jamii kujijenga kiuchumi na kiimani kupitia maarifa ya kusoma vitabu.

Uzinduzi huo ulifanyika juzi katika Kanisa la Ngurumo ya Upako, Kisongo, wilayani Monduli mkoani Arusha, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa GeorDavie alisema vitabu hivyo vimebeba hazina kubwa ya maarifa ya kiuchumi na kiimani, yatakayosaidia jamii kubadilika na kupiga hatua kupitia elimu iliyomo ndani yake.

“Ninafuraha kuzindua vitabu hivi muhimu katika ulimwengu wa sasa. Nimeanza kuviandika kwa muda mrefu, lakini kutokana na majukumu mengi ya kiutumishi, ilichukua muda kuvimaliza. Hatimaye sasa viko tayari kwa manufaa ya jamii,” alisema.

Akifafanua kuhusu kitabu cha The Kingdom Business chenye zaidi ya kurasa 900, alisema kinaelezea kwa kina masuala ya uchumi na nafasi ya fedha katika kumtumikia Mungu, kikilenga kuwajengea watumishi wa Mungu na jamii kwa ujumla uelewa wa umuhimu wa nguvu ya kifedha katika kazi za ufalme.

Alieleza kuwa shughuli nyingi za maendeleo, ikiwemo kazi za kiroho, zinahitaji rasilimali fedha ili kufanikisha utekelezaji wake.

“Hata mipango ya kufanya mikutano ya kimataifa katika nchi kama Ufaransa, Croatia na Ethiopia inahitaji gharama kubwa. Kupitia kitabu hiki, watu watapata maarifa ya namna ya kujiandaa kiuchumi,” alisisitiza.

Kuhusu kitabu cha Kuendana na Viwango vya Utukufu wa Serikali Tukufu ya Ufalme wa Mungu, alisema kinaelekeza namna ya kuelewa misingi, itifaki na utendaji wa kiroho katika ufalme wa Mungu, pamoja na kuwajengea watumishi uwezo wa kukua katika huduma za kinabii.

Alisema kitawasaidia watumishi wa Mungu kufahamu huduma ya kinabii na namna nguvu yake inavyotenda kazi katika kudhihirisha utukufu wa Mungu.

Kwa upande wake, Msemaji Binafsi wa Nabii Mkuu, Askofu Willy Ackyoo, alisema wamefurahi kwa tukio hilo la kihistoria la uzinduzi wa vitabu hivyo viwili muhimu ikiwa ni mwendelezo wa kazi kubwa inayofanywa na Nabii Mkuu Profesa GeorDavie ikiwa ni awamu ya pili kwa mwaka huu huku akisema itasaidia kwa kiasi kikubwa jamii.

Mhandisi Mariam Hindumi, ambaye alinunua vitabu hivyo kwa zaidi ya dola 5000, alisema uamuzi wa kufanya hivyo ni kwasababu ya maarifa yaliyosheheni katika vitabu hivyo ambayo amekuwa akiyasikia kutoka kwa Profesa GeorDavie.

Alieleza kuwa amekuwa akijifunza mengi kwa kiongozi huyo, ambaye amekuwa baraka kwa wengi ikiwemo yeye kwa kuponywa na kuinuliwa kiuchumi.

Mchungaji Boris wa Croatia, alisema wamefurahi kuudhuria katika tukio hilo la kihistoria la uzinduzi wa vitabu ambavyo vimesheheni maarifa kutoka kwa kiongozi huyo mashuhuri duniani.

Katika hatua nyingine, Mwekezaji wa Madini, Messi Chengula alimpongeza kiongozi huyo kwa udhubutu wake mkubwa wa kuandika vitabu vyenye maarifa makubwa katika masuala ya kifedha na ufalme wa Mungu kwani vitasaidia kwa kiasi kikubwa jamii na viongozi wa dini.

Uzinduzi wa vitabu hivyo viwili unafikisha jumla ya idadi ya vitabu vinne vya Nabii Mkuu Profesa GeorDavie, alivyozindua mwaka huu, kwani Januari mwaka huu alizindua vingine viwili cha Afrika Moja Bara na Nuru na Diplomasia ya Amani.

Previous Post

KUVUMILIANA MUHIMU

Next Post

TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Next Post
TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

8 months ago
KARDINALI PENGO AACHA SIMANZI

KARDINALI PENGO AACHA SIMANZI

2 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?