• ePaper
Thursday, May 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kupatikana kwa sehemu ya kichwa cha marehemu James Temba, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Institute of Finance Management (IFM), ambacho kilikuwa kikitafutwa katika uchunguzi wa tukio la mauaji lililotokea jijini humo mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema mafanikio hayo yametokana na uchunguzi wa kina uliofanywa kwa ushirikiano wa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi pamoja na vyombo vingine vya dola.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, marehemu Temba aliuawa katika mazingira ya kutatanisha, ambapo mwili wake ulipatikana ukielea kwenye maji ya Mto Msimbazi katika eneo la Kipawa, wilayani Ilala, ukiwa hauna kichwa.

Amesema baada ya taarifa ya awali iliyotolewa Mei 3 mwaka huu, uchunguzi uliendelea kwa umakini mkubwa na kufanikisha kubaini eneo la Kitunda Kibeberu, ambako sehemu ya kichwa hicho ilikutwa kikiwa kimefukiwa ardhini.

Kamanda Muliro amesema jumla ya watuhumiwa watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mtuhumiwa mmoja mpya aliyetajwa kwa jina la Said Ally (34), ambaye anadaiwa kujihusisha na shughuli za uganga wa kienyeji.

Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulisaidia kupatikana kwa sehemu hiyo ya mwili baada ya kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uchunguzi, huku taratibu za kisheria zikiendelea ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa dhidi ya wote wanaohusika.

Aidha, alisema kutokana na mazingira ya tukio hilo, polisi inaendelea kuchunguza uwezekano wa kuwepo kwa viashiria vya imani za kishirikina, akibainisha kuwa aina ya ukatili uliofanyika inaibua maswali mazito yanayohitaji uchunguzi wa kina wa kitaalamu.

“Baadhi ya mambo hayawezi kuwekwa wazi kwa sasa kwa kuwa yako kwenye hatua za kisheria na uchunguzi, lakini tunawahakikishia wananchi kuwa kila hatua inafanyika kwa umakini ili haki itendeke,” alisema Kamanda Muliro.

Jeshi la Polisi pia limewashukuru wananchi pamoja na mamlaka mbalimbali za uchunguzi wa kisayansi kwa ushirikiano walioutoa, ambao umewezesha kufikiwa kwa hatua hiyo muhimu katika upelelezi wa shauri hilo.

Aidha, wananchi wametakiwa kuendelea kuwa watulivu, kuepuka kusambaza taarifa zisizo sahihi kwenye mitandao ya kijamii, na kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola, huku jeshi hilo likisisitiza kuwa litaendelea kufuatilia kwa karibu kesi hiyo hadi wahusika wote wafikishwe mahakamani.

Previous Post

BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AHADI 5 ZA MGOMBEA URAIS WA CCM, IGUNGA

AHADI 5 ZA MGOMBEA URAIS WA CCM, IGUNGA

8 months ago
MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

3 months ago

Popular News

  • POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI

    POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?