• ePaper
Friday, May 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YAGEUZA KIBAO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 15, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA YAGEUZA KIBAO
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetangaza kujipanga kushirikiana na benchi la ufundi  kuhakikisha timu inashinda michezo saba iliyobaki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli hiyo imetolewa ikiwa ni siku moja baada ya kukishuhudia kikosi chao kikifungwa mabao 3-2 na Dodoma Jiji,  katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Airtel mkoani Singida.

Yanga imebakiza mechi saba kabla ya kumaliza msimu huu, katika msimamo   ipo kileleni kwa pointi 54 baada ya kushuka dimbani mara 23.

Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe alisema kila anguko lina funzo ndani yake, hivyo benchi la ufundi lina nafasi ya kujipanga na kuiongoza timu kupata ushindi katika mechi zilizobaki.

“Haikuwa siku nzuri, lakini imekuwa  siku nzuri ya uongozi na benchi la ufundi kukaa chini na kufanya tathimini ya mechi saba zilizobaki, tuna kila sababu ya kujipanga na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuiwezesha timu kutetea ubingwa wetu.” 

Aliongeza “Tupo katika hatua ya mwisho ya kumalizia ligi, hivyo lazima tujipange  kuhakikisha tunafikia malengo ya kutetea ubingwa,” alisema.

Alifafanua kuwa hakuna timu ambayo haijawahi kufungwa katika ligi, timu ilifanya makosa na kupoteza mchezo hivyo huu ni wakati wa kujipanga tena. 

KUHUSU  DJIGUI  DIARRA

Akizungumzia majeruhi ya kipa namba moja Djigui Diarra, ofisa huyo alisema wanasubiri ripoti ya madaktari ili kujua   aliumia  kiasi gani katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

“Daktari bado hajatoa taarifa ya jeraha la kipa wetu,  ripoti ikiwa tayari tutawajulisha hali yake,” alisema.

KOCHA DODOMA ATOBOA SIRI

Kocha wa Dodoma Jiji, Aman Josiah alisema siri ya wachezaji wake kupata ushindi dhidi ya Yanga ni kufuata maelekezo ambayo  aliwapa baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

“Vijana walipokea maelekezo vizuri,  kweli kipindi cha kwanza walicheza bila umakini, lakini walipambana na kufanya yale tuliyofanya, hii ni hatua nzuri kwetu,” alitamba.

Previous Post

NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

Next Post

NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

Next Post
NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM YAJIVUNIA KAMPENI ZA KISTAARABU – DK MWINYI

CCM YAJIVUNIA KAMPENI ZA KISTAARABU – DK MWINYI

7 months ago
BILIONI 400/- KUJENGA ARENA YA KISASA

BILIONI 400/- KUJENGA ARENA YA KISASA

1 month ago

Popular News

  • MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

    MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA YAGEUZA KIBAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?