• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

Imeelezwa kuwa Tanzania ni miongoni kwa nchi za awali katika bara la Afrika zilizopewa hadhi ya kimataifa ya Kijiopaki na UNESCO kutokana na mchango mkubwa kupitia Jiopaki ya Ngorongoro Lengai iliyopelekea Serikali kujenga makumbusho ya kisasa ya jiopaki (Urithi Geopark Museum) iliyojengwa na serikali wilaya ya Karatu Mkoani Arusha na kuzinduliwa mwaka 2025.

Akiwaslisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema makumbusho hayo ni sehemu ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai ambayo imejengwa kwa lengo la kutoa  elimu kuhusu sayansi ya miamba, volkano, na historia ya mazingira, na ni ya pekee katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Amesema kupitia makumbusho hayo Watalii na wadau wanaotembelea jengo hilo wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo muonekano wa dunia miaka mingi iliyopita na ilivyo sasa, maumbile asilia yanayopatikana katika ukanda wa bonde la ufa, kujionea mwamba wenye umri wa miaka milioni tatu iliyopita unaopatikana hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai, sambamba kujifunza tamaduni za makabila ya  Wahadzabe, Wairaq, Wadatoga na Wamasai pamoja, kupima uwezo wa kutambua sauti za wanyamapori, kushindana mbio kwa kutumia baiskeli na wanyamapori  ndani ya makumbusho na mengine mengi.

Makumbusho hii inayosimamia na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa sehemu ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) lenye hadhi tatu zinazotambulika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo hadhi hizo ni Eneo la Hifadhi ya Mazingira na Binadamu (Man and Biosphere Reserve 1981), Eneo la Urithi Mchanganyiko wa Asili na Kitamaduni (Mixed World Heritage 2010) na hadhi ya tatu Eneo la Hifadhi ya Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai  (Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark 2018) ambazo Tanzania ni nchi ya pili kupata hadhi hiyo ikitanguliwa na nchi ya Morocco

Tanzania Ina Jumla ya maeneo ya malikale 158 na maeneo 7 yametambuliwa kama urithi wa dunia

Previous Post

SERIKALI YAIPONGEZA PUMA ENERGY KWA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI

Next Post

DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

Next Post
DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

2 months ago
4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

4 weeks ago

Popular News

  • MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?