• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, leo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote, Ikulu Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijielekeza katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na makampuni ya Dangote katika maeneo ya nishati, viwanda, bandari, gesi, mbolea na miundombinu.

Aidha, Alhaji Dangote ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, pamoja na kutatua changamoto za wawekezaji nchini.

Amesema hatua za Serikali katika kutatua changamoto zilizokuwa zikikabili shughuli za Kiwanda cha Saruji cha Dangote, mkoani Mtwara, zimeongeza tija na ufanisi wa undeshaji, na imani ya kampuni hiyo kwa Tanzania kama eneo muhimu na la kimkakati la uwekezaji barani Afrika.

“Nataka nikushukuru kwa dhati kwa kushughulikia changamoto nyingi za uwekezaji wetu wa Kiwanda cha Saruji Mtwara.

Ulipoingia madarakani tulikuwa na changamoto nyingi, lakini kama ulivyoahidi, kila changamoto imeshughulikiwa ipasavyo,” amesema Alhaji Dangote.

Katika hatua nyingine, Dangote Group tayari imeleta chini malori 400 yanayotumia gesi asilia kwa ajili ya kusafirisha na kusambaza saruji katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kubadilisha malori 700 ya kampuni hiyo kwenda katika matumizi ya nishati hiyo mbadala ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.

Vilevile, Alhaji Dangote amesema kiwanda hicho kinaendelea kufanya vizuri na kinatarajia kuzalisha takribani tani milioni 2.8 kwa mwaka huu, kati ya lengo lake la kuzalisha takribani tani milioni 3.2.

“Tunafanya vizuri. Lazima nikushukuru Mheshimiwa Rais kwa uongozi wako; kwa sababu bila uongozi wako, soko lisingekuwa bora na lenye tija ya kutuwezesha kufanya biashara kwa ukubwa huu,” ameeleza Alhaji Dangote.

Mazungumzo yao pia yameangazia uwezekano wa Dangote Group kuingia ubia na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza mradi wa kusafisha mafuta ghafi unaokadiriwa kugharimu takribani Dola za Marekani bilioni 17, utakaonufaisha nchi za Afrika Mashariki na Ethiopia.

Alhaji Dangote amesema mradi huo unaweza kutoa fursa kwa nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki kushiriki kupitia umiliki wa hisa, kama sehemu ya kujenga uwezo wa bara la Afrika katika kujitosheleza kwa uzalishaji wa mafuta na bidhaa za mafuta na hivyo kupunguza utegemezi kutoka nje na kujilinda dhidi ya athari za misukosuko ya bei na upatikanaji wa bidhaa hizo.

Kwa upande wake, Rais Dk. Samia amemhakikishia ushirikiano na amemuomba Alhaji Dangote kundelea kuangalia fursa zaidi za biashara na uwekezaji nchini zenye tija na manufaa kwa mwekezaji, Serikali, na Taifa kwa ujumla.

Halikadhalika, Rais Dkt. Samia ameikaribisha Dangote Group kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea nchini akibainisha kuwa mahitaji ya bidhaa hiyo ni makubwa kuliko uwezo wa sasa wa uzalishaji wa ndani.

Previous Post

TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

Next Post

DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

Next Post
DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AJIRA 45,000 ZANUKIA

AJIRA 45,000 ZANUKIA

1 month ago
ATCL YARUDISHA WATANZANIA 236

ATCL YARUDISHA WATANZANIA 236

2 months ago

Popular News

  • MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?