• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA FEDHA ZA MIRADI RUKWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA FEDHA ZA MIRADI RUKWA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU, Dk. Mwigulu Nchemba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Rukwa kufuatia taarifa za kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

Ametoa agizo hilo leo Jumapili (Machi 8, 2026) akizungumza na mamia ya wananchi wa Laela mkoani Rukwa baada ya kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo.

Dk. Mwigulu amesema Serikali haitavumilia kuona miradi ya maendeleo ikicheleweshwa wakati fedha zake tayari zimetolewa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

 “Kamanda wa TAKUKURU nifanyie uchunguzi wa kina, senti mpaka senti, yeyote aliyehusika kwenye hii fedha hapa nipe taarifa hiyo ili niweze kufanya maamuzi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameonesha kutoridhishwa na kuchelewa kwa utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari, madarasa pamoja na miundombinu mingine ya elimu katika eneo hilo.

Amesema miradi hiyo imepokea fedha kutoka Serikali lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua, jambo ambalo halikubaliki kwani wananchi wanahitaji kuona matokeo ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo yao.

Aidha, Dk. Mwigulu amesisitiza kuwa fedha za miradi ya maendeleo hazipaswi kufanywa siri na kwamba taarifa za fedha hizo zinapaswa kuwafikia viongozi mbalimbali wa Serikali ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi hiyo.

“Msifanye fedha za miradi ya maendeleo kuwa siri. Fedha zikishafika nakala iende kwa Mkuu wa Mkoa, na zikishatumwa kwenye halmashauri nakala apewe Mkuu wa Wilaya na Mbunge, ili kuwe na ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa miradi hiyo,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji watakaobainika kuchepusha au kutumia vibaya fedha za miradi ya maendeleo kwa kuwa fedha hizo ni mali ya umma na zinapaswa kutumika kwa manufaa ya wananchi.

Previous Post

SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

Next Post

CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA – KIHONGOSI

Next Post
CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA – KIHONGOSI

CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA - KIHONGOSI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAREKANI YAKOSHWA KASI MAENDELEO Z’BAR

MAREKANI YAKOSHWA KASI MAENDELEO Z’BAR

3 weeks ago
DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

2 weeks ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?