• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA – KIHONGOSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA – KIHONGOSI
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesema CCM ndiyo baba wa demokrasia nchini kwani ndiyo chanzo cha kuzaliwa kwa vyama vingine vya siasa na utawala wa vyama vingi.

Kihongosi amesema hayo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Lagangabilili wilayani Itilima mkoani Simiyu.

Amesema kabla ya kuzaliwa kwa vyama vingine vya siasa, akisema ilianza Tanganyika African National Union (TANU) 1954 na baada ya muungano Februari 5,1977 ikaundwa CCM ambacho ndicho kilizaa siasa ya vyama vingi 1992 lakini bado kimeendeleo kuwa kinara na chama namba moja nchini.

Amebainisha kuwa muasisi wa vyama vingi ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye hata baada ya kura za ndio kwa siasa za vyama vingi kuwa chache bado alitaka kuwe na mfumo huo, hali inayothibitisha ukomavu wa demokrasia wa chama hicho.

Amesisitiza vyama vingine vidogo vimekuwa vikiendeshwa kama saccos hali inayotofautisha CCM na vyama vingine kwani ni chama kikubwa na chenye uzoefu wa miaka mingi.

Amesema uongozi wa nchi unahitaji watu wenye uzoefu, maarifa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa na kusimamia masuala ya maendeleo kwa manufaa ya taifa. Alifananisha uongozi wa nchi na dereva wa gari kubwa, akieleza kuwa kama ilivyo kwa madereva wa malori au mabasi makubwa wanaohitaji uzoefu mkubwa, ndivyo ilivyo pia kwa uongozi wa taifa.

“Hawa waliokwisha kuendesha magari makubwa kwa miaka mingi wana uzoefu. Ukimpa mtu ambaye hajazoea kuendesha gari kubwa anaweza kushindwa kulimudu,” amesema Kihongosi.

Amesema wananchi ni mashahidi kuwa CCM imelitoa taifa hili mbali na ndiyo maana wanapata sababu ya kushinda chaguzi nyingi kwani wamekuwa wakitekeleza yake ambayo wamekuwa wakiyaahidi kupitia ilani ya uchaguzi.

Previous Post

DK. MWIGULU AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA FEDHA ZA MIRADI RUKWA

Next Post

MAGEUZI MAKUBWA HOSPITALI YA OCEAN ROAD

Next Post
MAGEUZI MAKUBWA HOSPITALI YA OCEAN ROAD

MAGEUZI MAKUBWA HOSPITALI YA OCEAN ROAD

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

5 months ago
BONDIA DULLAH MBABE AWAITA MASHABIKI

BONDIA DULLAH MBABE AWAITA MASHABIKI

4 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?