• ePaper
Wednesday, September 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, leo tarehe 16 Mei 2026 amemwakilisha Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Botswana, Hayati Festus Gontebanye Mogae, yaliyofanyika jijini Gaborone.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais Dk. Samia , Dk. Kikwete amesema Tanzania inaungana na Serikali pamoja na wananchi wa Botswana katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kufuatia kifo cha kiongozi huyo mashuhuri wa Bara la Afrika.

Katika hotuba yake, Dk. Kikwete amesema kuwa wakati wa uongozi wa Hayati Mogae, ushirikiano na uhusiano wa kindugu kati ya Tanzania na Botswana uliendelea kuimarika kwa kiwango kikubwa. Akizungumzia mapenzi ya Hayati Mogae kwa Tanzania, Dkt. Kikwete amesema:

“Hayati Rais Mogae alikuwa rafiki wa kweli wa Tanzania na aliipenda nchi yetu kwa dhati.”

Dk. Kikwete pia alieleza kuwa Hayati Rais Mogae alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umoja, mshikamano na amani barani Afrika, sambamba na kushiriki kikamilifu katika juhudi mbalimbali za usuluhishi wa migogoro katika mataifa tofauti ya Afrika.

Akizungumzia uhusiano wake binafsi na Hayati Mogae, Dkt. Kikwete amesema:

“Napenda pia kueleza kuwa binafsi nilipata heshima ya kufanya kazi na Rais Mogae kwa mara ya kwanza alipokuwa Makamu wa Rais, wakati mimi nikihudumu kama Waziri katika Serikali za Rais Ali Hassan Mwinyi na Rais Benjamin Mkapa. Nilianza kama Naibu Waziri wa Nishati na Madini, baadaye nikawa Waziri wa Maji, Nishati na Madini, kisha Waziri wa Fedha, na tulifanya kazi vizuri sana ndani ya SADC. Baadaye, alipokuwa Rais wa taifa hili kubwa, mimi nilikuwa nikihudumu kama Rais wa nchi yangu pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Rais Mogae alikuwa mtu mzuri kufanya naye kazi. Alikuwa mwenye misimamo, mwadilifu, na siku zote alikuwa akisema kile alichokiamini, lakini kwa upole na heshima.” Mazishi hayo ya Kitaifa yalihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wastaafu, pamoja na viongozi

Previous Post

DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

Next Post

DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

Next Post
DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIKAKATI KABAMBE UJENZI WA VIWANDA

MIKAKATI KABAMBE UJENZI WA VIWANDA

4 months ago
DK. SAMIA AHIMIZA UPIGAJI KURA OKTOBA 29

DK. SAMIA AHIMIZA UPIGAJI KURA OKTOBA 29

11 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?