• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 17, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba, amewahimiza wananchi kuendelea kuiombea Tanzania ili amani, umoja na mshikamano wa kitaifa viendelee kuimarika sambamba na nchi kuendelea kupiga hatua za maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Amesema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2026 aliposhiriki ibada katika (KKKT) Usharika wa Kondoa Mjini, Jimbo la Kondoa, Dayosisi ya Dodoma.

Ibada hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, pamoja na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kondoa Mjini na Mkuu wa Jimbo la Kondoa KKKT, .

Waziri Mkuu amesema anaendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini akitambua mchango wake katika kujenga jamii yenye maadili, umoja na maendeleo.

“Ujumbe wake kwa wananchi wa Kondoa ni kwamba tuendelee kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa ya amani na kuendelea kupiga hatua za maendeleo,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ikiwemo ujenzi wa daraja la kuingia Kondoa Mjini pamoja na daraja la barabara ya kuelekea Hanang.

“Tumebeba jambo la daraja la kuingia hapa Kondoa Mjini, hilo tutaanza nalo. Lakini la pili ni daraja la kuelekea Hanang ambalo na lenyewe kero yake ni kubwa sana,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea na maandalizi ya utekelezaji wa mfumo wa elimu ya lazima wa miaka 10 unaotarajiwa kuanza mwaka 2028.

“Hatutakuwa na jambo linaloitwa mtoto amemaliza darasa la saba. Tunaenda kuondoa mfumo wa kuishia darasa la saba ili elimu ya lazima iwe miaka 10,” amesema.

Amesema utekelezaji wa mfumo huo unahitaji ushiriki na hamasa kutoka kwa Watanzania wote kutokana na umuhimu wa mabadiliko hayo katika sekta ya elimu nchini.

Kwa upande wake, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu , kwa ushirikiano na sisi watu wa imani na viongozi wa dini,” amesema.

Aidha, amesema kanisa linaendelea kumuombea Waziri Mkuu pamoja na viongozi wa Serikali ili waendelee kulitumikia taifa kwa hekima na uadilifu.

Previous Post

DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

Next Post

WASIRA: WALIOFANYA VURUGU WAPATIKANE

Next Post
WASIRA: WALIOFANYA VURUGU WAPATIKANE

WASIRA: WALIOFANYA VURUGU WAPATIKANE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KASI YA DK. MWIGULU YAWAIBUA WASOMI

KASI YA DK. MWIGULU YAWAIBUA WASOMI

6 months ago
DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

2 months ago

Popular News

  • MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?