• ePaper
Monday, May 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 25, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Shirikisho la Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amewataka wanahabari kuwahamasisha waajiri nchini kuhusu umuhimu wa kuripoti kwa wakati matukio ya ajali, ugonjwa ama vifo vinavyotokana na kazi, katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kurahisisha utolewaji wa fidia kwa wakati.

Nyamhokya ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo ,akifungua mafunzo kuhusu Fidia kwa Wafanyakazi kwa Wanachama wa Chama cha Waandishi wanaofanya kazi katika vyombo vya Habari (JOWUTA).

Amesema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kushughulikia masuala ya fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Vilevile, amesema WCF inatoa mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za matibabu, fidia ya ulemavu wa muda na wakudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki, huduma za utengemao, na msaada wa mazishi.

” Mafao haya yanatolewa kwa wafanyakazi au wategemezi wa wafanyakazi watakaopata ajali, ugonjwa au kifo kutokana na kazi zao. Ndio maana ninawaambia kuwa WCF ni taasisi yetu na hivyo tuna wajibu kuhakikisha tunaulinda kwa nguvu zote kuhakikisha unakuwa himilivu.”amesema Nyamhokya .

Aidha,Nyamhokya amewataka waandishi wa habari kuwaelimisha wafanyakazi juu ya umuhimu wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi kwa ajili ya kuunganisha nguvu katika kutetea maslahi yao.

“Slogan yetu ya ‘SOLIDARITY FOREVER’ inamaanisha umuhimu wa umoja na mshikamano katika kutetea maslahi ya wafanyakazi. Wafanyakazi ni jeshi kubwa lakini bila kuwa wamoja hatuwezi kufanikiwa katika mapambano ya kudai haki zetu” amesema.

Previous Post

MAKONDA ASISITIZA KULINDWA KWA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA CHINA

Next Post

MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

Next Post
MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

“Wasichana milioni mbili wanufaika na elimu ya stadi za maisha

9 months ago
NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

1 month ago

Popular News

  • MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAKONDA ASISITIZA KULINDWA KWA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA CHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?