• ePaper
Wednesday, June 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 10, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amefungua milango ya uwekezaji kwa Singapore, huku akitaja maeneo matano ya kimkakati yaliyoandaliwa kwa fursa ya uwekezaji nchini.

Baadhi ya maeneo hayo ni bandari, kuongeza thamani katika mnyororo wa kilimo na madini, nishati mbadala na utalii.

Pia, Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, amemshukuru Rais Dk. Samia na Watanzania kwa ukaribisho mzuri uliojaa ukarimu huku akimhakikishia utayari wao wa kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kupitia maeneo mapya ya uwekezaji waliyoingia makubaliano.

Rais Dk. Samia alisema hayo jijini Dar es Salaam, alipofungua Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Singapore katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), ulioudhuriwa na wawekezaji na wafanyabishara ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais wa Singapore nchini.

“Eneo la kwanza ni bandari kutokana na Tanzania ni lango la kimkakati kwa ajili ya nchi sita ambazo hazina bandari zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hivyo kuna fursa kubwa ya soko la usafirishaji.   

“Pia, bandari za Tanzania zinahudumia nchi za Malawi, Uganda, Rwanda na Zambia.

“Bandari ya Dar es Saalam inabeba na kushughulikia sehemu kubwa ya biashara hiyo, ushirikiano wetu utaongeza ufanisi na kuunganisha nchi za Bara la Asia,”alisema.

Alisema kupitia upanuzi wa Bandari ya Dar es Saalam, Bagamoyo na Mangapwani iliyopo Zanzibar, Serikali ya Tanzania, inaikaribisha Singapore kushirikiana katika eneo la usafirishaji, huduma za meli na maendeleo ya viwanda yanayounganishwa na bandari.

Rais Samia, alisema eneo la pili ni kuongeza thamani katika mnyororo wa kilimo na madini, kumekuwepo na fursa kubwa ya usambazaji bidhaa za kilimo katika masoko ya Singapore.

“Chini ya mkakati wao wa chakula unaotafuta ubadilishwaji wa uingizaji wa vyakula na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kufikia usalama endelevu wa chakula

“Katika hili, tunaweza kujifunza kutoka nchi zingine za Bara la Asia kama Vetinam na Thailand ambazo ziliweka mkataba rasmi wa maelewano juu ya biashara ya mchele kati ya Singapore unaohakikisha usalama na usambazaji thabiti wa mchele.

“Kwa hiyo, tunaweza kuchagua bidhaa gani ya kilimo ambayo tunaweza kusambaza Singapore na kuwa na makubaliano kwa upande wetu. “Makubaliano hayo, yanaweza kujumuisha bidhaa kama kahawa, chai, korosho na viungo,”alisema

Alisema Tanzania ni wazalishaji wakubwa wa madini aina ya Tanzanite na asilimia kubwa ya madini hayo, dhahabu na vito vya thamani, vinapitishwa katika mipaka bila ya kuchakatwa.

“Kwa hiyo, tukiweza kulitatua jambo hili, tunaweza tukahama kutoka usafirishaji wa vito hivyo vya thamani ambavyo vinaingia katika malighafi hadi kufikia bidhaa zilizochakatwa ambazo zitafaa masoko ya Bara la Asia,”alisema

Eneo la tatu ni nishati mbadala ambapo Tanzania ina uwezo mkubwa katika nishati jua, upepo, gesi na nishati ardhi.

Rais Samia jingine ni utalii na uchumi wa buluu, ambapo Tanzania imepokea wageni wa kimataifa takribani zaidi ya milioni mbili kwa kipindi cha mwaka jana huku Zanzibar ikipokea zaidi ya wageni 900,000.

“Sekta yetu ya anga inakuwa ikibeba abiria zaidi ya milioni 6.8 kati ya kipindi cha Julai mwaka 2025 na Machi 2026, ni ongezeko la zaidi ya asilimia 12, uwanja wa ndege wa Changi wa Singapore unahudumia abiria milioni 70 na zaidi ya tani milioni mbili za mizigo mwaka 2025.

“Hata hivyo, Asia na Singapore zinabaki kuwa soko la utalii nchini Tanzania, kuna fursa kubwa kwenye eneo hilo, tufanye kazi kwa pamoja kwa ajili ya kukuza utalii,”alisema.

Eneo lingine ni huduma za kifedha na utatuzi wa migogoro ya kibiashara ambapo Singapore ni miongoni mwa nchi zenye vituo vikubwa vya kifedha na uwekezaji mkubwa barani Asia.

“Ikiwa ina uwezo mkubwa kwenye masoko ya mitaji ya fedha za miradi na fedha za uwekezaji na msimamo wa utatuzi wa migogoro upo wazi, mwaka 2025 kituo cha kimataifa cha usuluhishi cha Singapore kilishughulikia kesi ya 886 kutoka katika mamlaka 80, asilimia 89 kati ya hizo ni za kimataifa

“Tunapoendelea kukusanya mitaji kwa ajili ya bandari zetu, reli, nishati na kanda maalumu za kibiashara, tunakaribisha ushirikiano katika kuendeleza kituo cha fedha cha kimataifa na kuanzisha kinachotambulika cha usuluhuhishi chenye sifa za kimataifa ili kukuza imani ya wawekezaji na msimamo wa Tanzania kama eneo la kipaumbele la uwekezaji Afrika,”alisema.

Alisema utalaamu wa Singapore na uwezo wa Tanzania, unalingana vyema na kusababisha kuunda ushirikiano mkubwa, wenye tija katika kuchochea maendeleo ya mataifa hayo na wananchi wake.

Alissisitiza kuweka katika vitendo mikakati hiyo katika uwiano unaopimika katika kutekeleza malengo hayo, kuharkisha ushirikiano wa kuongeza thamani katika mnyororo wa usafirishaji dhahabu, vito na usindikaji wa bidhaa, utengenezaji wa bidhaa kama dawa na mitambo ya kilimo, kujenga ushirikiano wa kimkakati wa Bandari kupitia ushirikiano wan chi hizo wenye lengo la kuimarisha biashara inayofanyika kwa njia ya bahari.

Pia, kuendeleza ukanda wa utalii na singapole kwa muunganiko bora wa usafirishaji wa anga, majini kuunganisha na jukwaa la kidijitali, kufungua mkondo wa kifedha  na utatuzi wa migogoro.

Alisema mafanikio ya mkutano huo, yatapimwa kwa miradi na utekelezaji utakaozaliwa.

Previous Post

WASOMI WADOKEZA MANUFAA YA UWEKEZAJI MAENEO MANNE

Next Post

TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

Next Post
TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA KUIUA TRA UTD

SIMBA KUIUA TRA UTD

3 months ago
MTIHANI MZITO KWA MOALIN

MTIHANI MZITO KWA MOALIN

1 month ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA VITA KALI

    YANGA, SIMBA VITA KALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASOMI WADOKEZA MANUFAA YA UWEKEZAJI MAENEO MANNE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?