• ePaper
Thursday, June 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RUNGU ZITO KUWASHUKIA WAWEKEZAJI ‘JANJAJANJA’

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 25, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RUNGU ZITO KUWASHUKIA WAWEKEZAJI ‘JANJAJANJA’
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW,Dodoma

SERIKALI imetangaza vita dhidi ya wawekezaji wanaotumia majina ya Watanzania kujinufaisha kupitia zabuni zilizotengwa kwa wazawa.

Pia, imesema itawachukulia hatua dhidi ya wanaojihusisha na utengenezaji na uingizaji wa bidhaa bandia nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, alipomwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika uzinduzi wa Kituo cha Kisasa cha Huduma za Magari na Chuo cha Mafunzo ya Usafiri na Usalama Barabarani cha Superdoll.

Dk. Mwigulu, alikemea baadhi ya wawekezaji wanaotumia majina na vitambulisho vya Watanzania kupata zabuni zilizotengwa kwa wazawa na baadaye kuwaondoa katika umiliki wa kampuni hizo.

“Huu ni utapeli, ni uhujumu wa uchumi wetu. Tumewatengea Watanzania wanufaike, wapo wanaotaka hata nafasi hiyo ndogo wasiipate. Huu ni ubinafsi uliokithiri,” alisema.

Alisema serikali tayari imeanza kufuatilia kampuni zinazojihusisha na udanganyifu huo na kwamba, hatua kali ikiwemo kuzuia kufanya biashara nchini, zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kukiuka sheria.

Dk. Mwigulu, alisema marekebisho yaliyofanywa katika sheria mbalimbali, yameanza kuzaa matunda kwa kuwa, yamewapa nafasi wakandarasi na kampuni za ndani kushiriki katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

“Hatutaki kuona Watanzania wanakuwa watumwa katika nchi yao. Sheria tulizoweka lazima ziheshimiwe na kila mmoja,” alisema.

Aliwahakikishia wawekezaji kuwa, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na kwamba, milango ya wizara zote na Ofisi ya Waziri Mkuu, ipo wazi kupokea na kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji wenye nia njema

Waziri Mkuu alisema uwekezaji huo ni uthibitisho wa dhamira ya serikali ya kujenga uchumi unaoshirikisha sekta binafsi.

Alisema miradi ya kisasa inayojengwa Dodoma, imebadili taswira ya makao makuu ya nchi na kuonesha kuwa, maono ya Rais Dk. Samia kuhusu uwekezaji na ukuaji wa sekta binafsi, siyo maneno isipokuwa ni vitendo vinavyoonekana.

“Rais amenituma niwahakikishie kuwa serikali yake itaendelea kusimamia mikakati yote na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na sekta binafsi katika kukuza uchumi, uwekezaji na biashara,” alisema.

Dk. Mwigulu alisema katika kipindi cha takribani miaka mitano, serikali imefuta zaidi ya kodi na tozo 250 katika sekta mbalimbali kuweka mazingira rafiki kwa biashara na uwekezaji, hatua ambayo imechangia kuibuka kwa kampuni nyingi za ndani zenye ushindani wa kimataifa.

Alisema kituo hicho cha kisasa, kitaongeza ubora wa huduma za usafirishaji, mafunzo na biashara huku kikiiweka Dodoma katika nafasi ya kuwa kitovu cha huduma kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini.

Alisema uwekezaji huo, umefungua fursa za ajira kwa vijana ambapo baadhi yao, wamepata ajira baada ya kuhitimu mafunzo, huku mamia ya wananchi wakinufaika kupitia shughuli mbalimbali za mradi huo.

Waziri Mkuu aliipongeza Superdoll kwa kuonesha kuwa, Watanzania wana uwezo wa kuanzisha na kuendesha kampuni kubwa zinazoweza kushindana katika viwango vya kimataifa.

“Superdoll mmeonyesha kwa vitendo kwamba Watanzania wanaweza kuanzisha, kuendesha na kukuza taasisi za kiwango cha kimataifa na kushindana na kampuni yoyote duniani,” alisema.

Alisema serikali itaendelea kusimamia maono ya Rais Samia ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi na kunufaika na rasilimali zilizopo kupitia sekta binafsi yenye nguvu.

“Lazima Watanzania washike uchumi wa nchi yao, lazima wanufaike na rasilimali za nchi yao. Hatuna nia ya kubagua,Tanzania ndiyo kwetu,”alisema.

BIDHAA BANDIA

Dk. Mwigulu alisema bidhaa bandia ni adui wa maendeleo kwa kuwa zinahatarisha maisha ya wananchi, zinadhoofisha viwanda vya ndani na kusababisha hasara kubwa kwa uchumi wa taifa.

“Niwaahidi Superdoll, tutaendelea kupambana na watengeneza bidhaa feki na waingizaji wa bidhaa feki nchini. Msiwe na huruma hata kidogo kwa sababu wanaharibu uchumi wetu,” alisema.

Aliwataka mawaziri na taasisi zinazohusika kuhakikisha wahusika wa biashara ya bidhaa bandia wanachukuliwa hatua kali bila upendeleo, akisema vita dhidi ya bidhaa hizo ni vita ya kulinda maisha na uchumi wa Watanzania.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alisema uwekezaji huo, unaenda sambamba na jitihada za serikali za kuboresha sekta ya usafirishaji na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la kikanda, hasa kwa nchi za Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alisema hadi Machi, mwaka huu, zaidi ya tani milioni 10 za mizigo zilihudumiwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam kwenda katika nchi hizo, jambo linalodhihirisha umuhimu wa kuendelea kuboresha huduma za usafirishaji.

“Mizigo mingi inayohudumiwa Bandari ya Dar es Salaam huenda Zambia na DRC, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuruhusu matumizi ya matairi ya ‘super single’ ambayo yana matumizi madogo ya mafuta, uwezo mkubwa wa kubeba mizigo na kuongeza ushindani kwa wasafirishaji wetu,” alisema.

Previous Post

YANGA, SIMBA KAZI KAZI UBINGWA LIGI KUU

Next Post

SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

Next Post
SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

5 months ago
MPINZANI WA MWAKINYO HADHARANI

MPINZANI WA MWAKINYO HADHARANI

6 months ago

Popular News

  • SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

    SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RUNGU ZITO KUWASHUKIA WAWEKEZAJI ‘JANJAJANJA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI UBINGWA LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?