• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MICHANGO YA LISSU YAIBUA MAKUBWA CHADEMA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MICHANGO YA LISSU YAIBUA MAKUBWA CHADEMA
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Arusha

Na Mwandishi Wetu

MICHANGO ya ‘Vuka Mwaka na Tundu Lissu’ imeleta balaa kubwa ndani ya CHADEMA na familia ya Mwenyekiti wao, Tundu Lissu ambaye anashirikiriwa gerezani kwa kosa la Uhaini.

Hatua hiyo inatokana na michango iliyokusanywa na wanachama wa CHADEMA ambao miongoni mwao wapo wajumbe wa Kamati Kuu akiwemo kudaiwa kutafuna mamilioni ya fedha ya michango yaliyokuwa yanakusanywa.

Taarifa tulizozipata Uhuru zimedai kuwa wanachama wa CHADEMA wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa, Fredie Mbwambo, Brenda Rupia (Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano CHADEMA), Rose Mayemba (Mjumbe wa Kamati Kuu) wametajwa kuwa mstari wa mbele kutafuna fedha hizo.

Wengine waliotajwa katika kadhia hiyo ni pamoja na John Pambalu (Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni) ambaye jana alitoa kauli katika mtandao wake wa kijamii wa X (zamani Twitter) pamoja na mwanaharakati Maria Sarungi kuwa hawahusiki na kura michango hiyo.

ILIKUAJE MICHANGO KULIWA

Taarifa za kuaminika zilidai michango ya Mwenyekiti wa Chadema, Lissu iliyokusanywa zaidi ya shilingi million 41 ambapo sehemu ya fedha hizo kiasi cha shilingi million 18 zimeliwa na wanaharakati wa mitandaoni.

Michango hiyo iliyojulikana kwa jina la ‘VUKA MWAKA NA TUNDU LISSU’ ikikusanywa kupitia namba za simu 0770263180 – Tigo na 0797527876 – Voda zikiwa zimesajiliwa kwa majina ya Kaka yake Lissu Alute Mughwai.

Michango hiyo ilichangwa kwa wananchi ikiwa na lengo la kumsaidia Lissu ambaye yuko gerezani kuwa Watanzania bado wapo pamoja na yeye huku nyuma ya pazia wakiwa wanajinufaisha wenyewe.

Inadaiwa kuwa michango hiyo ilikua inaratibiwa na wanaharakati mitandaoni wakiongozwa na Maria, Twaha Mwaipaya, Rose, Pambalu, Hilda Newton, Freddie Justine Mbwambo kwa kushirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Golugwa.

Wanaharakati hao kwa kushirikiana na Naibu Katibu waliibua hoja kwamba Mzee Alute Mughai amezeeka hawezi kutoa taarifa ya michango mara kwa mara mitandaoni ambapo Golugwa na Fredie walienda nyumbani kwa Mzee Alute wakimshawishi asajili line mpya na kisha wapatiwa pamoja na password za namba hizo.

Line hizo za simu ambazo gazeti hili imezipata zilisajiliwa kwa jina la kaka yake Lissu ambaye alikubali Maskini mzee Alute akawaamini wakora akijua wana nia njema ya kumsaidia mdogo wake,akaenda kusajili line akawakabidhi Amani Golugwa pamoja na Fredie kwa ajili ya uratibu wa michango.

“Kweli tukaona mitandaoni wanaharakati wakihamasisha kumchangia Lissu salamu za Christmas huku wananchi tukihamasika kweli kutoa michango kwa nguvu na upendo wote tukiamini kwa kuwekwa namba za Mzee Alute,Kaka yake Lissu fedha zetu zitakua salama.” alisema mmoja wa wananchi Yericko Nyerere.

Aliendelea “Tulichanga fedha, wanaharakati wakasema zimekusanywa Million 23,na kumkabidhi Mzee Alute, na sisi wananchi tukashukuru kwa msaada wa wanaharakati hao. Kumbe ni wezi watupu”

Hata hivyo, taarifa ya gazeti hili zilieleza kuwa Mzee Alute alienda Kampuni ya Vodacom na Yas kwa ajili ya kuchukua statement za miamala kama tujuavyo ni mwanasheria na muhimu kutunza kumbukumbu na kuangalia uwajibikaji.

Alipochukua ‘statement’ zote mbili zilionyesha fedha zilizokusanywa ni shilingi million 41 na yeye alikabidhiwa shilingi milion 23 pekee ikiwa ni pungufu ya shilingi milioni 18 zilizoliwa na viongozi hao wa CHADEMA.

Baada ya tukio hilo, Mzee Alute aliripoti tukio hilo Kituo Kikuu cha Polisi Kati Arusha, akimshtaki Fredrick Justine Mbwambo na Amani Golugwa pamoja na wenzake kwa kufanya wizi wa kuaminika. Hii ilitokana na taarifa ya miamala ya kifedha (statement) ilionyesha fedha ziligawanya kwa watu mbalimbali

POLISI WAIBUKA WAANZA KUWADAKA WARATIBU

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumshikilia Fredrick kwa tuhuma za wizi wa fedha alizokuwa anachangisha kwa wananchi kumsaidia Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu.

Taarifa ya polisi ilisema Fredrick ambaye ni mkazi wa mkoa wa Arusha alikuwa anachangisha fedha hizo kupitia kampeni iliyopewa jina la “Funga mwaka na Tundu Lissu”.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha tunamshikilia mtu mmoja anayehafamika kwa jina la Fredrick Mbwambo kwa tuhumuma za wizi wa fedha alizokuwa anachangisha kupitia kampeni iliyopewa jina la “Funga mwaka na Tundu Lissu” ilisema taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo.

Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na kesi iliyofunguliwa na kaka yake Lissu na Fredrick alikamatwa Januari 27 mwaka huu baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

“Ufuatiliaji wa awali umeonyesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishiwa kwenye namba mbili za simu moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ni kampuni ya simu ya nchi jirani.” alisema

Aidha alifafanua kuwa kutokana na malalamiko hayo jalada lilifunguliwa kwa utaratibu wa kisheria ambapo uchunguzi ulianza na kupelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Hivyo, jeshi la Polisi mkoani hapa limesema kuwa jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wengine waliotuhumiwa kuhusika katika wizi huo na vielelezo unaendelea na hatua nyingine za kisheria zitafuata.

Previous Post

HISTORIA ELIMU MSINGI YAANDIKWA

Next Post

PAPA LEO XIV APOKEA UJUMBE WA RAIS DK. SAMIA

Next Post
PAPA LEO XIV APOKEA UJUMBE WA RAIS DK. SAMIA

PAPA LEO XIV APOKEA UJUMBE WA RAIS DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AMANI NYENZO MUHIMU YA MAENDELEO AFRIKA

AMANI NYENZO MUHIMU YA MAENDELEO AFRIKA

1 week ago

GAMONDI AJA KIVINGINE KUIVAA MOROCCO AFCON

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?