• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

HISTORIA ELIMU MSINGI YAANDIKWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
HISTORIA ELIMU MSINGI YAANDIKWA
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameandika historia kubwa katika sekta ya elimu msingi kwa kuzindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) huku akieleza mpango umelenga kumjenga mtoto kielimu na kimaisha kuanzia elimu ya awali, darasa la kwanza na la pili.

Kuzinduliwa kwa mkakati huo ni sehemu ya utekelezaji ahadi ya Rais Dk. Samia aliyoitoa katika kampenzi za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29 mwaka jana kwamba ndani ya siku 100 atahakikisha ana anzisha mpango huo kuboresha kiwango cha kusoma, kuandika na kuhesabu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mpango huo, Rais Dk. Samia alisema serikali imeamua kushughulikia changamoto za elimu kuanzia mizizi yake, badala ya kusubiri matatizo yajitokeze katika ngazi za juu za elimu.

Alisema mpango huo unaonesha dhamira ya dhati ya serikali kuboresha matokeo ya ujifunzaji watoto, hivyo stadi za KKK ndizo msingi wa elimu na maendeleo ya Taifa.

“Mpango huo una kauli mbiu ya  KKK ambayo ni Msingi wa Elimu kwa Maendeleo Endelevu, umebuniwa kuwajengea watoto uwezo wa kukabiliana na masomo yao katika mazingira yanayobadilika duniani, huku ukichangia katika ujenzi wa uchumi wa Taifa,” alisisitiza.

KUHUSU MPANGO HUO

Rais Dk. Samia alieleza kwamba mpango huo ni sehemu ya utekelezaji Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayosisitiza maendeleo ya rasilimali watu na taifa linaloongozwa kwa maarifa na uadilifu, hivyo mpango huo unatekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo inayolenga kumwezesha mwananchi kuchangia maendeleo ya Taifa.

Alisema serikali inaweza kujenga miundombinu bora ya elimu na kukuza teknolojia, lakini bila kuimarisha msingi wa elimu ya awali, taifa litakuwa linajenga msingi dhaifu utakaoathiri matokeo ya wanafunzi wanapohitimu elimu ya msingi.

Rais Dk. Samia alisema serikali imefanya maboresho ya mitaala ya elimu ya lazima kuwa ya miaka 10 ili kuhakikisha watoto wanapata maandalizi thabiti kabla ya kuendelea katika ngazi nyingine za elimu.

Alieleza kuwa mkakati wa KKK ni sehemu ya utekelezaji maazimio ya kikanda na kimataifa ikiwemo Azimio la Umoja wa Afrika kuhusu elimu ya Afrika katika karne ya 21 na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, hususan lengo namba nne.

Akizungumzia teknolojia, Rais Dk. Samia alisema watoto wa kizazi cha sasa wanapaswa kuendana na mabadiliko hayo, hivyo amevutiwa na maonyesho ya zana za kufundishia zilizobuniwa ndani ya nchi kwa kutumia vifaa rahisi vyenye ufanisi mkubwa.

“Maonyesho hayo yameonesha kuwa watoto wanaweza kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia vitendo, michezo na ushiriki wa moja kwa moja badala ya nadharia pekee,” alisisitiza.

Dk. Samia aliipongeza wizara kwa kuzingatia ujumuishi hususani kwa watoto wenye mahitaji maalum wakiwa wamezingatiwa katika mpango huo, hatua inayodhihirisha dhamira ya serikali kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma.

Alisisitiza kuwa katika dunia ya sasa, kuwekeza katika stadi za awali za elimu siyo hiari bali ni wajibu wa serikali, wazazi na jamii kwa ujumla.

JUHUDI ZA SERIKALI

Rais Dk. Samia alisema serikali imeongeza juhudi katika uandikishaji wanafunzi na ujenzi wa miundombinu ya elimu, ambapo idadi ya madarasa shule za msingi na sekondari imeongezeka kwa kiwango kikubwa kati ya mwaka 2021 na 2025.

“Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuboresha upatikanaji elimu kwa kuongeza kiwango cha uandikishaji na kuimarisha miundombinu katika shule za msingi na sekondari.

“Katika elimu msingi, madarasa yameongezeka kutoka 151, 315 mwaka 2020 / 2021 hadi madarasa  184, 550 mwaka 2020/2025  na upande wa elimu ya sekondari madarasa yameongezeka kutoka 64, 204 mwaka 2021 hadi 101,473 mwaka 2025. Takwimu hii inatuonesha tumetoka mbali,”alisema.

Katika kipindi hicho, alisema serikali imeongeza kasi ya ujenzi wa madarasa ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo kwa wastani wa miaka 60, Tanzania ilikuwa ikijenga madarasa 3,080 ya msingi kwa mwaka ikilinganishwa na wastani wa zaidi ya madarasa 8,000 kwa mwaka katika kipindi cha sasa.

Pia, alisema sekta binafsi nayo imekuwa ikifanya kazi kubwa katika utoaji elimu nchini kuanzia awali hadi ngazi ya juu, hivyo serikali inathamini nguvu au mchango wao.

“Katika suala la watumishi wa elimu, ahadi zangu za siku 100  tuliahidi tutaajiri walimu 7,000 ninayo furaha kusema tumeshaajiri na kuwapangia vituo vya kazi walimu 644 huku walimu 956 wapo katika mchakato kujaza nafasi zilizobaki ili tutakapofika Februari tatu, tuwe tumemaliza nafasi zote 7,000,” alisema.

Rais Dk. Samia alisisitiza kuwa ujenzi wa miundombinu na ajira za walimu havitoshi bila kusimamia ubora wa mafunzo yanayotolewa, hususan katika hatua za mwanzo za ukuaji wa mtoto.

“Serikali imejipanga kuhakikisha waliju wanakuwa sehemu ya suluhusho na wadau muhimu katika utekelezaji wa makakatu huu kwa kuwapatia nyenzo , mafunzo na mbinu za kisasa katika ufundishaji,”alisema.

MAAGIZO KWA WAKAGUZI, WIZARA NA WAZAZI

Rais Dk. Samia aliwataka wakaguzi wa elimu kuhakikisha mpango wa KKK unasimamiwa kikamilifu katika shule zote huku akisisitiza matokeo ya mpango huo lazima yaonekane moja kwa moja kwa mtoto darasani.

Pia, aliitaka Wizara ya Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kikamilifu.

Vilevile, aliwataka wazazi na jamii kushirikiana na serikali katika kufanikisha mpango huo kwa sababu elimu ya awali huanzia nyumbani kabla ya kuendelea shuleni.

WAZIRI MKENDA

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf  Mkenda, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa  kutimiza ahadi yake kwa Watanzania ya kuandaa na kuzindua mpango huo ndani ya siku 100 tangu kuunda serikali yake.

Alisema mpango huo umeandaliwa kwa kina ukiwa umezingatia maeneo makuu matano muhimu ambayo ni kuimarisha ufundishaji kwa kutoa mafunzo endelevu kwa walimu na kuboresha mbinu bora za ufundishaji.

“Mpango unalenga maendeleo endelevu ya walimu kwa kuwashirikisha kikamilifu maandalizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

“Eneo lingine muhimu ni upatikanaji nyenzo za kufundishia na kujifunzia zinazotokana na mazingira halisi ya Tanzania, ikiwemo matumizi ya vifaa rahisi kama vizibo vya chupa za soda,” alifafanua.

Alisema vifaa hivyo ni sehemu ya sayansi ya mpango huo, unaoeleza umuhimu kuwajengea watoto umahili wa stadi hizo ndani ya miaka minane ya awali ya makuzi yao.

Pia, alisema umeweka mkazo kwenye tathmini na upimaji wa mara kwa mara kuhakikisha maendeleo yanapimwa na kufuatiliwa ipasavyo.

Mkenda alitaja eneo lingine ni ushirikishwaji wazazi, walezi na jamii kwa ujumla katika kukuza elimu ya watoto.

KATIBU MTENDAJI NECTA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Profesa Said Mohamed, alisema baraza hilo limekuwa likiendesha upimaji stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa njia ya sampuli tangu mwaka 2015 kwa lengo la kufuatilia kiwango cha umahiri wa wanafunzi katika hatua za awali za elimu.

Alisema upimaji huo ulihusisha wanafunzi wa darasa la pili kutoka shule chache zilizochaguliwa katika kila halmashauri nchini na ukusanyaji wa taarifa muhimu kutoka kwa walimu wakuu kuhusu mazingira ya ujifunzaji, ufundishaji, upatikanaji vitabu.

Alieleza kuwa matokeo ya upimaji huo kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2023 yalibainisha kuwa wanafunzi wengi walikuwa na umahiri mdogo katika stadi za KKK, huku umahiri mzuri zaidi ukionekana katika stadi za kusoma na kuandika.

Hata hivyo, alifafanua kuwa wanafunzi wengi waliweza kusoma kwa ufasaha maneno rahisi yenye silabi moja au zenye konsonanti na irabu, lakini walipata changamoto kusoma maneno yenye silabi changamani, vinyongo na maneno yanayohitaji kasi na ufasaha zaidi.

Kwa upande wa stadi za kuhesabu, Profesa Mohamed alisema changamoto kubwa zilizobainika ni kushindwa kubaini namba zinazokosekana, kufanya hesabu za kujumlisha kwa kubeba, kutoa kwa kukopa pamoja na kutafsiri maneno yanayoelezea matendo ya kihisabati kama vile kupungua, kuongezeka na kubaki.

Alisema changamoto hizo ziliathiri uwezo wa wanafunzi kufumbua mafumbo ya kihisabati katika ngazi ya msingi.

Alieleza kuwa kufuatia changamoto hizo, NECTA kwa kushirikiana na wadau wa elimu ilichukua hatua za makusudi ikiwemo kutoa mafunzo ya upimaji wa KKK kwa walimu wa elimu ya awali, walimu wa darasa la kwanza na la pili, wakuu wa shule, maofisa elimu taaluma pamoja na wadhibiti ubora.

“Mafunzo hayo yalihusisha walimu zaidi ya 43,000 yalilenga kuimarisha ufundishaji na ufuatiliaji wa stadi za KKK mapema kabla ya mwanafunzi kufika ngazi za juu,” alisisitiza.

MKUU WA MKOA

Mkuu wa Mkoa Dar es  Salaam, Albert Chalamila, alisema jambo hilo lina tija kwani linakwenda kuthibitisha kuwa Dar es Salaam ni mdau mkubwa katika utekelezaji wa programu  hiyo.

Alisema mkoa huo una mchango mkubwa katika kuandikisha wanafunzi wa shule ya awali na darasa la kwanza, hatua inayodhihirisha dhamira ya serikali kuwekeza katika elimu ya msingi.

Alifafanua kuwa hadi sasa wanafunzi 32,000 wa shule ya awali tayari wameshasajiliwa sawa na asilimia 24 ya lengo lililowekwa.

Previous Post

NMB YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA, YAZINDUA MKAKATI WA MIAKA MITANO

Next Post

MICHANGO YA LISSU YAIBUA MAKUBWA CHADEMA

Next Post
MICHANGO YA LISSU YAIBUA MAKUBWA CHADEMA

MICHANGO YA LISSU YAIBUA MAKUBWA CHADEMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

FOUNTAIN GATE KUITIBULIA YANGA?

FOUNTAIN GATE KUITIBULIA YANGA?

4 months ago
TANZANIA YATIKISA KIMATAIFA

TANZANIA YATIKISA KIMATAIFA

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?