• ePaper
Saturday, June 27, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 27, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

LEO siku ya kilio au kicheko, kwa timu za Yanga na Simba zitakaposhuka  kucheza viwanja tofauti katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu hizo zitashuka dimbani katika michezo ya ligi hiyo kuwania ubingwa ambapo timu zote 15 zinazoshiriki michuano hiyo, zitacheza katika viwanja tofauti.

Yanga na Simba watakuwa nyumbani katika mechi zake za ligi, huku kila mmoja akimuombea mwenzake apote.

Hali hiyo, inakuja huku Yanga ikiwa inaongoza  ligi hiyo kwa ponti 69, wakati Simba yenyewe ina pointi 67 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu, ina alama 58.

Pamoja na vita ya Yanga na Simba, bado kuna timu zinaendelea kupambana kukwepa kushuka daraja huku KMC tayari imeshuka.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Yanga watashuka dimbani kupambana na TRA United katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa KMC.

Akizungumza jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moalin alisema kikosi chake kimejipanga kushinda katika mchezo huo.

 “Tunaingia katika mchezo huo kwa kuwaheshimu wapinzani wetu, tutapambana kupata ushindi na kuendelea kuongoza ligi,” alisema Moalin.

Nyota wa timu hiyo, Abuutwalib Mshery alisema mechi hiyo ni muhimu zaidi kwao ili kupata matokeo mazuri.

Kocha wa TRA United, Etienne Ndairagije alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanapata ushindi leo.

“Yanga siyo timu ya kuibeza, tunahitaji kupambana nao mwanzo mwisho ili kupata ushindi katika mchezo huo muhimu, tutapambana  kwa nguvu zote,” alisema Ndairagije.

Naye nyota wa TRA United, Shaban Chilunda alisema wamejipanga vizuri na wachezaji wote wana hamu ya kucheza mchezo huo.

Kwa upande wa Simba,  itacheza leo na timu ya  Singida Black Stars katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, kocha wa Simba Steve Barker alisema timu yao imejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa leo.

 “Huu ni mchezo mgumu na wenye changamoto kubwa kwani Singida ni timu bora na yenye wachezaji bora hivyo tutapambana mwanzo mwisho kupata ushindi katika mchezo huo muhimu,” alisema.

Barker alisema wanachokihitaji katika mchezo huo ni kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi watakazozipata na kuibuka na ushindi.

Mchezaji wa Simba, Antony Mligo alisema zinapokutana timu hizo mbili haiwezi kuwa mechi nyepesi.

Kocha Mkuu wa Singida Black Star, Muhibu Kanu alisema amekiandaa vizuri kikosi chake kiweze kupambana kupata ushindi.

“Tunaenda kutumia kaosoro za Simba, tupate matokeo mazuri, tayari tushakata tiketi ya kucheza michuano ya kimataifa, hivyo mechi zilizobaki ni za kusherekea mafanikio yetu,” alisema Kanu.

Mechi nyingine ni Azam Fc dhidi ya Coastal Union, Namungo Fc na Fountain Gate FC, Pamba Jiji na JKT Tanzania, Mashujaa FC kupambana na KMC, Tanzania Prisons ikimenyana na Mtibwa Sugar huku Dodoma Jiji ikipambana na Mbeya City.

Mechi zote hizo zitachezwa saa 10:00 jioni katika viwanja tofauti.

Previous Post

VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NI MARIDHIANO

NI MARIDHIANO

7 months ago
KIHONGOSI AWATAKA VIJANA KUTOKUBALI KUVURUGA AMANI

KIHONGOSI AWATAKA VIJANA KUTOKUBALI KUVURUGA AMANI

9 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?