• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 13, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Suleiman Jongo, Beijing – China

CHINA imezihakikishia nchi za Afrika kuwa, itaendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa lengo la kufanisha jitihada za kujiendeleza kichumi  na kupiga hatua kubwa za maendeleo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Shuai Guipeng, alipokuwa akizungumza kuhusu Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Sera ya Kuondoa Ushuru wa Forodha kwa Bidhaa za Afrika zinazoingizwa nchini humo, alipokutana na wahariri wa vyombo vya habari kutoka Afrika, jijini Beijing.

Wahariri hao wanahudhuria mkutano wa vyombo vikuu vya habari vya Afrika, ulioandaliwa na China ukiwa na mada mbalimbali kuhusu hatua za maendeleo zilizofikiwa na nchi hiyo na sera zake kuhusu ushirikiano na nchi zingine.

Shuai alisema nchi za Afrika zina nafasi kubwa ya kufikia ya kujiendeleza kutokana na uwepo wa rasilimali mbalimbali na kwamba serikali ya China itaendelea kushirikiana nazo kufanikisha hatua hiyo.

Alisema China imeendelea kuchukua hatua ikiwamo kuanzisha majukwaa ya ushirikiano kama FOCAS ambalo lengo lake ni kuzikutanisha nchi hizo kukaa pamoja kujadili changamo na fursa zilizopo kujiendeleza.

“China imeendelea kuwa mshirika wa kweli, wa karibu kwa nchi za Afrika kwa lengo la kusaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha ushirikiano wa watu.

“Tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo kuanzisha FOCAC jambo ambalo limeigwa na wengine. Tunavisihi vyombo vya habari kuwa daraja la kutambua na kufungua fursa zilizopo kwa maendeleo ya pande zote,” alisema.

Akitaja hatua nyingine zinazoendelea kuchukuliwa kuimarisha ushirikiano wa Afrika na China na kufungua milango ya maendeleo, alisema uamuzi wa kuziondolea ushuru wa forodha bidhaa za Afrika zinazoingizwa katika soko la China umeanza kuzaa mafunda kwa baadhi ya nchi kuongeza uwezo wake wa kuuza bidhaa za kilimo nchini humo.

Kwa mujibu wa Shuai, miongoni mwa nchi za mfano zilizotumia vizuri fursa hiyo ni Tanzania ambayo imeongeza mauzo yake baadhi ya bidhaa hususan za kilimo katika soko hilo.

Wakizungumzia ushirikiano wa China na Afrika baada ya kukutana na mkurugenzi huyo, baadhi ya wahariri walisema China ni rafiki wa kweli anayestahili kukumbatiwa kwa kuwa amekuwa bega kwa bega katika safari ya maendeleo ya nchi za Afrika.

“China ni rafiki wa kweli, anastahili kuwekwa karibu zaidi kwa maendeleo ya Afrika kupitia ushirikiano katika utatuzi wa changamoto na kufungua fursa,” alisema Angela Chishimba, Mhariri kutoka gazeti la Zambia Daily Mail la Zambia. Kwa upande wake Ezekiel Mwambopo kutoka kituo cha Televisheni cha Channel 10, Tanzania alisema alama za wazi zinazowekwa na China katika maendeleo ya Afrika ukiwemo mchango wake katika ujenzi wa miundombinu muhimu kama reli ya TAZARA, ni kielelezo tosha cha nia njema ya nchi hiyo kuona Afrika inainuka kiuchumi.

Previous Post

SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

Next Post

VYAMA 12 VYAKEMEA VIKALI UCHOCHEZI, CHUKI

Next Post
VYAMA 12 VYAKEMEA VIKALI UCHOCHEZI, CHUKI

VYAMA 12 VYAKEMEA VIKALI UCHOCHEZI, CHUKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

4 months ago
YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI

YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI

6 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?