• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU : TUUNGANE KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 17, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU : TUUNGANE KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania, taasisi za umma na binafsi, mashirika na wadau wa maendeleo waungane na Serikali katika kuwezesha matibabu ya upandikizaji wa figo na uloto kwa wananchi wasiokuwa na uwezo ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hizo za kibingwa.

“Hiki ni kitendo cha kiungwana, cha ibada na kinachogusa maisha ya Watanzania. Nawapongeza Umoja wa Wanawake Tanzania kwa kuitikia wito huu na kuwa sehemu ya kuokoa maisha ya wananchi,” amesema.

“Tunachokifanya leo ni kurejesha matumaini kwa wagonjwa na familia zao. Kila anayeguswa na jambo hili aendelee kushiriki ili wananchi wengi zaidi wanufaike na huduma hizi muhimu,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo jana (Alhamisi, Julai 16, 2026) katika hafla ya Okoa Maisha Gala iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kushirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa katika Ukumbi wa Mabele Hall, Jenerali Venance Mabeyo Complex, jijini Dodoma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu, kuongeza vifaa tiba na kuimarisha huduma za kibingwa ili Watanzania wengi zaidi wapate matibabu ya kiwango cha juu ndani ya nchi.

Awali, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za kibingwa nchini kwa kuimarisha miundombinu ya afya, vifaa tiba na rasilimali watu, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono Mfuko wa Matibabu ya Upandikizaji wa Figo na Uloto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Profesa Abel Makubi, amesema hospitali hiyo imefanikiwa kufanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 58 na upandikizaji wa uloto kwa watoto 31 wenye ugonjwa wa selimundu. Alisema kampeni hiyo inalenga kukusanya shilingi bilioni saba kwa ajili ya kusaidia matibabu ya wagonjwa na kupanua miundombinu ya huduma hizo.

Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Pius Chatanda, amesema umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha wadau na wananchi kushiriki katika juhudi za kuokoa maisha ya wananchi kupitia upatikanaji wa huduma bora za afya.

Katika hafla hiyo, jumla ya shilingi bilioni 2.225 zilipatikana kupitia michango na ahadi za wadau mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono Mfuko wa Matibabu ya Upandikizaji wa Figo na Uloto.

Fedha hizo zitatumika kusaidia matibabu ya wagonjwa pamoja na kuboresha miundombinu ya huduma za upandikizaji wa figo na uloto.

Previous Post

DK. MPOKI: WATAALAMU WAPEWE FURSA KUBORESHA MFUMO WA AFYA

Next Post

KUMEKUCHA ‘SIMBA DAY’ 

Next Post
KUMEKUCHA ‘SIMBA DAY’ 

KUMEKUCHA ‘SIMBA DAY’ 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

3 months ago
YANGA, SINGIDA, MLANDEGE MZIGONI TENA KIMATAIFA

YANGA, SINGIDA, MLANDEGE MZIGONI TENA KIMATAIFA

10 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?